Mauzauza: Alichojibiwa Makonda kero ya Iringa ni ile aliyotishia kumpiga kibao Naibu Waziri

Mauzauza: Alichojibiwa Makonda kero ya Iringa ni ile aliyotishia kumpiga kibao Naibu Waziri

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Wakuu heshima kwenu.
Poleni na msiba mkubwa sana wa kitaifa wenye historia kubwa hapa JamiiForums. Nipende kuwakumbusha kuwa akiwa ziarani Iringa ndugu Makonda alikutana na KERO ya wafanyakazi kiwanda cha karatasi mgololo ambapo kwa miaka 20 wafanyakazi hao wamekuwa wakiidai serikali mafao yao. Naomba niambatanishe uzi unao zungumzia tukio Hili.


 Ikumbukwe
Naibu waziri alipopatikana alieleza kuwa wafanyakazi hao waliwahi kulipwa jambo ambalo ni Uongo mkubwa. Ni muhindi tuu aliwalipa wafanyakazi hao ambao walimtumikia kwa miaka miwili.

Ikumbukwe
Siku hiyo mwenyekiti wa CCM mkoa alisema mbele ya makonda kuwa hajui jambo Hilo (tazama video kwenye uzi hapo)

Ikumbukwe
Makonda alilaumu ucheleweshaji wa kesi hiyo. Alimuagiza waziri huyo kushiriki kikao cha wafanyakazi na DC siku ya jumatano tarehe 14 yaani Leo.

MAJIBU
  • Mwenyekiti CCM mkoa aliomba kikao jumatatu tarehe 12 ili aombe radhi kwa wanamgololo kwa maana aliongea uongo mbele ya makonda kwani alisema hajui changamoto hiyo wakati anaifahamu vizuri. Kikao hicho kilikutana pia kujibu usuruhishi wa mgogoro huo.
  • Katika kikao hicho naibu waziri viwanda ambaye pia ni mbunge wa watu hao hakuona umuhimu wa kutii agizo la Paul Makonda. Hakuhuudhuria anautwa Mh Kihenzile.
  • Katika kikao hicho eti DC alisema yeye ameteuliwa na Mama na hawezi kumuangusha. Alisema kuwa atarudisha jambo hilo mahakamani ili iweze kuliendesha kwa haraka kwani mahakama ndio inachelewesha. Eti mtuhumiwa ataiomba mahakama iendeshe kesi kwa haraka ili ahukumiwe mapema.
*Kigogo wa muda mrefu kiwandani hapo mzee chogo alikumbushia kuwa mwaka 2011 mahakama iliamuru wafanya kazi hao walipwe serikali ikasema kikwazo ni muhindi ambaye hayupo tayari kulipa. Muhindi akawalipa wafanyakazi hao ila serikali bado inaendeleza makida makida mahakamani. Alieleza kuwa wafanyakazi zaidi ya 200 wamekufa vifo vya mateso kutokana na ugumu wa maisha familia zao zinaishije? Alisema mwaka jana wameipa serikali billion 200 kutoka kiwandani hapo ni kwanini wasitoe hizo billion 14 wawalipe watanzania hao wasio na hatia.

Mwisho
kinachoendelea mgololo ni kilio tuu hakuna cha maana kilicho fikiwa

Kwa mawazo yangu
Sheria imetoa room kwa mashauri ya madai muda wowote kusikilizwa nje under the umbrella of ADR. Wanasheria katili wa serikali hawajui hili.

Ni nani mbabe anaye zuia malipo ya wafanyakazi kiwanda cha karatasi mgololo?

download (1).jpeg


Mufindi paper Mills the factory in Iringa formerly Southern paper Mills built under mwalimu's administration 1980's
 
Kikao Cha DC na wafanyakazi hao kimeamua nini mkuu
 
Kikao Cha DC na wafanyakazi hao kimeamua nini mkuu
Amesema DC ataiamuru mahakama Imalize kesi hiyo mapema. Watu wamefedheheka sana hakuna mwanqmgololo Anae muongelea vizuri DC
 
Makonda hana na hatakuwa na suluhu na matatizo ya watanzania.
Wanaoenda kumsikiliza hawana tofauti na wanaoenda kwa MWAMPOSA
 
Amesema DC ataiamuru mahakama Imalize kesi hiyo mapema. Watu wamefedheheka sana hakuna mwanqmgololo Anae muongelea vizuri DC
Rais aingilie kati wananchi hawa wapate haki yao. Hizi janja janja sio sahihi.
 
Back
Top Bottom