sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nguvu moja hatukatai, Lakini sasa kwa hali hii uongozi wa Simba mmeanza kutukatisha tamaa asiee, Ni kivipi deal ya Manzoki imebuma ?? ......
nimeanza kuamini hata maneno ambayo sipendi kuyaamini ya mitandaoni na vijiweni kwamba uongozi wamegeuza timu iendeshwe kibahili bahili kwa lengo la kutengeneza faida zinazoenda kudhamini miradi ya familia ya wamiliki.. Kwamba Simba kwa sasa hawataki kununua wachezaji wa gharama kwa kuhofia hawataweza kurudisha pesa ya usajili na mishahara pindi wakija kuuzwa hapo mbele, kwamba wanapenda kusajili wachezaji wa bei rahisi ili waje kuuzwa kwa faida kama Miqson, Kuna tetesi kwamba hata mishahara inapungua kwa lengo la kuongeza faida inayoenda kwenye miradi ya familia.
Nimepata taarifa iliyonipa mstuko wa moyo na kuniharibia mood yangu baada ya kupata habari dakika chache zilizopita kwamba Yanga wameweza kuinasa saini ya Manzoki kwa kutia kitita cha mlioni 466 , Hizi ni pesa ambazo naamini kabisa Simba inaweza kumudu lakini tatizo ni kwamba huenda ubahili wa kutaka faida kubwa kuliko mafanikio ya Simba ndio umeponza dili likabuma.
Maumivu ni makali sana kwakweli