Mawakili wanena kuhusu Mfanyakazi wa TRC aliyefukuzwa kazi kwa kupinga tozo

Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
Umefafanua vizuri sana.Wewe utakuwa ni msomi wa kiwango cha juu sana na una kipaji.Wajuwa wengine wanasomea kama udaktar,sheria,uhandisi nk,lakini hawana kipaji navyo.
 
Wanatafuta sifa tu. Mbona hawajawatetea wafanyakazi kibao wanafukuzwa kazi kwenye Kampuni ya Wahindi, Wachina na Waarabu n.k!!? Kama kweli aliandika maneno machafu dhidi ya mwajiri wake (Serikali) lazima afukuzwe kazi. Hata sisi tulioko kwenye private sector ukifanya ujinga huo kesho yake huna kazi.
Umesema kweli tupu.
 
Mkuu hata kwenye private sector ukikashifu mwajiri wako unafukuzwa kazi mara moja. Huyu alistahiri kufukuzwa kazi mara moja. Tena disciplinary hearing yake imechukua muda mrefu sana tangu mwaka jana anakula mshahara bure tu.
Ni kweli tupu,umesema.
 
TANZANIA HAINA UTAWALA WA KIFALME AU KIDIKTEKTA

Hii siyo nchini ya kiFamle, kiSultani au kiMalkia, hivyo serikali hii ni ya wananchi kwa ajili ya wananchi.

Tusimtwike rais aonekane rais-mfalme kuwa anaimiliki nchi hii binafsi au kwa ajili ya kikundi fulani kidogo.

Nchi za kifalme tena za kizamani ndiyo ilionekana ni kosa kuhoji sera, matamshi, matamko, ilani au visheni ya mtawala wa kifalme.

Democracy

Abraham Lincoln said, "Democracy is a rule of the people, for the people and by the people". It means that democracy is a form of government in which the rulers are elected by the people. The citizens of the country elect the Government to rule the country and the elected government work for the welfare of the people
 
Wanasheria mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu kufukuzwa kazi kwa Meneja wa Shirika la Reli nchini (TRC) Kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye huku baadhi yao wakionyesha nia ya kumpatia msaada wa kisheria.

Juzi, Afumwisye alipokea barua iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ikimjulisha uamuzi wa shirika hilo wa kumfukuza kazi kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuthibitishwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka jana.

Baadhi ya makosa anayotuhumiwa kuyafanya ni kupinga juhudi za Serikali za kuanzisha tozo kwenye miamala ya simu na pia kupinga chanjo inayotolewa kwa wananchi kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.

Kadogosa alibainisha makosa mengine kwenye barua hiyo kuwa ni kukashifu viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia makundi ya kijamii.

Wakizungumza kuhusu kufukuzwa kwa mfanyakazi huyo, mawakili mbalimbali wamesema wako tayari kumsaidia Afumwisye kwa sababu hajatendewa haki katika kufukuzwa kwake na wengine wamebainisha kwamba alikiuka kanuni za utumishi wa umma.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema yuko tayari kumtetea kijana huyo kupitia taasisi yake kwa sababu ana uhuru wa kutoa maoni yake.

“Sio fair (haki) kabisa, tena mwambie kabisa, mimi binafsi ninajitolea kumsaidia kumtetea kupitia sehemu yangu, kwenye vyombo vya kisheria. Yeye ni kama Watanzania wengine kama sisi na wengine wengi ambao wanahoji hizo tozo,” alisema Olengurumwa.

Wakili kiongozi kutoka kampuni ya Haki Kwanza, Alloyce Komba, alisema atakuwa tayari kumsaidia endapo atajua kesi yake ilitokana na nini, lakini kama ilitokana na tamko la Mkurugenzi Mkuu wa TRC, basi ataweza kusaidia.

“Sisi wanasheria tunasema hapana, ni unfair termination (amefukuzwa isivyo halali) ambayo haujafanyiwa judicial process (taratibu za kimahakama) kwa sababu tunasema hata mtu aliyeua dhahiri, lazima ufuate taratibu,” alisema Komba.

Aliongeza kwamba kuna taratibu za kumfukuza mtumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kumsikiliza, kumwonya na kisha kuchukua hatua kama aliyopewa ya kufukuzwa kabisa katika ajira yake.

Komba alisisitiza kwamba kwa nafasi yake kama mtumishi wa umma, jambo lake limepewa uzito na kwamba katika utumishi wa umma, kosa la kutotii mamlaka linatazamwa kwa jicho kali zaidi kuliko makosa mengine.

“Kwa hiyo, maoni yangu ni kwamba administratively (kiutawala), kuna hayo masuala ya insubordination (kutotii mamlaka), lakini legally (kisheria) ningependa kujua kama utaratibu wa kisheria ulifanyika,” alisema Komba.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole, alisema watu wana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kwamba hilo siyo sababu ya kumfukuza kazi ili mradi kazi zake anazifanya kikamilifu.

Alisema hata mtu aliyeko serikalini ana haki ya kutoa maoni na hadhani kama kufanya hivyo kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha utovu wa nidhamu kiasi cha mwajiri wake kumfukuza kazi.

“Mimi namshauri akate rufaa kwa sababu uamuzi huo unakiuka Katiba na sheria za nchi. Katiba haijasema watumishi wa umma hawana uhuru wa kutoa maoni, imesema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni,” alisema Kambole.

Alisisitiza kwamba Afumwisye ana haki ya kukata rufaa na kusikilizwa na kwa mazingira ya kufukuzwa kwake, anaweza kupatiwa msaada wa kisheria endapo mamlaka za awali zitaamua vinginevyo.

Mwasisi mwenza wa kampuni ya uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates, Onesmo Mpenzile alisema kosa kubwa ambalo linasimamiwa kwa ukali na Serikali ni kutotii mamlaka.

Alisema Ofisi ya Rais ndiyo inaongoza utumishi wa umma, hivyo mtumishi yeyote wa umma anatakiwa kuheshimu mamlaka za juu yake kwa sababu sheria, kanuni na utaratibu katika utumishi wa umma unaelekeza hivyo.

Juzi Afumwisye alisema kuwa anafanya utaratibu wa kukata rufaa ndani ya siku 45.
Ndiyo mjue tukisema kuwa sa10000 ni [emoji117][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90]
 
Pamoja na kukata rufaa kiutumishi nadhani huyu anaweza pia kufungua kesi mahakamani kwani inawezekana kabisa sheria ya usalama kazini haikuzingatiwa. Ipo wapi mahakama huru ya kulinda haki ya kila raia?
 
CCM ni ile ile, mtaji wao ni ule ule!
Watu wale wale, ujinga ule ule!

Masikini Tanzania! CCM imeihatamia mithili ya chatu mwenye njaa! CCM imetubana mbavu hatupumui, tunakoroma kwa upungufu wa uhuru, haki na usawa.

Kwa sababu ya ujinga uliokithiri, ni wachache sana ndani ya taifa hili wanaoelewa kuwa hata Rais ni mtumishi tu kama watumishi wengine.

Rais tumemwajiri sisi wananchi na mshahara wake anaolipwa unatokana na kodi zetu na pale akipoboronga tunatakiwa tumwajibishe.

Lakini kwa Tanzania hii yetu ambayo kwa ujinga wetu tumeiweka rehani mikononi mwa genge hili kuimilki kwa kivuli cha chama tawala, thubutu!

Na sasa hata kale ka uhuru ka kuikosoa serikali, sembuse viongozi tunaowalipa kututumikia, eti nako marufuku! Who's kidding who? Na bado!
 
Nakumbuka wakati nimeajiriwa serikalini, tuliambiwa, nanukuu.
"MTUMISHI HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA SIASA, LKN HAJAKATAZWA KUPIGA KURA AU KUCHAGULIWA PALE AKIONA INAFAA, LAKN MKUMBUKE PIA, HATA KAMA HUIPENDI CCM UWAPO KAZINI UJUE UNATEKELEZA ILANI YA CCM, USIMKASHIFU RAIS WA NCHI, YY NDIO MWAJIRI WAKO, NI KOSA KUMKOSOA BILA STAHA AU HADHARANI. UTAPOTEZA KAZI YAKO."

Huo ushauri, kila mtumishi anaambiwa, huwezi kumkosoa aliyekuajiri hata siku moja. Sheria zetu zinaeleza wazi kabisa. Hao wanasheria wanajidanganya tu. Ni sawa umtukane Baba yako afu akufukuze nyumbani usema ni haki yangu kukaa hapa, Haiwezekani.
Taja vifungu hivyo vinavyoeleza wazi mkuu...
 
CCM wanajiona kama miungu watu vile. Wanafanya mambo ya hovyo, halafu wenye akili wakiwakosoa, wanawafanyia zengwe.

Yote aliyoyasema yana mashiko! Tozo zimezidi, na zinaumiza wananchi wa kipato cha chini! Na pia hiyo chanjo ya corona haina tija yoyote ile! Zaidi tu imetokana na shinikizo kutoka kwa mabeberu.

Sasa kwa nini wamfukuze kazi, na wakati amesema ukweli mtupu! Mbona hawa chawa wanaosifia kila kitu hawafukuzwi kazi? Au imefikia wakati wananchi wanatakiwa kisifia tu! Kamwe jambo hilo haliwezekani.

Katika maisha haya ya Africa kushindana naa watawali nikazi ngumu ila kuna watu wapo na kazi yao ni kuwasemea watu Vyama Vya siasa nao wapo kimya wanalamba Asali si Mama Tanzania ,Cuf iwe chandema wanasubilia uchaguzi
 
Back
Top Bottom