Maumivu ya mwanamke kusalitiwa: Hana wa kumtetea, jamii inaona ni haki yake

Maumivu ya mwanamke kusalitiwa: Hana wa kumtetea, jamii inaona ni haki yake

Sasa mbona mnaringa?
Ukimuambia mke wa ndoa geukia huku muda wa usiku ataanza kutoa visingizio visivyo na miguu, Mara naumwa na tumbo, au siko kwenye mood au nimechoka. Mwanamke Kama huyo atakosa kusalitiwa?
Siku akiamua kukupa Ni Kama anakufanyia favour, kwa Hali hii mwanamme utaacha kua na mchepuko?
Wanawake up your game na hatasalitiwa....
 
Sio kwamba jamii imemjengea mwanamke huo mtazamo, hii ni nature tokea dunia imeanza mpaka leo hii kuanzia kwenye vitabu vya dini mpaka kwenye history za kiafrika polygamy ndo utaratibu, hivyo jamii imemnyanganya mwanaume haki ya kuwa na wake wengi na matokeo yake ndo haya uliyoyaandika.
Haki tunyimwe sisi nyie ndo mnalalamika
Jamii ipi imemnyang’anya Mwanaume haki ya kua na Wake wengi🤷‍♀️🤷‍♀️
 
"Jamii imekuwa ikihubiri kuwa mwanaume anahaki ya kuchepuka"

"Imekuwepo kampeni kuwa mwanamke anayevumilia mwanaume wake kuwa na michepuko ni mke anayefaa na kwani hujena familia,

Kwa haya sikubaliani nawe kwani wenye hofu ya Mungu hatuwezi kushabikia haya wala kusema kuwa ni haki ya mwanaume kuchepuka

Hao wanaofanya kampeni au hiyo jamii unayoisema labda ni secret society lakini hawapo hadharani na mabango au hiyo kampeni unayosema

Mwanamke aheshimiwe kama mama na mzazi pia Ana heshima yake kwenye jamii na anaemdharau na kuchepuka eti ni haki yake basi atakuwa ana laana huyo
Asante kwa kulitambua hilo
 
Taasisi zote hizo bado unasema hana wa kumtetea? Na mwanaume ambaye anasalitiwa anatetewa na nani?

Mimi naamini katika mfumo dume tu ndo una haki

Kama kuna kosa mwanadam alifanya hasa mwanaume ni kukubali mambo ya haki sawa!
Hili jambo kwa Mungu hakutaka liwe hivyo na shetani alivyo vile alivyotukataza Mungu ndipo hapo hapo shetani anapita na kukuonyesha sio vibaya kufanya alichokaza Mungu!
 
Uchepakaji ni matokeo ya kukiuka asili yetu!
Mi ni mkristo nikisoma biblia na historia ya mababu zetu kuna vitu hatupati kama wazee wetu wa imani na babu zetu walivyopata matokeo yake tunajikuta turudi kwenye asili yetu kwa kujificha (kuchepuka)

Mfano:
wazee wetu wa imani walikuwa na mke zaidi ya mmoja na mambo yalikuwa sawa.
Ibrahimu - sala na hajiri tena sala ndo msuka mambo
Yakobo - Leah na Raheli watoto wa uncle’ ake
Daudi - alikuwa nao wengi tu ila hawakumtosha
Suleman - idadi ya wake mnaijua

Hao ni ambao tumepewa history zao, je ambao taarifa zao hazipo kwenye biblia au hawakuwa maarufu?

Ok historia ya babu zetu huko nyuma mnazijua

Kwa hiyo mkoloni alivyokuja kututawala na mila zetu nazo alizibadili ndo hizo leo hii kwa sababu ya uasili huo tunajikuta tu automatic unakuwa na ziada ya mke make huyo mmoja ulo nae hatoshi!

Ni vile umekuta haki za wanawake zimejitokeza leo hii ila naamini ungekuwepo enzi za mababu we ndo ungewashauri wanawake wengine wasililie ulichoandika
 
Napenda kwa moyo wangu wote. Mahali kwenye mapenzi hisia ni 100%.
Penzi likifa najipa nafasi nyingine ya kupenda. Nina mapenzi tele tele
Huwezi ukamfumania mumeo alafu ukajisikia amani moyoni kama uko vzuri kihisia. Tatizo mnaficha maumivu
 
Yanahitajika mafundisho ya saikolojia ya mahusiano miongoni mwa jamii zetu.

Watu wanaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa wamejaa mapokeo na ujinga mwingi.

Ujinga ukiondoka maumivu yatapungua sana au kwisha kabisa .

Mauaji hayatasikika kabisa.
 
Back
Top Bottom