Mawakala wa huduma za fedha kwa mitandao ya simu acheni dharau

Mawakala wa huduma za fedha kwa mitandao ya simu acheni dharau

Nimefika kwa wakala kwa lengo la kutoa pesa kutoka mtandao wa simu, anasema hana salio la kutosha. Wakati huo naona watu wengine wanatoa na wanaondoka.

Aliniuliza unatoa kiasi gani nikamwambia 3000/= ghafla akakunja sura na kusema hana salio.

Sasa kosa langu ni lipi hapo? Au hicho kiasi ni kidogo kiasi kwamba haoni faida atakayopata? Na sio mara ya kwanza kuona hilo, ni kawaida yao kukataa kufanya miamala ya viwango hivyo.

Ikiwezekana waandike viwango vyao wanavyo vitaka wateja waanzie kutoa na sio kupata gadhabu pale mtu anapotaka kutoa kiasi kidogo.
Ameona ungemsumbua chenchi mkuu
 
Na ujue huyo sio mwenye biashara, ni muajiriwa tu. Mwenye biashara anajua kuwa anaingiza commission hata kama kiwango ni kidogo. Hawezi kukataa hela. Wafanyakazi ndio wana dharau sana
Ni kweli mkuu me kuna huyo mmoja nilifika nikamwambia nataka kuweka hela akauliza sh ngap nkamwambia 15k akaanza kubofya ile batani ake ili aweke,sasa akaniuliza jina ambalo sio Lang nikasema, umesemajeee??

Akabinua gudomo gwake kwa dharau akakata then akaanza kuweka upya ulipofika muda wa kutaja namba nikataja bila kinyongo sasa alipokuwa anaweka akaja jamaa mwngne akasema anataka aweke hela 25k cha ajabu akafuta yang ili amwekee huyo mwamba nilipata hasira, daadek
Nkasepa na hela yangu bila kusema chochote 🏃 🏃
 
Back
Top Bottom