Mawakili wa Lissu wawashukia Waziri Bashungwa, AG Johari

Mawakili wa Lissu wawashukia Waziri Bashungwa, AG Johari

Cha msingi nilicho okota ni kuminywa kwa haki za mfungwa. Sasa kama wanasheria wanalalama badała ya kukosoa kazi ipo.

Nilitegemea pamoja na hiyo sheria waliyoitaja nina uhakika kuna sheria zingine luluki Tanzania za ‘fair trials’.

Criminal case haiwezi kuwa private hearing (that’s only possible in civil disputes) vinginevyo criminal proceedings ni public hearing. Kuna clear breach of fair trial and human right (I think it’s articles 6, not certain though). Hiyo ni international convention ambayo ni sehemu ya katiba. Kunq mambo luluki ya haki za Lissu ambazo ni breached.

Bado kuna sheria za Tanzania mfano 👇


View attachment 3323727

Sasa kama mwanasheria wako analalama kuongea na mteja huku kasimamiwa na afande bila ya kusema sheria gani hairuhusu, hayo si majanga.

Kwa kifupi Kibatala na wenzake ni mediocre lawyers tu, my god the team has 35 of them na hawajui hata sheria za fair trials Tanzania wala prisoners rights. Wamekadhana kutumia sheria moja tu ya mienendo ya kesi za jinai.

Tunaposhindwa kesi huko ulaya sio kwamba tunakuwa tumekosea kisheria kuvunja mikabata, it’s just overall we have bad lawyers.
Basi kajiunge nao uwasaidie,walikochemka!!
 
Yaani maisha haya ni kama tumechanganyikiwa. Kuna wakati kama nilisikia baadhi ya watu wana sema serikali munchies Lissu, swali je waziri Bashungwa angesema tuna muachia Lissu hawa mawakili wangelalamika kuwa mahakama imeingiliwa?
Ahahahahaha! Umeuliza swali zuri kweli!
 
Mawakili, Peter Kibatala na Jebra Kambole wanaomwakilisha Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu katika kesi za uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni wamelalamikia kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa wakisema zinaingilia kesi hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Mawakili hao wamesema watafungua kesi kwa kutumia kauli hizo kuonyesha kuwa mahakama imeingiliwa.

Akizungumza na maofisa wa Jeshi la Magarereza mkoani Dodoma Aprili 30, Waziri Bashungwa alisema uamuzi wa baadhi ya kesi kufanyika kwa njia ya mtandao, alitolea mfano wa kiongozi wa Chadema akisema alitoa tamko linaloashiria uvunjifu wa amani na usalama.

Mbali na kaulio ya Waziri Basghungwa, mawakili hao pia wametaja kauli iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari akiwa bungeni Aprili 30 akiwa bungeni jijini Dodoma akisema utaratibu wa kusikiliza kesi ya Lissu kimtandao ulifanywa kwa mujibu wa shera na kwa kufanya tathmini.

Lissu alikamatwa Aprili 9 akiwa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na kisha kusafirishwa usiku hadi Dar es Salaam, ambako alifikishwa katika mahakama hiyo Arili 10 na kusomewa mashitaka manne likiwamo kosa la uhaini na matatu ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.

Soma pia: Lissu alipofikishwa Mahakamani

Soma pia: Kesi za Lissu hizi hapa

Kauli za Bashungwa, AG Johari

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 3 jijini Dar es Salaam, Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alisema kauli hiyo ya Waziri Bashungwa imemweka hakimu anayesikiliza kesi hiyo katika wakati mgumu, kwani ni miongoni mwa hoja walizolalamikia na zitatolewa uamuzi Mei 6.

“Waziri amekwenda kwa Kiingereza tunasema, ‘he let the cat out of the bag’. Hivi mnamweka kwenye nafasi gani hakimu Muhini anayekwenda kutoa uamuzi kwenye suala hilo hilo Mei 6? Mnakwenda kumpa majibu ya mtihani aseme kwamba Waziri ameshasema kwamba kwa sababu za kiusalama kwamba Chadema walitaka kufanya maandamano na vurugu?” amehoji Kibataka

Ameendelea, “Je angekuwa ndugu yake au mwanafamilia wake anachakatwa kisheria angetoa matamko kama yale?

“Kisheria ni kwamba amemuweka hakimu Muhini katika a very difficult position (wakati mgumu), kwamba sisi mawakili wa Lissu tutajisikiaje kwamba Mahakama ilifanya sahihi kabisa? Kwanini tusijisikie kwamba kuna mawasiliano yasiyo rasmi kati ya Mahakama na Jeshi la Polisi?”

“Yeye (Waziri Bashungwa) na wenzake wote wasitoe kauli zozote zinazoweza kutafsiriwa kwamba nzinakwenda kuingilia utendaji huru wa Mahakama,” amesema.

Kuhusu kumwona Lissu katika Gereza la Ukonga, Kibatala amesema mteja wao Lissu amekataa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa amenyimwa haki ya kuwasiliana na mawakili wake.

“Hatuna ugomvi na askari Magereza, lakini huwezi kukataa kwamba bosi wao ndio huyo Bashungwa, ndiye anayesimamia polisi waliokamata Lissu Mbinga wakamsiafirisha usiku kwa usiku bila kumpa nafasi ya kuonana na wakili wake,” amesema.

Amerejea Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa la Januari 8, 2016 linaloitwa The Nelson Mandela Rules, akisema limetoa haki za watuhumiwa na wafungwa kuonana na mawakili wao.

“Wafungwa wote waliohukumuwa na ambao bado hawajafungwa watapewa nafasi ya kufanya mawasiliano na mawakili wao wa kisheria, bila kuchelewa na bila kuingiliwa.

“Unapofanya mimi niongee na mteja wangu kwa simu najua nani anarekodi na anapewleka wapi Wakati kanuni inasema iwe kwa siri?”

Huku akibubujikwa na machozi, Kibatala amesema alitumia muda wa Zaidi ya saa 3 kusubiri kuonana na Lissu gerezani na hata walipoonana walitenganishwa kwa kioo na waliongea kwa simu huku wakilindwa.

“Ikabidi tuwe wabunifu tuzungumze kwa Kiingereza. Kama mna mshitaki Lissu na mna ushahidi mnaogopa nini?” amehoji.

Kuhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kibatala amemkosoa, akisema alikosea aliposema kwamba watu wanapotosha.

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johari aliingia mahakamani hata siku moja? Hata hizo hoja, maana nimesikia anasema kuna watu wanapotosha, yeye amejuaje kama kuna watu wanapotosha? Alikuja mahakamani akasikia hoja kweli?”

Hoja nyingine walizotoa na zitakazotolewa uamuzi Mei sita ni kuhusu Lissu kunyimwa kuabudu katika siku za Ijumaa Kuu, Jumapili na Jumatatiu ya Pasaka zimemkuta Lissu akiwa mahabusu.

“Jumapili ya pasaka ametumwa Baba paroko wa Parokia ya Ukonga, amekwenda Gereza la Ukonga, hii ni siku muhimu kwa Lissu sio tu kwa sababu ya Wakristo, bali niyeye kibinafsi alitaka, lekini amenyimwa.

“Paroko ameacha kazi zake amekwenda kuendesha ibada, akaambiwa, anybody else be free, ila huyu, masharti maalum.”

Alisema hata Jumatau ya Pasaka aliomba kwenda kusali akanyimwa.

“Hayo ndio malalamiko yaliyomfanya Lissu akatae kushiriki kesi ya mtandao.

“Hoja hizo tumezitoa na zinakuja kutolewa uamuzi tarehe 6, lakini watu barabarani wanaongea mambo waliyoongea, kama sio kuipa pressure mahakama ni nini? Kama sio kutufanyia ujeuri sisi kwamba ninyi hoja zenu si chochote na hazitafanyiwa kazi, ni nini? Tutafsiri nini?” amehoji Kibatala.

Ameongeza kuwa, katika hoja zao walioma aitwe Ofisa Magereza wa Mkoa na Mkuu wa Gereza la Ukonga ili wajibu hoja hizo na watajibiwa Mei 6.

“Tumeomba lile na litajibiwa tarehe 6, lakini tayari watu barabarani wameanza kuongea,” amnesia.

Kuhusu kuzuia watu kuja kusikiliza kesi hiyo, Kibatala ametaja kesi za watu wengine akiwamo Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Zakaria Hanspope na makada wa Chadema, Boniface Jacom na Godlisten Malisa, akisema watu hawakuzuiwa kuingia bali walifurika na shughuli za mahakama ziliendelea kama kawaida.

Ametaja kifungu cha 186 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai akisema kesi zote za jinazi zinapaswa kusikilizwa kwenye mahakama ya wazi isipokuwa kwa sababu maalum na ni lazima hizo sababu zijulishwe kwa pande zote.

Pia ametaja kifungu cha 192 cha CPA akisema usikilizwaji wa awali haupaswi kufanywa kwa remote kwa sababu kuna mambo ambayo yanayohitaji mshitakiwa awepo mahakamani.

“Hoja nyingine tuliyozungumzia ni haki ya watu kushiriki kesi, hata mawakili, Lissu ana mawakili 28 hadi 33. Kitendo cha nyie kumshitaki mtu halafu mawakili 33 wanaacha shughuli zao wanakuja mahakamani. Kama ningekuwa mimi ningezema something is not right somewhere, maana yake hawa mawakili wana akili wamesoma hati ya mashitaka wamesema hapana, hata mimi lazima nione,” amesema.

Amesema hata mawakili walisumbuliwa kuingia mahakamani.

Amezungumzia pia kukamatwa kwa viongozi wa Chadema akiwamo Makamu Mwenyekiti, John Heche akisema ni kuwanyika haki zao.

“Wamekwenda kuzuia ya mteja wetu Lissu. Yaani mawakili tunakwenda kwenye vita ya kupigania haki ya mteja wetu, unaamka asubuhi unasikia nyumba ya mteja imezingirwa, kwa nini tusitafsiri kwamba ni kututoa kwenye mstari? Halafu mtu anasema ni ulinzi wa kawaida. Give me a break.”

Bila kutaja jina, Kibatala pia amezungumzia kauli ya kiongozi mmoja aliyesema kuwa kauli ya Lissu kwamba watakinukisha ndio imemponza, suala hilo lipo kwenye hati ya mashitaka.

“Hayo ndio maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kwenye kesi Namba 8607, halafu anaibuka mtu barabarani, anakwenda kuzungumza maneno yanayo kama yanajibu hoja kwenye hati ya mashitaka, kama sio kuingilia mahakama ni nini? Kama sio kukosa busara za kisheria ni nini?”

“Hatutaishia hapo, tutaschukua hatua za kisheria, kama nilivyosema Jumatatu nitakwenda Ukonga, kisha nitaitaka mahakama kuona kwamba kuna mistrial (ukiukwaji wa mashauri).

Wapanga kuwashitaki viongozi waliotoa kauli

Amesema viongozi wote waliotoa kauli kuhusu kesi ya Lissu watashitakiwa.

“Tunawashukuru Waziri Bashungwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengine kwa kutupa silaha kwa kukosa kiasi. Ni kama tayari wanaona Tundu Antiphas Lissu ameshahukumiwa. Ndio maana wanasema ukikinukisha utanuka wewe, maana tafsiri yetu ni kwamba ukitamka hayo maneno you will be convicted, na adhabu ya uahini ni kifo,” amesema.

Hija za Mawakili wa Lissu hizi paka

Lissu kuanza mgomo wa chakula

Kibatala pia ametoa taarifa kuwa Lissu ataanza mgomo wa chakula kushinikiza haki itendeke katika kesi hiyo.

“Kwa hiyo atasusia kula mpaka haki itendeke.”

Kwa upande wake Wakili Jebra Kambole amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaweka mihimli mitatu ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali na haipaswi kuingiliana.

“Mahakama ndio chombo cha juu cha utoaji wa haki Katiba ibara ya 107B tunapona mahakama inangiliwa lazima tutoke.

“Kanuni ya Adhabu 114(d) Sura namba 16 inakataza kuzungumzia jambo lililoko mahakamani,” amesema.

Kuhusu kusikiliza kesi mtandao, amesema mtindo huop sio mbadala ya mahakama ya wazi.

“Mbadala ya mahakama ya wazi ni chamber court (Mahakama ya ndani) ile ambayo unakuwa na hakimu chumbani.

“Unapomshitaki wa caliber ya Lissu ni lazima watu waje, sio kama unamshitaki Mwajuma wa Mbagala, kwa hiyo ni lazima ubebe na matokeo yake.

“Huyu alikuwa Mbunge mstaafu, mgombea urais, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani, lazima watu waje, usiendeshe kesi chumbani haiwezekani,” amesema.

Kuhusu kumwona Lissu gerezani Kambole alisema ni kama unakwenda gereza la Guantanamo (Cuba).

“Kaka yake Lissu ni wakili, anatoka Arusha, amesomba ndugu zake, wengine kutoka Singida na wengine kutoka Songea, wanazuiwa kuingia.

“Hutaki mawakili wamwone, huitaki asali, hutaki wamwingie chakula, unataka nini?

Umemkamata, hutaki kupelekeza, hutaki mashahidi, unataka nini sasa?”
Huyo ni mwanasheria mkuu au mwanasheria wa Yanga? Maana kama ni Mkuu mwenyewe hapaswi kutoa kauli hiyo!
 
Cha msingi nilicho okota ni kuminywa kwa haki za mfungwa. Sasa kama wanasheria wanalalama badała ya kukosoa kazi ipo.

Nilitegemea pamoja na hiyo sheria waliyoitaja nina uhakika kuna sheria zingine luluki Tanzania za ‘fair trials’.

Criminal case haiwezi kuwa private hearing (that’s only possible in civil disputes) vinginevyo criminal proceedings ni public hearing. Kuna clear breach of fair trial and human right (I think it’s articles 6, not certain though). Hiyo ni international convention ambayo ni sehemu ya katiba. Kunq mambo luluki ya haki za Lissu ambazo ni breached.

Bado kuna sheria za Tanzania mfano 👇


View attachment 3323727

Sasa kama mwanasheria wako analalama kuongea na mteja huku kasimamiwa na afande bila ya kusema sheria gani hairuhusu, hayo si majanga.

Kwa kifupi Kibatala na wenzake ni mediocre lawyers tu, my god the team has 35 of them na hawajui hata sheria za fair trials Tanzania wala prisoners rights. Wamekadhana kutumia sheria moja tu ya mienendo ya kesi za jinai.

Tunaposhindwa kesi huko ulaya sio kwamba tunakuwa tumekosea kisheria kuvunja mikabata, it’s just overall we have bad lawyers.
Sindio huyo huyo anayeliingizia hasara taifa, kila siku kesi tunaangukia pua
 
Sindio huyo huyo anayeliingizia hasara taifa, kila siku kesi tunaangukia pua
Hii sio serious government kama yule jamaa aliekuwa anapiga kuuza bandari ndio mwanasheria mkuu leo.

I can’t imagine demoralisation ya wanasheria wenzako huko ofisini ambao wamefika walipo kwa succession planning; halafu anaokotwa tu mtu kuwa mkubwa wao

Sikujua hata kama jamaa ni mwanasheria kipindi cha makelele ya DPW si alikuwaga sijui kwenye usimamizi wa viwanja or someplace where his role did not include everyday legal thinking.

We are not serious people, civil services ya Tanzania ni weak mno, you don’t ascend to senior post kirahisi hivyo nchi zingine.

Huyu Hamza Johari amewahi hata ku-practicing lawyer katika maisha kweli, it’s just ridiculous.
 
Back
Top Bottom