Tetesi: Mawaziri 10 Kutemwa Baraza Jipya, hofu yatanda watu wakihaha kwa sangoma

Tetesi: Mawaziri 10 Kutemwa Baraza Jipya, hofu yatanda watu wakihaha kwa sangoma

Hilo si lakusema kwenye maswala maslahi yao weee huwa wanaungana hakuna cha wapinzani wala chama cha mambuzi wote kapu moja
Hili Nina ushahidi nalo,ndio maana sipendi kabisa wanasiasa ndio waongoze harakati za Katiba mpya..

Hao kwenye maslahi wako pamoja ,huwatumia Wananchi Kama daraja tuu
 
Gutter Politics, alichokifanya Dr Kimei CRDB kila mwenye akili anafahamu.

Wenye mapenzi mema na nchi hii tulitajia Dr Kimei ndio angeteuliwa kuwa Gavana wa BOT baada ya Profesa Beno Ndulu, lakini kwa chuki zake kwa Wachaga yule shetani wenu wa Chato akamuweka pembeni na kumlazimisha kustaafu CRDB.
Gavana wa Sasa anafanya kazi nzuri ukiacha ule upuuzi wa kupora Pesa za watu chini ya Jiwe.

Huyu bwana ametajwa na majarida kibao ya Mambo ya Fedha Africa na Duniani kwa kusimamia vyema Sera za Uchumi na amewahi pata tuzo mwaka Jana ya Central banker of the year na pia alikuwa miongoni mwa magavana kumi Bora Duniani.
 
Wabongo ni wezi sana,, pm anajitahidi sana kupambana😄
Sasa kama kashindwa kukomesha wizi si ina maana kashindwa kazi.Anapaswa kuwa mkali.It is easy, watolewe kafara a few wawe mfano,wengine watanyooka.Tukienda hivi kwa kubembelezana bembelezana hatufiki.
 
Mwizi, mtoa rushwa etc. Hafai kabisa. Nina uhakika hakuna mamlaka itakayompatia kimei uongozi serikalini kwa sababu ni mwizi, jambazi, mtoa rushwa na mla rushwa mkubwa. Hana tofauti na akina Mafuru wezi wezi na wala rushwa
Mbona unatoa tuhuma nzito namna hii bila ushahidi wowote mkuu.Hasira hizi zinaonyesha kwamba kuna chuki binafsi.Kama una ushahidi lete,vinginevyo huu utabaki kuwa udaku.To me Kimei is a serious person na kwa jinsi alivyoitoa CRDB from ground zero na ikawa na ufanisi mkubwa,angeweza kabisa kutusaidia Wizara ya Fedha.
 
Mabosi nao wanakuwa na favourite chawa.

Ebu angalieni vizuri video za Bi Tozo kwenye mikutano yake. Yaani wengine wakimpamba anasikiliza tu. Hila Mwigulu akianza kumpamba maza dakika moja uso unajawa na tabasamu la ajabu.

Binafsi sitegemii amtoe favourite pet (Mwigulu) nje ya uwaziri anapenda huyo mtu anavyompamba.
 
Shabiby anatakiwa atuambie; ameua tembo wangapi! Alikuwa anauza wapi pembe zao! washirika wake ni akina nani!
 
Hao Mawaziri wapya anawatoa nje ya mfumo wa CCM?maana CCM ni sawa na gari bovu injini,sasa ukitaka gari yenye injini mbovu ikimbie,unabadilisha injini,sasa kinachofanyika sasa badala ya kuweka injini mpya tunabadilisha tairi[emoji1787].
Kama tunataka tuende mbele inatakiwa Rais awe na uwanja mpana wa kuteua,asilazimishwe kuteua Mawaziri kutoka Bungeni tu,aende mpaka nje ya Bunge.Hawa wakina Mwigulu,Biteko na Jafo na PhD zao za mchongo hatutafika kwa kweli!
Umeandika ukweli mtupu.
Hii comments inafanya huu uzi ufungwe tuu,maana kila kitu umemaliza.
 
Mawaziri wengi anaowapenda Bimkubwa wanatumia madaraka yao na kazi za kuzurura majukwaani na vijijini kujikuza kisiasa.
Mawaziri wengi vijana wanahaha na harakati kibao kwenye jamii eti wanadai Mama hatoshi wao ndo wanafaa na wanautaka urais wa Bimkubwa!
Bimkubwa usikubali wakuangushe usiwaonee aibu toa vijana wajinga , wazee wachovu weka sura mpya za kazi, bongo inachosha sana kuna watu ni mawaziri tangu uhuru na nchi ni maskini tangu uhuru , hivi hakuna watu wengine baraza jipya sura za zamani zimechoka mawazo ya kizamani baraza jipya weka sura mpya mawazo mapya!!
 
Wizara ya ardhi wakibakizwa hawahawa waliopo itakuwa haina maana kabisa
 
Kama Kassimu mtu aliyeshindwa majukumu ya uwaziri mkuu na kugeuka nyapara wa kuangalia kama Simtank imekuwa installed au la ataendelea kuwa waziri mkuu basi hamna chochote hapo ni cosmetic change!.

Apige chini Kassim alete Waziri mkuu wa viwango, siyo waziri mkuu wa Jiwe.
Wewe unachuki ndo maana huoni uchapakazi wa waziri mkuu.na hatoki mpaka amalize muda wake.
 
Back
Top Bottom