Kipindi cha Magufuri na kipindi hiki cha huyu Rais ni kipindi ambacho nchi imeongozwa bila utaratibu ndiyo maana haya yote tumeshuhudia yakitokea mfano:-Kupigwa Risasi Tundu Lissu akiwa mbunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye eneo lenye ulinzi wa kila namna,Kuondolewa kwa CAG Professor Assad bila utaratibu kisa kagundua ubadhirifu mahali fulani hasa palipokuwa panamhusu mheshimiwa Rais,Kujiuzulu kwa Wabunge kwenye Chama fulani na kugombea Ubunge huo huo na watu wale wale jimbo lile lile kupitia chama tawala na kushinda kwa nguvu,Kukataza mikutano ya vyama vya siasa,kujizulu Uspika kwa bwana Job Ndugai,kuwepo wabunge 19 Bungeni ambao chama chao hakiwatambui.