Unajua mwanamke hasalitiwi kwa mwanaume kuwa na mke mwingine bali mwanamke anasalitiwa pale mwanaume anapoacha kumpenda na kumtelekeza na kutokumzingatia kama mke wa ndoa tena.
Kama ni kweli mwanamke anasalitiwa kwa mwanaume kuwa na mwanamke mwingine pembeni yake nitakuuliza maswali;
Je, unafahamu kuwa imani ya kiislam inahusisha Ndoa ya mke zaidi ya m'moja yaani wake hadi kufikia wa4, so unataka kutuambia kuwa waslam na imani yao inaruhusu usaliti?!
Kama wanawake wanachukulia mwanaume kuwa na mwanamke mwingine pembeni yake ni usaliti, je, umeshawahi kujiuliza kwann wanawake wengi wapo tayari kutembea na mume wa mtu na wakijua wazi ana mke wake? Ingekuwa wanawake wanasalitiwa kwa mwanaume kuwa na mwanamke mwingine pembeni yake then hakungekuwa na mwanamke ambaye anakubali kutongozeka au kuwa side chick au baby moma wa mume wa mtu.
Kama wanawake wanasalitika kwa mwanaume kuwa na mwanamke zaidi yake then kusingekuwa na Ndoa za mitaala a.k.a ndoa za wake wengi yaani wake kumi na zaidi.
Nadhani umezungumza hoja zako kwa kutumia hisia bila kuzingatia uhalisia.
Haya uliyosema yanatokana na mfumo wa mataifa ya magharibi ya kumuaminisha mwanamke kuwa anaweza kuwa na mwanaume wa pekee yake. Na ndio maana ndoa hazikaliki miaka hii.
Mwanamke ni monogamy kwa mwanaume ila mwanaume ni polygamous kwa wanawake. Mwanaume hawezi kunest na mwanamke m'moja maisha yake yote unless apate mahitaji yake muhimu kwa huyo mwanamke pekee jambo ambalo ni gumu sana.
Jiulize swali moja, mwanamke anahitaji vitu gani kwa mwanaume wake na mwanaume anahitaji nini kwa mwanamke wake?!
Mwanamke anahitaji sana matunzo more than anything kwa mwanaume na ndio maana kujihakikishia hilo wakajijengea hii fikra ya kuwa na mume wa pekee yake ili aweze pata hiyo attention na matunzo pekee yake maana ndio kitu muhimu kuliko vyote.
On the other hand mwanaume anataka attention ya mwanamke wake ila haihitaji. Ukitaka kuprove hiyo mwanamke awe anamzonga mwanaume muda wote utaona mwanaume anavyolalamika kuwa mke anamkera sababu ya too much attention.
Mwanaume anataka akihitaji attention apewe muda anataka then akiwa anataka privacy apewe pia ili awe karibu na mwanamke anayetaka.
Na jambo lingine, tazama mahusiano, ni lazima utakuta mwanaume ana mke ila lazima awe na demu wa nje amempangishia au anampa mahitaji na mke hawezi jua hadi afuatilie au mwanaume awe hana heshima na mkewe tu amuonyeshe kinachoendelea. Ila mwanamke akithubutu kufanya mahusiano nje ya Ndoa yake yaani hata awe msiri vipi itajulikana haraka sana na atabainika.
Kwa kuhitimisha naomba nikwambie kuwa mwanamke hasalitiwi na mwanaume kwasababu mwanaume ana mwanamke mwingine pembeni. Bali mwanamke anasalitiwa na mwanaume pale tu mwanaume anapomtelekeza na kumpotezea mwanamke wake na kumpa hadhi au privilege mwanamke mwingine nje ya huyu ambaye anastahiki kupewa heshima ya mke.
Kwa upande mwingine, mwanamke ndie ambaye akianzisha mahusiano na mwanaume mwingine by principle anakuwa amesaliti na kuharibu mahusiano.