Mawakili wanena kuhusu Mfanyakazi wa TRC aliyefukuzwa kazi kwa kupinga tozo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wanasheria mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu kufukuzwa kazi kwa Meneja wa Shirika la Reli nchini (TRC) Kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye huku baadhi yao wakionyesha nia ya kumpatia msaada wa kisheria.

Juzi, Afumwisye alipokea barua iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ikimjulisha uamuzi wa shirika hilo wa kumfukuza kazi kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuthibitishwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka jana.

Baadhi ya makosa anayotuhumiwa kuyafanya ni kupinga juhudi za Serikali za kuanzisha tozo kwenye miamala ya simu na pia kupinga chanjo inayotolewa kwa wananchi kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.

Kadogosa alibainisha makosa mengine kwenye barua hiyo kuwa ni kukashifu viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia makundi ya kijamii.

Wakizungumza kuhusu kufukuzwa kwa mfanyakazi huyo, mawakili mbalimbali wamesema wako tayari kumsaidia Afumwisye kwa sababu hajatendewa haki katika kufukuzwa kwake na wengine wamebainisha kwamba alikiuka kanuni za utumishi wa umma.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema yuko tayari kumtetea kijana huyo kupitia taasisi yake kwa sababu ana uhuru wa kutoa maoni yake.

“Sio fair (haki) kabisa, tena mwambie kabisa, mimi binafsi ninajitolea kumsaidia kumtetea kupitia sehemu yangu, kwenye vyombo vya kisheria. Yeye ni kama Watanzania wengine kama sisi na wengine wengi ambao wanahoji hizo tozo,” alisema Olengurumwa.

Wakili kiongozi kutoka kampuni ya Haki Kwanza, Alloyce Komba, alisema atakuwa tayari kumsaidia endapo atajua kesi yake ilitokana na nini, lakini kama ilitokana na tamko la Mkurugenzi Mkuu wa TRC, basi ataweza kusaidia.

“Sisi wanasheria tunasema hapana, ni unfair termination (amefukuzwa isivyo halali) ambayo haujafanyiwa judicial process (taratibu za kimahakama) kwa sababu tunasema hata mtu aliyeua dhahiri, lazima ufuate taratibu,” alisema Komba.

Aliongeza kwamba kuna taratibu za kumfukuza mtumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kumsikiliza, kumwonya na kisha kuchukua hatua kama aliyopewa ya kufukuzwa kabisa katika ajira yake.

Komba alisisitiza kwamba kwa nafasi yake kama mtumishi wa umma, jambo lake limepewa uzito na kwamba katika utumishi wa umma, kosa la kutotii mamlaka linatazamwa kwa jicho kali zaidi kuliko makosa mengine.

“Kwa hiyo, maoni yangu ni kwamba administratively (kiutawala), kuna hayo masuala ya insubordination (kutotii mamlaka), lakini legally (kisheria) ningependa kujua kama utaratibu wa kisheria ulifanyika,” alisema Komba.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole, alisema watu wana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kwamba hilo siyo sababu ya kumfukuza kazi ili mradi kazi zake anazifanya kikamilifu.

Alisema hata mtu aliyeko serikalini ana haki ya kutoa maoni na hadhani kama kufanya hivyo kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha utovu wa nidhamu kiasi cha mwajiri wake kumfukuza kazi.

“Mimi namshauri akate rufaa kwa sababu uamuzi huo unakiuka Katiba na sheria za nchi. Katiba haijasema watumishi wa umma hawana uhuru wa kutoa maoni, imesema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni,” alisema Kambole.

Alisisitiza kwamba Afumwisye ana haki ya kukata rufaa na kusikilizwa na kwa mazingira ya kufukuzwa kwake, anaweza kupatiwa msaada wa kisheria endapo mamlaka za awali zitaamua vinginevyo.

Mwasisi mwenza wa kampuni ya uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates, Onesmo Mpenzile alisema kosa kubwa ambalo linasimamiwa kwa ukali na Serikali ni kutotii mamlaka.

Alisema Ofisi ya Rais ndiyo inaongoza utumishi wa umma, hivyo mtumishi yeyote wa umma anatakiwa kuheshimu mamlaka za juu yake kwa sababu sheria, kanuni na utaratibu katika utumishi wa umma unaelekeza hivyo.

Juzi Afumwisye alisema kuwa anafanya utaratibu wa kukata rufaa ndani ya siku 45.
 
Alikosa tu Hekima! Sheri’s nyingi sana hazifuatwi, sasa kwa comment zisizompa faida kapoteza ajira, ujinga!

Jiulizeni tu:

- Hukumu imekaa Mda gani ya yeye kufukuzwa? Mda mrefu, ni kwamba wameshauriana sana na kuamua kumfukuza.

- Anakata rufaa kwa nani? He he he nani anasikiliza rufaa?
 
Hii kesi ya huyo jamaa kama kweli hawa wanasheria watajitolea kumsaidia na akaenda kushinda kesi italeta precedence nzuri sana.

Unawezekana huo ndio ukawa mwisho wa watendaji wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujipendekeza kwa watawala, na kwa watawala wenyewe kukaa kimya pale haki za mtu zinapokandamizwa makusudi ili kuwafurahisha wao.
 
Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
 
Mliambiwa hayo maneno mkapewa na vifungu vya sheria kusapoti kile mlichoambiwa, au mliambiwa tu kisha wote mkaitikia ndio mzee?

Inawezekana tatizo la ajira mlilokuwa nalo liliwafunga upeo wenu mkashindwa kuuliza maswali kwa kuhofia kupoteza kazi hata kabla hamjaianza.
 
Ishaisha hiyo, huyo malafyale kashaula wa chuya
 
Alikosa tu Hekima! Sheri’s nyingi sana hazifuatwi, sasa kwa comment zisizompa faida kapoteza ajira, ujinga!

Jiulizeni tu:

- Hukumu imekaa Mda gani ya yeye kufukuzwa? Mda mrefu, ni kwamba wameshauriana sana na kuamua kumfukuza.

- Anakata rufaa kwa nani? He he he nani anasikiliza rufaa?
Hapo Sasa !!
 
CCM wanajiona kama miungu watu vile. Wanafanya mambo ya hovyo, halafu wenye akili wakiwakosoa, wanawafanyia zengwe.

Yote aliyoyasema yana mashiko! Tozo zimezidi, na zinaumiza wananchi wa kipato cha chini! Na pia hiyo chanjo ya corona haina tija yoyote ile! Zaidi tu imetokana na shinikizo kutoka kwa mabeberu.

Sasa kwa nini wamfukuze kazi, na wakati amesema ukweli mtupu! Mbona hawa chawa wanaosifia kila kitu hawafukuzwi kazi? Au imefikia wakati wananchi wanatakiwa kisifia tu! Kamwe jambo hilo haliwezekani.
 
Alikosa tu Hekima! Sheri’s nyingi sana hazifuatwi, sasa kwa comment zisizompa faida kapoteza ajira, ujinga!

Jiulizeni tu:

- Hukumu imekaa Mda gani ya yeye kufukuzwa? Mda mrefu, ni kwamba wameshauriana sana na kuamua kumfukuza.

- Anakata rufaa kwa nani? He he he nani anasikiliza rufaa?
Baada ya hapo rufaa itaenda hadi mahakamani kama atashindwa kwenye rufaa za taasisi husika.
 
Wanasheria mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu kufukuzwa kazi kwa Meneja wa Shirika la Reli nchini (TRC) Kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye huku baadhi yao wakionyesha nia ya kumpatia msaada wa kisheria.

Juzi, Afumwisye alipokea barua iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ikimjulisha uamuzi wa shirika hilo wa kumfukuza kazi kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuthibitishwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka jana.

Baadhi ya makosa anayotuhumiwa kuyafanya ni kupinga juhudi za Serikali za kuanzisha tozo kwenye miamala ya simu na pia kupinga chanjo inayotolewa kwa wananchi kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.

Kadogosa alibainisha makosa mengine kwenye barua hiyo kuwa ni kukashifu viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia makundi ya kijamii.

Wakizungumza kuhusu kufukuzwa kwa mfanyakazi huyo, mawakili mbalimbali wamesema wako tayari kumsaidia Afumwisye kwa sababu hajatendewa haki katika kufukuzwa kwake na wengine wamebainisha kwamba alikiuka kanuni za utumishi wa umma.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema yuko tayari kumtetea kijana huyo kupitia taasisi yake kwa sababu ana uhuru wa kutoa maoni yake.

“Sio fair (haki) kabisa, tena mwambie kabisa, mimi binafsi ninajitolea kumsaidia kumtetea kupitia sehemu yangu, kwenye vyombo vya kisheria. Yeye ni kama Watanzania wengine kama sisi na wengine wengi ambao wanahoji hizo tozo,” alisema Olengurumwa.

Wakili kiongozi kutoka kampuni ya Haki Kwanza, Alloyce Komba, alisema atakuwa tayari kumsaidia endapo atajua kesi yake ilitokana na nini, lakini kama ilitokana na tamko la Mkurugenzi Mkuu wa TRC, basi ataweza kusaidia.

“Sisi wanasheria tunasema hapana, ni unfair termination (amefukuzwa isivyo halali) ambayo haujafanyiwa judicial process (taratibu za kimahakama) kwa sababu tunasema hata mtu aliyeua dhahiri, lazima ufuate taratibu,” alisema Komba.

Aliongeza kwamba kuna taratibu za kumfukuza mtumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kumsikiliza, kumwonya na kisha kuchukua hatua kama aliyopewa ya kufukuzwa kabisa katika ajira yake.

Komba alisisitiza kwamba kwa nafasi yake kama mtumishi wa umma, jambo lake limepewa uzito na kwamba katika utumishi wa umma, kosa la kutotii mamlaka linatazamwa kwa jicho kali zaidi kuliko makosa mengine.

“Kwa hiyo, maoni yangu ni kwamba administratively (kiutawala), kuna hayo masuala ya insubordination (kutotii mamlaka), lakini legally (kisheria) ningependa kujua kama utaratibu wa kisheria ulifanyika,” alisema Komba.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole, alisema watu wana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kwamba hilo siyo sababu ya kumfukuza kazi ili mradi kazi zake anazifanya kikamilifu.

Alisema hata mtu aliyeko serikalini ana haki ya kutoa maoni na hadhani kama kufanya hivyo kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha utovu wa nidhamu kiasi cha mwajiri wake kumfukuza kazi.

“Mimi namshauri akate rufaa kwa sababu uamuzi huo unakiuka Katiba na sheria za nchi. Katiba haijasema watumishi wa umma hawana uhuru wa kutoa maoni, imesema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni,” alisema Kambole.

Alisisitiza kwamba Afumwisye ana haki ya kukata rufaa na kusikilizwa na kwa mazingira ya kufukuzwa kwake, anaweza kupatiwa msaada wa kisheria endapo mamlaka za awali zitaamua vinginevyo.

Mwasisi mwenza wa kampuni ya uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates, Onesmo Mpenzile alisema kosa kubwa ambalo linasimamiwa kwa ukali na Serikali ni kutotii mamlaka.

Alisema Ofisi ya Rais ndiyo inaongoza utumishi wa umma, hivyo mtumishi yeyote wa umma anatakiwa kuheshimu mamlaka za juu yake kwa sababu sheria, kanuni na utaratibu katika utumishi wa umma unaelekeza hivyo.

Juzi Afumwisye alisema kuwa anafanya utaratibu wa kukata rufaa ndani ya siku 45.
Wakishamtetea anarudi ofisi gani labda apewe haki zake akafungue biashara au kilimo huku Ngwendeza
 
Hili limeneja likuu la TRA Ni kulitia adabu kwa vyovyote
 
Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
Ni wapi raisi ametukanwa sasa?! Nchi hii ina shida kubwa sana ya kufikiria!!!
 
Alikosa tu Hekima! Sheri’s nyingi sana hazifuatwi, sasa kwa comment zisizompa faida kapoteza ajira, ujinga!

Jiulizeni tu:

- Hukumu imekaa Mda gani ya yeye kufukuzwa? Mda mrefu, ni kwamba wameshauriana sana na kuamua kumfukuza.

- Anakata rufaa kwa nani? He he he nani anasikiliza rufaa?
Acha kujaza watu uwoga wa kipumbavu,Mimi namsifu,ifike wakati Watanzania tuache woga wa kipuuzi,tudai haki zetu.Kuna uozo mwingi unaendelea si busara kuendelea kuufumbia macho.Hata Mungu hapendi.
 
Wanasheria mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu kufukuzwa kazi kwa Meneja wa Shirika la Reli nchini (TRC) Kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye huku baadhi yao wakionyesha nia ya kumpatia msaada wa kisheria.

Juzi, Afumwisye alipokea barua iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ikimjulisha uamuzi wa shirika hilo wa kumfukuza kazi kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuthibitishwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka jana.

Baadhi ya makosa anayotuhumiwa kuyafanya ni kupinga juhudi za Serikali za kuanzisha tozo kwenye miamala ya simu na pia kupinga chanjo inayotolewa kwa wananchi kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.

Kadogosa alibainisha makosa mengine kwenye barua hiyo kuwa ni kukashifu viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia makundi ya kijamii.

Wakizungumza kuhusu kufukuzwa kwa mfanyakazi huyo, mawakili mbalimbali wamesema wako tayari kumsaidia Afumwisye kwa sababu hajatendewa haki katika kufukuzwa kwake na wengine wamebainisha kwamba alikiuka kanuni za utumishi wa umma.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema yuko tayari kumtetea kijana huyo kupitia taasisi yake kwa sababu ana uhuru wa kutoa maoni yake.

“Sio fair (haki) kabisa, tena mwambie kabisa, mimi binafsi ninajitolea kumsaidia kumtetea kupitia sehemu yangu, kwenye vyombo vya kisheria. Yeye ni kama Watanzania wengine kama sisi na wengine wengi ambao wanahoji hizo tozo,” alisema Olengurumwa.

Wakili kiongozi kutoka kampuni ya Haki Kwanza, Alloyce Komba, alisema atakuwa tayari kumsaidia endapo atajua kesi yake ilitokana na nini, lakini kama ilitokana na tamko la Mkurugenzi Mkuu wa TRC, basi ataweza kusaidia.

“Sisi wanasheria tunasema hapana, ni unfair termination (amefukuzwa isivyo halali) ambayo haujafanyiwa judicial process (taratibu za kimahakama) kwa sababu tunasema hata mtu aliyeua dhahiri, lazima ufuate taratibu,” alisema Komba.

Aliongeza kwamba kuna taratibu za kumfukuza mtumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kumsikiliza, kumwonya na kisha kuchukua hatua kama aliyopewa ya kufukuzwa kabisa katika ajira yake.

Komba alisisitiza kwamba kwa nafasi yake kama mtumishi wa umma, jambo lake limepewa uzito na kwamba katika utumishi wa umma, kosa la kutotii mamlaka linatazamwa kwa jicho kali zaidi kuliko makosa mengine.

“Kwa hiyo, maoni yangu ni kwamba administratively (kiutawala), kuna hayo masuala ya insubordination (kutotii mamlaka), lakini legally (kisheria) ningependa kujua kama utaratibu wa kisheria ulifanyika,” alisema Komba.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole, alisema watu wana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kwamba hilo siyo sababu ya kumfukuza kazi ili mradi kazi zake anazifanya kikamilifu.

Alisema hata mtu aliyeko serikalini ana haki ya kutoa maoni na hadhani kama kufanya hivyo kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha utovu wa nidhamu kiasi cha mwajiri wake kumfukuza kazi.

“Mimi namshauri akate rufaa kwa sababu uamuzi huo unakiuka Katiba na sheria za nchi. Katiba haijasema watumishi wa umma hawana uhuru wa kutoa maoni, imesema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni,” alisema Kambole.

Alisisitiza kwamba Afumwisye ana haki ya kukata rufaa na kusikilizwa na kwa mazingira ya kufukuzwa kwake, anaweza kupatiwa msaada wa kisheria endapo mamlaka za awali zitaamua vinginevyo.

Mwasisi mwenza wa kampuni ya uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates, Onesmo Mpenzile alisema kosa kubwa ambalo linasimamiwa kwa ukali na Serikali ni kutotii mamlaka.

Alisema Ofisi ya Rais ndiyo inaongoza utumishi wa umma, hivyo mtumishi yeyote wa umma anatakiwa kuheshimu mamlaka za juu yake kwa sababu sheria, kanuni na utaratibu katika utumishi wa umma unaelekeza hivyo.

Juzi Afumwisye alisema kuwa anafanya utaratibu wa kukata rufaa ndani ya siku 45.
Wanatafuta sifa tu. Mbona hawajawatetea wafanyakazi kibao wanafukuzwa kazi kwenye makampuni ya Wahindi, Wachina na Waarabu n.k!!? Kama kweli aliandika maneno machafu dhidi ya mwajiri wake (Serikali) lazima afukuzwe kazi. Hata sisi tulioko kwenye private sector ukifanya ujinga huo kesho yake huna kazi.
 
Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
Technically waajiri wako ni Wananchi, kwahio ukiona hawatendewi haki ukakaa kimya ni unafiki.. Ni kama kwenu wanakula nyama za watu wewe ule tu sababu ni nyumba ya baba yako
 
Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
Mkuu hata kwenye private sector ukikashifu mwajiri wako unafukuzwa kazi mara moja. Huyu alistahiri kufukuzwa kazi mara moja. Tena disciplinary hearing yake imechukua muda mrefu sana tangu mwaka jana anakula mshahara bure tu.
 
Back
Top Bottom