Mawakili 386 wajitokeza kumtetea Mbowe Mahakamani 05/08/2021

Mawakili 386 wajitokeza kumtetea Mbowe Mahakamani 05/08/2021

Sio kosa wala sio jambo la kisiasa kuwakilishwa na mawakili 386, kwasababu sheria za nchi zinatoa haki kwa washtakiwa wote kutetewa na mawakili mbele ya mahakama (Natural Justice - Right To Be Represented), na haki hio haina mipaka juu ya idadi ya mawakili wanao mwakilisha mshtakiwa.

Ila cha ajabu CCM wataligeuza jambo hilo la Gaidi Freeman Mbowe kuwa la kisiasa zaidi, kama alivyotangulia IGP Sirro kuligeuza la kisiasa jana kwenye press na waandishi wa habari. Akaenda mbele zaidi na kumtia hatiani hata kabla mtuhumiwa Gaidi Freeman Mbowe hajafikishwa mbele ya mahakama.

Cha ajabu IGP Sirro hakuwahi kuongelea kwenye vyombo vya habari swala la viongozi wa umma kutumia vijana wake wa police kufanya uhalifu. Mfano, Paul Makonda na Ole Sabaaya walivokua wakitumia vijana wa IGP Sirro kufanya uhalifu wa kutumia silaha na risasi (Kama alivosema jana tunanunua kwa hela zetu) kuteka na kufanya ujambazi kwa kutumia silaha hizo katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Kilimanjaro.

IGP Sirro mungu anakuona, usichokifahamu kesi ya Gaidi Freeman Mbowe umeishaivuruga kwa kuiongelea mbele ya vyombo vya habari, wewe utaitwa kama shahidi na kama nawaona kina Kibatala jinsi watakavyo kupiga maswali siku hio. Mmesha isiriba kinyesi Tanzania kwenye swala la Gaidi Freeman Mbowe kwenye uso wa dunia.

HAPA NI KUFANYA MAOMBI KESI HII IRUSHWE LIVE COVERAGE, ili wananchi waone kitakachojiri mahakamani.

Nawewe utakuwa unamatatizo....unamlaumu sirro wakati huohuo kila ukitaja jina LA MBOWE unatanguliza GAIDI...huo ugaidi umeshauthibitisha?DHAMBI MOJA TU YA UNAFIKI NDIO INAKUSUMBUA,UNGEENDA MBINGUNI
 
Ni nani atakae waruhusu mawakili zaidi ya 300 kuingia mahakamani? Pia kama kweli anahusika na mashitaka waliyomfungulia basi hata wakiruhusiwa mawakili 1000 kumtetea haitosaidia. Waswahili wanasema "Siku ya kifo cha nyani miti yote huteleza"
Twasubiri kwa HAMU kuiona hiyo miti ikiteleza. Ili tumuone kwelikweli ATAKAETELEZA.
 
Back
Top Bottom