Mawakala wa huduma za fedha kwa mitandao ya simu acheni dharau

Mawakala wa huduma za fedha kwa mitandao ya simu acheni dharau

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Nimefika kwa wakala kwa lengo la kutoa pesa kutoka mtandao wa simu, anasema hana salio la kutosha. Wakati huo naona watu wengine wanatoa na wanaondoka.

Aliniuliza unatoa kiasi gani nikamwambia 3000/= ghafla akakunja sura na kusema hana salio.

Sasa kosa langu ni lipi hapo? Au hicho kiasi ni kidogo kiasi kwamba haoni faida atakayopata? Na sio mara ya kwanza kuona hilo, ni kawaida yao kukataa kufanya miamala ya viwango hivyo.

Ikiwezekana waandike viwango vyao wanavyo vitaka wateja waanzie kutoa na sio kupata gadhabu pale mtu anapotaka kutoa kiasi kidogo.


#BM
 
Nimefika kwa wakala kwa lengo la kutoa pesa kutoka mtandao wa simu, anasema hana salio la kutosha. Wakati huo naona watu wengine wanatoa na wanaondoka...
Inawezekana hakua na note ndogo ndogo thus akakubwaga kimtindo.
 
Back
Top Bottom