Mauzauza: Nasumbuliwa na ndoto za kuhusu wazee wangu

Mauzauza: Nasumbuliwa na ndoto za kuhusu wazee wangu

Solution ni kuhama.

Nyumba hakuijenga Yeye iweje avunje mikataba ya nyumba ya mtu mwingine ambaye anaamini mikataba hiyo ni halali sawasawa na miungu yake?

Tupambanie tujenge nyumba zetu na tumkabidhi Mungu wetu azilinde, au ahamie nyumba ya watu wenye mikataba na madhabahu inayoendana na Imani ya Mungu wake.

Amen
Sawa mkuu.
 
Shukran ulosema Kuna ukwel ndani yake
Pole, ila Usichanganye Imani kama unatumia udi, chumvi, ubani, hirizi na vinginevyo tumia hivyo tu.

Na kama unamkiri Yesu Kristo Bwana au damu yake hakikisha una uhalali wa kulitumia. Uwe safi hakuna chochote kitakacho kusumbua maana yeye hachangamani na yeyote.

Jina lake na Damu yake linajitoshereza kukusaidia maana yeye ndio njia ya kweli na uzima huwezi fika kwa Baba bila kupita kwake.

Halafu hayo mandoto ya mababu, wazazi, mke au ndugu waliokufa kiimani sio ishara nzuri kwani hakuna ushirika kati ya wafu na walio hai ni roho zinazotaka kukurudisha nyuma na kupooza mambo na mipango yako
 
Hakuna vya kunirithisha wazee wangu walikuwa watu wa ibada sana 🙏 nahisi hii nyumba Ina kitu hakiko sawa
Uko tayari kujifunza mpendwa?
Nikisema kurithishwa Sina maana mikoba sijui ya uchawi km watu wengi wanavyojua...,ndo maana nimekuuliza ulishawahi pita shule ya ndoto kibiblia?
Umesema hapana!
So ni vzr kuuliza ambacho hujaelewa kuliko kubisha!

Kwenye kurithishwa Kuna vingi ,Kuna viti vya enzi hapo,Kuna tabia ,yaani ni vingi....
Kuhusu kuwa walikuwa watu wa Ibada Mungu ndo anaejua mpendwa
 
Sijachanganya lolote,damu ya Yesu nilitamka usingizi wakati nakabwa.Hii nyumba nimeambiwa aliyekuwa anaishi alikuwa mganga na alikuwa anaitumia kuagulia watu.Muda sio mrefu katoka kunipigia,sikuwa kwenye mazingira ya kupokea,nikitoka job ntampigia nione alikuwa ananitafutia nini.
Hayo mambo huwa hayampati mtu hivi hivi bila ya yeye kuwa na connection na vitu hivyo, inaonesha hiyo nyumba ina negative energy zimeweka makazi humo, solution ni kuhama tu hapo afu ili zisikufuate huko uendako endelea kuwa na imani uliyonayo, hayo maviumbe huwa yanamuogopa sana JESUS CHRIST.
 
Sina miungu ndugu yangu 🙏 nahisi huo udi umeenda kuamsha ishu za watu🤣saiv nimetoka kuongea na mwenye nyumba kanambia atakuja hapo home kesho tuongee,manake yeye anaishi kijijin huko,hii nyumba kaijenga mjini ya kupangisha🙏 ni msukuma🤣🤣
Ushauri wangu.
Simama na Mungu unayemwamini atakushindia.
Hiyo sio nshu ngumu mbona?

Udi na damu ya Yesu ni mbingu na ardhi mama/rafiki
 
Ushauri wangu.
Simama na Mungu unayemwamini atakushindia.
Hiyo sio nshu ngumu mbona?

Udi na damu ya Yesu ni mbingu na ardhi mama/rafiki
Yap nimeaxhana na ishu za udi na kuhama sihami,nishalipa miezi 6 kamili halafu hakuna refund
 
Ndugu yangu sifahamu namna ya kuziombea ndoto kibibilia,na isitoshe ndoto za wazee wangu naziota sana,sielewi tatizo ni nini,nimeuliza baadhi ya watu wazima wamenambia Nina mizimu ya ukoo,so sielewi ndugu,labda unisaidie jinsi ya kudil nazo.
Anyway,ngoja nifupishe....
Wengine washambia huko juu, si Kila mtu ana uhalali wa kutumia Damu ya Yesu km hajamkiri(kuokoka)
Ndo Maana Kuna walipkushauri uokoke huko juu Ili uwe na uhalali wa kutumia Damu ya Yesu.

Baada ya hapo, fuata hatua hizi
Toba..Sababu Kuna mlango ulisababisha wapate uhalali huo wa we kuota hayo mandoto...Zaburi 51 yote, Daniel 9:1-13..
tubu Kwa ajili ya huo mlango kutumia na adui...
Jitenge na hao waliokufa... biblia inasema,hakuna usharika kati ya walio hai na wafu ...(nimesahau mstari hapa nakutafuta nitarudi kuweka)
Hapa ss utaachilia Damu ya Yesu Kwenye lango lako la ndoto Ili lisipitoshe Tena hizo ndoto hizo.
 
Yap nimeaxhana na ishu za udi na kuhama sihami,nishalipa miezi 6 kamili halafu hakuna refund
Kuna namna ya kuombea ardhi hiyo ,ila ss mpaka uwe na hayo maarifa ya namna ya kuomba bila kugombana na hiyo miungu ....
Tena unaombea chumba chako tu basi wala sio issue.
 
Endelea kuwapelekea moto wa damu ya Yesu mpaka wahame wao
Mimi Wala siondok na Nina nguvu za kuwashinda manake nilipoita damu ya Yesu ndotoni nilishinda na wakaniachia,kesho mwenye nyumba kanambia anakuja,halafu ajabu kanitafuta mwenyewe bila mimi kumtafuta namsubir nimsikilize na nitamwelezea kuhusu huyo mpangaj alotoka kama vipi aje atoe mizigo yake aliyoiacha 🙏
 
Aombe ulinzi kwa kiumbe alie shindwa kujilinda na kuokoa maisha yake binafsi?.
Yesu ndiye anayekupa PUMZI Bure.

Uwe na Akiba ya maneno Yako.

(Yohana 1:1-14). Says:

Hapo Mwanzo kulikuwa NENO, naye NENO alikuwako Kwa Mungu, naye NENO alikuwa Mungu,

Vyote vilifanyika kupitia Yeye, na pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.

Ndani yake ndimo ulimokuwa Uzima, na ule Uzima ulikuwa Nuru ya watu, nayo NURU yangaa gizani, Wala Giza halikuiweza.

9. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye Nuru Kila mtu akija ULIMWENGUNI.

10. Alikuwako ULIMWENGUNI, hata Yeye Ulimwengu ulipata kuwako, Wala Ulimwengu
haukumtambua.

11. Alikuja kwake,Wala Walio wake hawakumpokea.

14. Naye NENO alifanyika mwili akakaa kwetu, nasi tukaona Utukufu wake, kama Utukufu wa mwana pekee atokaye Kwa Baba, amejaa neema na Kweli.

NB: Yesu alikuja Kwa Kila mtu avutaye PUMZI, Si Kwa Dini Fulani pekee.

Amen
 
Habari za asubuhi wanaJF, hope tumeamka salama kwa uweza wa manani🙏

Wiki kama mbili nilikuwa nasumbuliwa na ndoto za kuhusu wazee wangu (RIP, manake wote walishatangulia mbele za haki), walikuwa wananijia ndotoni wakiomba niwapatie vinywaji, sehemu nyingine niliota napeleka vyakula,wakaniomba na vinywaji, specifically soda, aliniomba Bibi mzaa mama.

Yani nilikuwa naona ndoto za kuwahusu wao na ndugu wengine walio hai katika familia. Ni wiki niliyokuwa najihisi huzuni na upweke sana bila sababu.

Basi Jumatatu nilipotoka job nikaenda kwenye msikiti wa jiran Kuna duka la dawa za kisuna nikanunua udi flan hivi huwa unatumika kuombea watu waliotangulia mbele za haki. Nikarudi nyumbani nikaoga, nikala then nikauchoma nikiwaombea pumziko hasa Bibi na mama, then kwenye saa kumi na moja nikalala,nimejiwekea utaratibu wa kulala mchana nikiwa free.

Ndani ya nusu saa toka nilale nikaota mwanamke mmoja mtu mzima kavaa upande wa kanga kajifunika Hadi kifuani, kasimama dirishani mwa chumba changu lakini kanipiga mgongo, hivyo sikumwona sura,then nikastuka toka usingizini, nikabadil upande nikarud kulala, this time kama nusu saa baadae nikaota nakabwa pumzi na mtu nisiyemwona huku amenikandamiza kichwa chini,nikawa napambana kujinasua huku nikitaja damu ya Yesu niokoe, nilihangaika kwa muda then akaniachia na nikaamka ghafla. Sikulala tena, nikaamka na kuendelea na ratiba nyingine ya kumalizia siku.

Kulipopambazuka, nikajiandaa, nikachoma udi then nikaingia mzigon, then saa 11 baada ya muda wa mkoloni, nikaenda sokon nikanunua chumvi ya mawe nikarudi home nikaipigia deki chumbani na sebuleni. Nikachoma na udi ule wa kuwaombea wazee wangu, nikaendelea na ratiba nyingine na hali ikaendelea kuwa shwari hata zile ndoto zikakata.

Kimbembe nimeamka leo nikajiandaa niende job, kabla sijatoka natafuta udi zangu zilizobaki nichome sizioni, nimekagua kote sijaziona, na ninaishi peke yangu, hii nyumba Ina usalama wa kutosha, nimebaki na bumbuwazi. Hapa nimepanga nikitoka job nikanunue za kutosha pamoja na ubani, manake hii nyumba nina wiki tu toka nihamie. Maoni yenu wadau.
Narudia tena kabla hujalala nyunyuzia lango lango la ndoto na damu ya Yesu wa nazareth usiache fanya kwa imani

Mim mauza uza kama hayo natumiaga damu ya Yesu yanaondoka na hayanisumbuagi na huwa nayashinda sana
kuna siri kubwa sana kwenye damu ya Yesu huku makanisa yakishupalia mafuta na chumvi za upako nawakati kuna damu ya Yesu
 
Narudia tena kabla hujalala nyunyuzia lango lango la ndoto na damu ya Yesu wa nazareth usiache fanya kwa imani

Mim mauza uza kama hayo natumiaga damu ya Yesu yanaondoka na hayanisumbuagi na huwa nayashinda sana kuna siri kubwa sana kwenye damu ya Yesu
Asante mkuu nitatekeleza 🙏
 
Aombe ulinzi kwa kiumbe alie shindwa kujilinda na kuokoa maisha yake binafsi?.
Yesu ni Mungu ndani ya mwanadamu, alikuja kuwakomboa watu na kuonesha namna tunavyopasa kupendana hata ikibidi kufa kwa ajili ya wenzetu. Yesu ni Jina Lipitalo Majina yote, hakuna mapepo yanayoweza kusimama Jina hili likitajwa!
 
Hizi imani ni mitihani sana,mimi ni Muisilamu nimefundishwa kuwaheshimu watu wote hata kama si Waisilamu,nimefundishwa kuwajali na kuwaheshimu wazazi wangu hata kama si waisilamu

Nimefundishwa kuwaombea dua waliotangulia, bali siyo kuwatukana hata kama wa Dini nyingine
 
Back
Top Bottom