Ironbutterfly
JF-Expert Member
- Feb 5, 2023
- 3,042
- 8,227
- Thread starter
-
- #21
Mizimu=WAFU=KUZIMU.Ndugu yangu sifahamu namna ya kuziombea ndoto kibibilia,na isitoshe ndoto za wazee wangu naziota sana,sielewi tatizo ni nini,nimeuliza baadhi ya watu wazima wamenambia Nina mizimu ya ukoo,so sielewi ndugu,labda unisaidie jinsi ya kudil nazo.
Achana na mambo ya udi
Sasa oud na kusali mbona mbingu na ardhi..au mie mgeniMie mwanamke na nasali sana
Ah wapi...sidhani...huenda amewakumbuka usiku lazima awaoteWhy usihame?mbona hili ndo jepesi kuliko yote??
Kama tatizo ni nyumba, basi yakupasa kuvunja maagano yote yaliyowekwa kwenye hiyo nyumba,, mtumaini Bwana kwa moyo wako wote naye atayanyoosha mapito yako.Sijachanganya lolote,damu ya Yesu nilitamka usingizi wakati nakabwa.Hii nyumba nimeambiwa aliyekuwa anaishi alikuwa mganga na alikuwa anaitumia kuagulia watu.Muda sio mrefu katoka kunipigia,sikuwa kwenye mazingira ya kupokea,nikitoka job ntampigia nione alikuwa ananitafutia nini.
UKWELI ni mchungu,Mie ni mkristo Mkatoliki,mwanachama wa Shirika la moyo mtakatifu wa Yesu,naamin katika ukombozi kupitia damu ya Yesu iliyomwagika msalaban na kuleta wokovu.Sala nyingi nisalizo zinaangukia ktk kuitaja damu ya Yesu 🙏
Solution ni kuhama.Kama tatizo ni nyumba, basi yakupasa kuvunja maagano yote yaliyowekwa kwenye hiyo nyumba,, mtumaini Bwana kwa moyo wako wote naye atayanyoosha mapito yako.
Hili ndo jibu...Dk isaac aliwahi fafanua mambo ya ubongo ..ninaona uvivu kuandikaInaonekana una wawaza sana
Hizo ni IBADA za mizimu.Kuna maelezo natamani nkuandikie ila nahs huta nielewa ila nenda kanisan waombee Misa hata zile za asubh kwa majina Yao mana kuota wanakuomba soda n kwamba wanakiu ya kua karbu na ww au kujumuika pamoja na ww waombee Misa wapate kupumzika mahali pema na roho zao zkae toharan pili udi na uban n chakula kwa viumbe wanao onekana na wasioonekana kwaio acha kutumia mana n kama unawaendekeza watakusumbua sana mwsho wa siku wataivuta nafs yako walipo mana wao n roho,nafs kwa sasa ndio mana mpka ulale ndio nafs yako inaweza kuwasiliana nao kama kwenu mna mila na amjasimama vzur katiba ibada chukua maziwa kwa ajil ya uyo anaeomba soda na pombe kwaajili ya baba kama alikua anatumia kunywa kidogo uku ukinena Kisha mwaga chin ardhin ukiwataja majina like wazee wangu karibuni kwa hik kidogo japo mpate na nyie Kisha mkapumzke kwenye makao yenu unakunywa na kumwaga chin apo shughuli imeisha na pombe ya mazao sio kvant
Umeianzisha vita ngumu ambayo hutaishinda.Habari za asubuhi wanaJF, hope tumeamka salama kwa uweza wa manani🙏
Wiki kama mbili nilikuwa nasumbuliwa na ndoto za kuhusu wazee wangu (RIP, manake wote walishatangulia mbele za haki), walikuwa wananijia ndotoni wakiomba niwapatie vinywaji, sehemu nyingine niliota napeleka vyakula,wakaniomba na vinywaji, specifically soda, aliniomba Bibi mzaa mama.
Yani nilikuwa naona ndoto za kuwahusu wao na ndugu wengine walio hai katika familia. Ni wiki niliyokuwa najihisi huzuni na upweke sana bila sababu.
Basi Jumatatu nilipotoka job nikaenda kwenye msikiti wa jiran Kuna duka la dawa za kisuna nikanunua udi flan hivi huwa unatumika kuombea watu waliotangulia mbele za haki. Nikarudi nyumbani nikaoga, nikala then nikauchoma nikiwaombea pumziko hasa Bibi na mama, then kwenye saa kumi na moja nikalala,nimejiwekea utaratibu wa kulala mchana nikiwa free.
Ndani ya nusu saa toka nilale nikaota mwanamke mmoja mtu mzima kavaa upande wa kanga kajifunika Hadi kifuani, kasimama dirishani mwa chumba changu lakini kanipiga mgongo, hivyo sikumwona sura,then nikastuka toka usingizini, nikabadil upande nikarud kulala, this time kama nusu saa baadae nikaota nakabwa pumzi na mtu nisiyemwona huku amenikandamiza kichwa chini,nikawa napambana kujinasua huku nikitaja damu ya Yesu niokoe, nilihangaika kwa muda then akaniachia na nikaamka ghafla. Sikulala tena, nikaamka na kuendelea na ratiba nyingine ya kumalizia siku.
Kulipopambazuka, nikajiandaa, nikachoma udi then nikaingia mzigon, then saa 11 baada ya muda wa mkoloni, nikaenda sokon nikanunua chumvi ya mawe nikarudi home nikaipigia deki chumbani na sebuleni. Nikachoma na udi ule wa kuwaombea wazee wangu, nikaendelea na ratiba nyingine na hali ikaendelea kuwa shwari hata zile ndoto zikakata.
Kimbembe nimeamka leo nikajiandaa niende job, kabla sijatoka natafuta udi zangu zilizobaki nichome sizioni, nimekagua kote sijaziona, na ninaishi peke yangu, hii nyumba Ina usalama wa kutosha, nimebaki na bumbuwazi. Hapa nimepanga nikitoka job nikanunue za kutosha pamoja na ubani, manake hii nyumba nina wiki tu toka nihamie. Maoni yenu wadau.
Nami nimemwambia kuwa vita hii hataishinda.Nimesema unachanganya sbb unatumia udi!
Ww unaemwamimi Yesu hutakiwi kutumia hivyo vitu.
Sawa mpendwa, nyumba Ina madhabahu za kiganga hiyo km kulikuwa na hizo kazi hapo, lkn na we hizo ndoto Zinaonyesha Kuna shida!
Kuna mdau kakuuliza swali zuri hapo unaufahamu ,uelewa kuhusu damu ya Yesu na namna ya kuitumia?
Mi nakuuliza una uelewa kuhusu ndoto kibiblia na namna ya kuziombea?
Sawa,Kuna ushauri juu hapo juu wa mdau ,uzingatie pia kadri unavyosikia ndani yako.Ndugu yangu sifahamu namna ya kuziombea ndoto kibibilia,na isitoshe ndoto za wazee wangu naziota sana,sielewi tatizo ni nini,nimeuliza baadhi ya watu wazima wamenambia Nina mizimu ya ukoo,so sielewi ndugu,labda unisaidie jinsi ya kudil nazo.
Ngoja tumsaidieNami nimemwambia kuwa vita hii hataishinda.
Mungu hachanganywi na miungu
Sina miungu ndugu yangu 🙏 nahisi huo udi umeenda kuamsha ishu za watu🤣saiv nimetoka kuongea na mwenye nyumba kanambia atakuja hapo home kesho tuongee,manake yeye anaishi kijijin huko,hii nyumba kaijenga mjini ya kupangisha🙏 ni msukuma🤣🤣Nami nimemwambia kuwa vita hii hataishinda.
Mungu hachanganywi na miungu
Sawa,Kuna ushauri juu hapo juu wa mdau ,uzingatie pia kadri unavyosikia ndani yako.
Biblia inasema ...hakuna ushirika kati walio hai na wafu....
Lkn pia kuota watu waliokufa,inaweza kuwa ni roho ya mauti inakufuatilia!
Na hiyo roho ya mauti sio lzm iwe kufa Kifo Cha kimwili tu hata kiroho hata kwenye mambo yako ,km uchumi, familia unaweza ona Kila kitu hakiendi...nk
Wakati mwingine inakuwa Kuna kitu wanataka kukurithisha vitu....
Biblia inasema kwenye Waebrania ....agano la urithi lilipo Iko mauti..
Soma Waebrania 9 yote, itakusaidia..
Ngoja tumsaidie