Mavazi ya Mchungaji Tony Kapola yachunguzwe

Nimeshawahi sikiliza sermons zake jamaa anamadini sema yupo rational sana stori nyingi. Mavazi sio inshu mbona jamaa yupo smart tu, kupiga sneaker na jinsi sio kigezo cha ku criticise mafundisho yake
 
Na nani TAKUKURU?
 
hao ni motivational speakers, sio wahubiri, ndio maana wasikilizaji wengi ni wanawake, wanacheka hadi jino la mwisho na wao wanajiona wanaongea vitu vya pointiiii. wala usiwaite wachungaji.
Sasa tuwaache hao wanawake waendelee kuliwa au tuwashtue?
 
Kuna mmoja jana jumapili siku ya pentekoste nilimshangaa sana akihubiri injili ambayo hakuipokea tangu akiwa kijana, najua ujana wake alikuwa moto ila sasa anahubiri injili nyepesi ya kuridhia urembo uliopigwa marufuku enzi hizo. Alimuinua mama mama mmoja alisuka rasta na kujipaka lipstick na wanja akimsifia kuwa anafanya vema kuonekana ana hela za kununua mapambo hayo, hivyo wanawake wote kanisani wawe na hela za kufanya maendeleo ikiwemo kujipamba kwa mapambo ya gharama si dhambi. Tuje kwa hawa vijana wa kileo watumishi wa mungu akina kapole na masanja wanavaa hovyo sana. Ni wachungaji lakini uvaaji wao ni utata mtupu, watasababisha hata mabinti wa makanisa ya nao watavaa hovyo kama wachungaji wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…