Maulid Kitenge wa E-Fm huo uufanyao sasa siyo Utangazaji bali ni uswahili!

Sijasema mimi ni FOLLOWER wako!! Watu si huwa mnaanzisha threads hapa jamvini? Na mkianzisha lengo lenu si ni kwamba wengine tusome? Sasa sisi wengine tukisoma huwa hatusahau mada wala jina la mleta mada hata kama muda umepita!

Na huwezi kuacha kumkumbuka Mtu ambaye ama HUMPENDI au UNAMPENDA hata siku moja. Jifunze Psychology utaligundua hili na unaweza ukawa FOLLOWER wa Mtu kwa mabaya au mazuri yake. Kwa mfano unaweza ukaamua tu umfollow ili uwe unampinga uridhike tu au ukaamua umfollow ili tu uwe unaelimika kwa madini yake adimu. Kwa ufafanuzi huu nadhani kidogo nitakuwa nimekutoa " tongo tongo " ya Kifikra.
 
Mnatusakama tunaoishi Dar, lakini cha ajabu ni kwamba mkifika tu huku mnaanza kuwatafuta akina Kitenge mpige nao picha, au majengo wanayofanyia kazi msimame mpige picha
Mimi nimezungumzia hicho kiredio chenu, hayo mengine yametoka wapi ewe mwanaume wa Dar?
 
Nafuata habari of my interest and I don't care nani analeta habari husika! But if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote!
 
Uzi hauoneshi huo uswahili unaosema mhusika anao...ongezea nyama zaidi ili tufahamu huo uswahili ni upi...NB: Sio kila mtu anasikiliza Radio, hasa hasa EFM, particularly kipindi ulichokitaja...
 
Mkuu Gentamycine, mimi namfahamu Maulidi wa Kitenge na kipaji anacho yaani wa watambuzi wa vipaji twaita "potential".

Kama kweli msingi wa elimu yake hauko sawa basi hapo Efm alipo angeingia kusoma kwa kujiendeleza tena kwa mtu kama yeye anaweza kabisa kusoma huku akiendelea na kazi katika vyuo vizuri kabisa.

Au anaingia online kuchukua kozi kujiendeleza.

Rafiki zangu wengine kama Sunday Shomari na wengine walifanya hivyohivyo.
 
....hahahaha..popoma ungekuwa demu wallah usingeolewa!
..ila Kitenge 40+,ujana kashapita..,
....kama wewe tu!
 
Nafuata habari of my interest and I don't care nani analeta habari husika! But if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote!

Hata hivyo jibu lako tayari limeshatoa picha yako halisi juu yangu kitu ambacho nilikisema katika bandiko langu kuwa unaweza ukawa unanifuatilia kwa mazuri au mabaya na kwa sentensi yako hii ambayo nainukuu umesema " but if you believe am your fun, then keep believing kv hainipunguzii wala kuniongezea chochote " mwisho wa kunukuu sentensi yako na jibu hapo umeliweka wazi kuwa unanifuatilia kwa CHUKI sasa ulichokuwa unazunguka na kutaka kupotezeana muda ni nini? au ulidhani nafanana na IQ yako hiyo ya " nzige? ". Halafu siku nyingine nakuomba andika tu kwa Kiswahili nitaelewa tu pia na kujua kuwa na Wewe ni msomi kuliko kukimbilia kuandika Kiingereza halafu unakikosea kosea. au umesahau kuwa wengine humu ni WORDSMITH? Haya tafuta haraka KAMUSI uangalie hilo neno lina maana gani na siku nyingine usije " kichwa kichwa " utaumbuka. Nakipenda mno Kiswahili changu na NAKITUKUZA sana.
 
....hahahaha..popoma ungekuwa demu wallah usingeolewa!
..ila Kitenge 40+,ujana kashapita..,
....kama wewe tu!

Hivyo hivyo na kwako Mkuu kama ingekuwa Wewe ni Demu nadhani kwa SURA yako ilivyo mbaya kama barabara mbovu ya pale Vigwaza sijui kama hata ungetongozwa labda kwa Wendawazimu ungewavutia.

Maulid Kitenge bado hajafikisha 40 kwani ni Mtoto wa juzi tu kama Wewe.

Kuhusu Mimi tafadhali usitake kunizeesha kihivyo bado hata sijafikisha hiyo 40 uisemayo ila nasubiria tu Christmas zangu tatu zijazo ndipo niifikie.
 
Umesahau mifano ktk madhaifu yake tafadhali.

Hivi kuna tofauti gani kati ya neno " mapungufu " na " madhaifu? ". Umesoma lakini UZI wangu wote vizuri na ukauelewa Mkuu? Hivi kwanini Watu huwa mnanitafutia tu sababu niwajibu vibaya halafu mkasirike? Nimekustahi tu kwakuwa ID yako ni dawa mwenzangu japo haina nguvu ila sasa hivi " ungeninunia ".
 
...teh hee hee....cha msingi umekubali usingeolewa!
...Kitenge wa juzi?.basi sawa!
..Xmass 3 si ushavuka ujana?.,au wajiona bado kigori?
 
Hahahaha maisha yenyewe ni hayahaya xo cwez kukununia kwa jibu baya la siku moja kwani najua kesho utanijibu vizuri.

Nyuzi zako huwa ni ndefu sana xo kukumbuka baadhi ya maneno ni kazi kwelikweli.

Ahsante kwa kunistahi.
 
...teh hee hee....cha msingi umekubali usingeolewa!
...Kitenge wa juzi?.basi sawa!
..Xmass 3 si ushavuka ujana?.,au wajiona bado kigori?

Mimi niliye katika 30's zangu nikiwa Mzee " Babaako " anayeitafuta 101 atakuwa nani?
 

Mkuu nilisikiaga alizungusha jamaa ZIRO.

..Nchi yetu tuna tatizo moja hasa hawa wenye vipaji,kujiendeleza inakuwaga tabu kwao.Nafikiri labda wanakuwa wanahisi wameshamaliza kila kitu wanachokihitaji..
Chukulia mfano Millardo Ayo,Gardner G Habash na huyo Kitenge kama wote wangejiendekeza zaidi katika hizo fani zao leo Tanzania tungejivunia sana ktk nchi yetu.

Labda kwa ufupi wengi wao wqanaridhika mapema na mafanikio kidogo wanayoyapata.
 
wewe huwa una chuki binafsi..
watanzania hawataki kujadili mambo muhimu katika maisha, hii thread regardless of whether mtoa hoja ana wivu ama la, ni ya kujenga na ndio haswa lengo la social media. Hao wanaoipinga ni wapumbavu wasioitakia tasnia mema. Si jambo jipya kuwa watangazaji wengi, pengine 80% wa Tanzania hawana shule, na kwa bahati mbaya hata hizo shule zilizopo ni kichekesho. Kitenge si mtoto tena ni jitu zima lenye wake kadhaa, kupewa ushauri huu wa maana sana ni faida. Hao wanaotupia maneno kila siku kama vile wana template, si wanyamaze for once? mwingine anakubali kabisa kuwa mtoa hoja anaonekana kuwa na weledi wa profession, sasa inakuaje tena badala ya kuheshimu maoni anone ana wivu, hii ni typical situation ya workplace ambako watanzania mmeandelea kufanya vibaya, unapata ajira hutaki feedback, matokeo yake huwezi kutunza kazi, kila leo uko barabarani. Hongera mtoa feedback na wewe kitenge jifunze hapo maana uko karibu sana na ticket yako ya international broadcasting kama ukijirekebisha, otherwise utafia hapo efm, tumia hiyo opportunity ujiongeze kwa kuwa ni kweli shule huna
 
E fm kipindi chao kimekuwa cha kidaku sana yaani wanaonesha mapenzi yao live bila kuficha...poor kitenge na team tako
#Back to SportXtra
 

Akhsante kwa kunielewa Mkuu kwani ni wachache sana ambao huwa mnanielewa humu labda pengine mna uwezo mkubwa wa kufikiri, kuchambua na kutathmini ambao wengi wetu humu umewapitia kombo. Post yako imenifariji mno na kunitia nguvu kuwa kumbe sijapoteza muda kuanzisha huu UZI. Ubarikiwe!
 
Jerry Milo no 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…