Maulid Kitenge wa E-Fm huo uufanyao sasa siyo Utangazaji bali ni uswahili!

Maulid Kitenge wa E-Fm huo uufanyao sasa siyo Utangazaji bali ni uswahili!

Sijasema mimi ni FOLLOWER wako!! Watu si huwa mnaanzisha threads hapa jamvini? Na mkianzisha lengo lenu si ni kwamba wengine tusome? Sasa sisi wengine tukisoma huwa hatusahau mada wala jina la mleta mada hata kama muda umepita!

Na huwezi kuacha kumkumbuka Mtu ambaye ama HUMPENDI au UNAMPENDA hata siku moja. Jifunze Psychology utaligundua hili na unaweza ukawa FOLLOWER wa Mtu kwa mabaya au mazuri yake. Kwa mfano unaweza ukaamua tu umfollow ili uwe unampinga uridhike tu au ukaamua umfollow ili tu uwe unaelimika kwa madini yake adimu. Kwa ufafanuzi huu nadhani kidogo nitakuwa nimekutoa " tongo tongo " ya Kifikra.
 
Mnatusakama tunaoishi Dar, lakini cha ajabu ni kwamba mkifika tu huku mnaanza kuwatafuta akina Kitenge mpige nao picha, au majengo wanayofanyia kazi msimame mpige picha
Mimi nimezungumzia hicho kiredio chenu, hayo mengine yametoka wapi ewe mwanaume wa Dar?
 
Na huwezi kuacha kumkumbuka Mtu ambaye ama HUMPENDI au UNAMPENDA hata siku moja. Jifunze Psychology utaligundua hili na unaweza ukawa FOLLOWER wa Mtu kwa mabaya au mazuri yake. Kwa mfano unaweza ukaamua tu umfollow ili uwe unampinga uridhike tu au ukaamua umfollow ili tu uwe unaelimika kwa madini yake adimu. Kwa ufafanuzi huu nadhani kidogo nitakuwa nimekutoa " tongo tongo " ya Kifikra.
Nafuata habari of my interest and I don't care nani analeta habari husika! But if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote!
 
Uzi hauoneshi huo uswahili unaosema mhusika anao...ongezea nyama zaidi ili tufahamu huo uswahili ni upi...NB: Sio kila mtu anasikiliza Radio, hasa hasa EFM, particularly kipindi ulichokitaja...
 
Mkuu Gentamycine, mimi namfahamu Maulidi wa Kitenge na kipaji anacho yaani wa watambuzi wa vipaji twaita "potential".

Kama kweli msingi wa elimu yake hauko sawa basi hapo Efm alipo angeingia kusoma kwa kujiendeleza tena kwa mtu kama yeye anaweza kabisa kusoma huku akiendelea na kazi katika vyuo vizuri kabisa.

Au anaingia online kuchukua kozi kujiendeleza.

Rafiki zangu wengine kama Sunday Shomari na wengine walifanya hivyohivyo.
 
....hahahaha..popoma ungekuwa demu wallah usingeolewa!
..ila Kitenge 40+,ujana kashapita..,
....kama wewe tu!
 
Nafuata habari of my interest and I don't care nani analeta habari husika! But if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote!

Hata hivyo jibu lako tayari limeshatoa picha yako halisi juu yangu kitu ambacho nilikisema katika bandiko langu kuwa unaweza ukawa unanifuatilia kwa mazuri au mabaya na kwa sentensi yako hii ambayo nainukuu umesema " but if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote " mwisho wa kunukuu sentensi yako na jibu hapo umeliweka wazi kuwa unanifuatilia kwa CHUKI sasa ulichokuwa unazunguka na kutaka kupotezeana muda ni nini? au ulidhani nafanana na IQ yako hiyo ya " nzige? ". Halafu siku nyingine nakuomba andika tu kwa Kiswahili nitaelewa tu pia na kujua kuwa na Wewe ni msomi kuliko kukimbilia kuandika Kiingereza halafu unakikosea kosea. au umesahau kuwa wengine humu ni WORDSMITH? Haya tafuta haraka KAMUSI uangalie hilo neno lina maana gani na siku nyingine usije " kichwa kichwa " utaumbuka. Nakipenda mno Kiswahili changu na NAKITUKUZA sana.
 
....hahahaha..popoma ungekuwa demu wallah usingeolewa!
..ila Kitenge 40+,ujana kashapita..,
....kama wewe tu!

Hivyo hivyo na kwako Mkuu kama ingekuwa Wewe ni Demu nadhani kwa SURA yako ilivyo mbaya kama barabara mbovu ya pale Vigwaza sijui kama hata ungetongozwa labda kwa Wendawazimu ungewavutia.

Maulid Kitenge bado hajafikisha 40 kwani ni Mtoto wa juzi tu kama Wewe.

Kuhusu Mimi tafadhali usitake kunizeesha kihivyo bado hata sijafikisha hiyo 40 uisemayo ila nasubiria tu Christmas zangu tatu zijazo ndipo niifikie.
 
Umesahau mifano ktk madhaifu yake tafadhali.

Hivi kuna tofauti gani kati ya neno " mapungufu " na " madhaifu? ". Umesoma lakini UZI wangu wote vizuri na ukauelewa Mkuu? Hivi kwanini Watu huwa mnanitafutia tu sababu niwajibu vibaya halafu mkasirike? Nimekustahi tu kwakuwa ID yako ni dawa mwenzangu japo haina nguvu ila sasa hivi " ungeninunia ".
 
Hivyo hivyo na kwako Mkuu kama ingekuwa Wewe ni Demu nadhani kwa SURA yako ilivyo mbaya kama barabara mbovu ya pale Vigwaza sijui kama hata ungetongozwa labda kwa Wendawazimu ungewavutia.

Maulid Kitenge bado hajafikisha 40 kwani ni Mtoto wa juzi tu kama Wewe.

Kuhusu Mimi tafadhali usitake kunizeesha kihivyo bado hata sijafikisha hiyo 40 uisemayo ila nasubiria tu Christmas zangu tatu zijazo ndipo niifikie.
...teh hee hee....cha msingi umekubali usingeolewa!
...Kitenge wa juzi?.basi sawa!
..Xmass 3 si ushavuka ujana?.,au wajiona bado kigori?
 
Hivi kuna tofauti gani kati ya neno " mapungufu " na " madhaifu? ". Umesoma lakini UZI wangu wote vizuri na ukauelewa Mkuu? Hivi kwanini Watu huwa mnanitafutia tu sababu niwajibu vibaya halafu mkasirike? Nimekustahi tu kwakuwa ID yako ni dawa mwenzangu japo haina nguvu ila sasa hivi " ungeninunia ".
Hahahaha maisha yenyewe ni hayahaya xo cwez kukununia kwa jibu baya la siku moja kwani najua kesho utanijibu vizuri.

Nyuzi zako huwa ni ndefu sana xo kukumbuka baadhi ya maneno ni kazi kwelikweli.

Ahsante kwa kunistahi.
 
...teh hee hee....cha msingi umekubali usingeolewa!
...Kitenge wa juzi?.basi sawa!
..Xmass 3 si ushavuka ujana?.,au wajiona bado kigori?

Mimi niliye katika 30's zangu nikiwa Mzee " Babaako " anayeitafuta 101 atakuwa nani?
 
Aliokotwa tu pale Uwanja wa Taifa maeneo ya kwa " Mama Chichi " akiwa anabwabwaja bwabwaja tu masuala ya mpira na yule Kijana mwenzie aitwae " Kambarage " ambaye mpaka sasa yupo pale na akifanya tu Kazi za kulinda magari ya Watu wanaokunywa Bia au wanaokuja kuangalia mechi za VPL na za Kimataifa Uwanja wa Taifa ila zamani uhondo wote huu ulikuwa pale Uwanja wa Uhuru a.k.a Shamba la Bibi.

Watu waliomuibua Maulid Kitenge walikuwa ni Watangazaji akina Charles Nkwanga Hillary na mwenzie Abdallah Idrisa Majura ambapo kipindi walipokuwa Watangazaji wa michezo hasa hasa mpira wa Miguu wakiwa na RTD walikuwa wakimwona mno Maulid Kitenge pale Taifa akiwa anabishana na Watu kuhusu mpira huku akionekana ni mjuaji mzuri wa masuala ya " Kandanda " hivyo basi Watangazaji wawili hawa walipoahamia tu Radio One / ITV miaka ya 1993 hadi 1994 wakiwa na akina Mama Faudhiat Abood waliamua kumchukua Maulid Kitenge na kuanza kumpa ujuzi pale pale Radio One huku akiwa bado hajapewa vipindi lakini wakati huo huo Maulid akiwa ndiyo kamaliza Form Four yake ambapo kwa Heshima kubwa niliyo nayo juu yake sipo tayari kusema alipata ALAMA gani na itabaki kuwa SIRI yangu na kwa wale wanayoijua.

Hata hivyo baadae alipoonekana sasa ameiva ndipo Mzee Mzima Charles Hillary akamtambulisha rasmi katika Utangazaji na hapo ndipo nyota ya Maulid Kitenge ikaanza kung'aa hadi alipoanza kuteka mioyo ya Watu na kukubalika hasa kwa aina yake ya Utangazaji na Interviews zake ambazo kiukweli kama hukujiandaa vizuri unaweza ukaomba ardhi ipasuke uzame tu upotee.

Basi baada ya hapo ndipo Kijana wa Watu akazidi kuimarika na kuwa tishio hata kwa wale Watangazaji wasomi huku akipata bahati ya kupendwa na wenye kujua kupenda na mwenzetu sasa kabarikiwa hivyo ana nyumba mbili ambazo zote zina uhakika ( namaanisha hajaoa magubegube kama wengi wetu ) na ambapo amebahatika pia kuwa exposed katika dunia nyingine ambako sasa anaweza kusafiri kwenda " mamtoni " ambako wengi wetu tunaishia tu kupaona katika BBC Habari kila siku Saa 3 usiku huku wengine tukiishia tu kupaota na tukiamka tunajikuta tupo pale pale uwanja wa Fisi.

Hata hivyo yawezekana ubora wake umeongezeka maradufu kutokana na kwamba hata Wake zake alionao nao ni Wana Habari na Watangazaji maarufu hivyo kuna namna nao walivyomjenga hadi baadae Redio ya E fm ilipoanzishwa basi Kijana wa Watu akaonekana na kupewa dili ya maana na hatimaye kuamua kuachana rasmi na Radio One / ITV ambapo sasa ndiyo amekuwa Bosi wa Sports Desk / Department pale E fm.

Ni Kijana ambaye kama akijiendeleza hasa Kimasomo na kimaadili ya Kazi ya Habari na Utangazaji nina uhakika Tanzania ipo siku tutakuja kujivunia na Kazi zake kwani katika Tasnia nzima ya Habari na Utangazaji kuwapata akina Maulid Kitenge kumi ( 10 ) unaweza " ukasota " hata miaka 25 usiwapate kwani ana vitu adimu ambavyo kwa Watangazaji wengine havipo na hata vikiwepo basi ni full artificial.

Naomba niishie hapa tafadhali.

Mkuu nilisikiaga alizungusha jamaa ZIRO.

..Nchi yetu tuna tatizo moja hasa hawa wenye vipaji,kujiendeleza inakuwaga tabu kwao.Nafikiri labda wanakuwa wanahisi wameshamaliza kila kitu wanachokihitaji..
Chukulia mfano Millardo Ayo,Gardner G Habash na huyo Kitenge kama wote wangejiendekeza zaidi katika hizo fani zao leo Tanzania tungejivunia sana ktk nchi yetu.

Labda kwa ufupi wengi wao wqanaridhika mapema na mafanikio kidogo wanayoyapata.
 
wewe huwa una chuki binafsi..
watanzania hawataki kujadili mambo muhimu katika maisha, hii thread regardless of whether mtoa hoja ana wivu ama la, ni ya kujenga na ndio haswa lengo la social media. Hao wanaoipinga ni wapumbavu wasioitakia tasnia mema. Si jambo jipya kuwa watangazaji wengi, pengine 80% wa Tanzania hawana shule, na kwa bahati mbaya hata hizo shule zilizopo ni kichekesho. Kitenge si mtoto tena ni jitu zima lenye wake kadhaa, kupewa ushauri huu wa maana sana ni faida. Hao wanaotupia maneno kila siku kama vile wana template, si wanyamaze for once? mwingine anakubali kabisa kuwa mtoa hoja anaonekana kuwa na weledi wa profession, sasa inakuaje tena badala ya kuheshimu maoni anone ana wivu, hii ni typical situation ya workplace ambako watanzania mmeandelea kufanya vibaya, unapata ajira hutaki feedback, matokeo yake huwezi kutunza kazi, kila leo uko barabarani. Hongera mtoa feedback na wewe kitenge jifunze hapo maana uko karibu sana na ticket yako ya international broadcasting kama ukijirekebisha, otherwise utafia hapo efm, tumia hiyo opportunity ujiongeze kwa kuwa ni kweli shule huna
 
E fm kipindi chao kimekuwa cha kidaku sana yaani wanaonesha mapenzi yao live bila kuficha...poor kitenge na team tako
#Back to SportXtra
 
watanzania hawataki kujadili mambo muhimu katika maisha, hii thread regardless of whether mtoa hoja ana wivu ama la, ni ya kujenga na ndio haswa lengo la social media. Hao wanaoipinga ni wapumbavu wasioitakia tasnia mema. Si jambo jipya kuwa watangazaji wengi, pengine 80% wa Tanzania hawana shule, na kwa bahati mbaya hata hizo shule zilizopo ni kichekesho. Kitenge si mtoto tena ni jitu zima lenye wake kadhaa, kupewa ushauri huu wa maana sana ni faida. Hao wanaotupia maneno kila siku kama vile wana template, si wanyamaze for once? mwingine anakubali kabisa kuwa mtoa hoja anaonekana kuwa na weledi wa profession, sasa inakuaje tena badala ya kuheshimu maoni anone ana wivu, hii ni typical situation ya workplace ambako watanzania mmeandelea kufanya vibaya, unapata ajira hutaki feedback, matokeo yake huwezi kutunza kazi, kila leo uko barabarani. Hongera mtoa feedback na wewe kitenge jifunze hapo maana uko karibu sana na ticket yako ya international broadcasting kama ukijirekebisha, otherwise utafia hapo efm, tumia hiyo opportunity ujiongeze kwa kuwa ni kweli shule huna

Akhsante kwa kunielewa Mkuu kwani ni wachache sana ambao huwa mnanielewa humu labda pengine mna uwezo mkubwa wa kufikiri, kuchambua na kutathmini ambao wengi wetu humu umewapitia kombo. Post yako imenifariji mno na kunitia nguvu kuwa kumbe sijapoteza muda kuanzisha huu UZI. Ubarikiwe!
 
Siku hizi nitajitahidi kuwa makini na thread zako manake nimegundua zingine unazileta ama kuwapa watu promo au kuchimbachimba kwa mambo yako binafsi! Si ni wewe ambae uliwahi kuleta thread kuulizia kuhusu Tunu Hassan?! Au ulitaka watu wafunguke kwa mapana na marefu; kwamba anamegwa na fulani ili halafu ukaanzishe mtiti endapo huyo fulani sio wewe?!
Jerry Milo no 2
 
Back
Top Bottom