Mawaziri hawa watano utumishi wao haujatukuka

Mawaziri hawa watano utumishi wao haujatukuka

Kuna mmoja anasura ya songesha na mwingine nipigetaf
 
Kunaumuhimu mawaziri Hawa wawe wanaomba hizo nafasi Kwa vigezo ,nadhani ndohoja yake
Hoja yake wawe wamepitia utumishi Sasa Si tutatengeze gang la wababe maana watumishi wataona wao ndo wanahaki ya kushika nyadhifa za kisiasa na fursa ya kuingia kwenye siasa ni nyembamba
 
Wana Bodi,

Kuna Mawaziri 5 ambao sina uhakika sana na rekodi zao katika Utumishi wa Umma hivyo mambo mengi yanayohusu Public Fund hawayajui na wanadhani wakiwa Mawaziri wanaweza kufanya maamuzi yoyote kuhusu fedha za Umma bila kufuata sheria za nchi.

1. Mwigulu Nchemba sijui rekodi yake kama aliwahi kuajiriwa Serikalini kama mtumishi wa umma ninachosikia ni kwamba aliwahi kuwa BOT kwa muda mfupi sana baadaye akatumbukia kwenye siasa sina uhakika na uzoefu wake kwenye eneo la utumishi wa umma na sasa ni Waziri wa Fedha.

2. Januari Makamba, yeye historia yake siijui imekaaje na sijui hata kama aliwahi kuajiriwa kama Mtumishi wa Serikali zaidi niliwahi kusikia alifanya kazi kwenye kambi ya wakimbizi kwenye Shirika la UNHCR na baadae akatumbukia kwenye siasa na kuwa msaidizi wa Rais na sasa Waziri. Sijui uzoefu wake katika utumishi wa umma na ufahamu wake wa kutosha kuhusu mambo ya Serikali. sasa ni Waziri wa Nishati.

3. Hussein Bashe, yeye hata historia yake ya haieleweki zaidi niliwahi kusikia alikuwa akifanya kazi kwenye gazeti la Mtanzania na baadaye akatumbukia kwenye siasa na sasa ni Waziri sijui hata aliwahi hata kuajiriwa serikalini na kujua mambo ya Serikali yanavyokwenda. Sasa ni Waziri wa Kilimo.

4. Nape Nauye, yeye historia yake hata ya elimu haijulikani lakini baadaye akatumbukia kwenye siasa mara akapewa Uenezi wa CCM mara DC na sasa Waziri wa Wizara kubwa ya TEHAMA sijui kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali na kufahamu mambo ya Serikali.

5. Prof. Makame Mbarawa 'Mzee wa Mkataba wa Bandari' yeye sijui hata historia yake ya elimu na hata sijui aliwahi kufanya kazi wapi zaidi tulimuona kwenye siasa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na Jakaya na sasa ni Waziri wa mambo ya Reli, Bandari na ANGA sijui hata kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali.

Na ndiyo maana Mawaziri hawa kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa utumishi wa Serikali na namna ya usimamizi wa Fedha za Umma ndiyo sababu wizara zao zinakubwa na kashfa lukuki kila siku kuhusu matumizi ya fedha za Umma.

Ninachokiona mimi Siku Rais Samia Suluhu Hassan atakapoondoka madarakani ambaye ndiye wanayemtegemea kama Kinga yao hao Mawaziri 5 waitashia kufungwa gerezani kwa makosa makubwa waliyofanya wakiwa kwenye nafasi zao za uwaziri. vinginevyo labda waamue kukimbia nchi na kuishi ughaibuni.

Taarifa zilizopo wengine wameshaanza kuhamishia familia zao kwenye makazi yao mapya huko Dubai.

View attachment 2718757
Mwigulu Nchemba

View attachment 2718758
Januari Makamba

View attachment 2718760
Hussein Bashe

View attachment 2718762
Nape Nauye

View attachment 2718764
Makame Mbarawa
Anza na mkuu wao ambaye kilembe kinampwaya! Hana ubavu wa kuongea lolote baada kuhonga bandari zetu kwa wajomba! Mwanae anampa uwaziri usiokuwepo!
Kiongoz pekee aliyeweza kuratibu rushwa na kugawa raslimali zote!
 
Uhusiano upo Mkuu ukiwa umewahi kuajiriwa serikalini Sheria nyingi za utumishi na mambo ya usimamizi wa fedha za umma utazijua mfano mtu aliwahi kuwa Mwalimu, akaja akafanya kazi Halmashauri hata Mkuu wa Idara, akaja akawa DC, akafanya kazi Wizarani hata leo akiwa Waziri atamudu majukumu yake vizuri atakuwa na upeo mkubwa wa mambo ya Serikali.
Huelewi unachosema. Hakuna uhusiano huo unaodai wewe. Hata hao unaowaona wewe wanafanya vizuri sio wote wametokea huko utumishi wa umma. Kwani huko idarani hakuna mapungufu? Halmashauri hakuna rushwa? Hakuna deals?
Halafu umefikiri vizuri au umeongea utoto tu?
Elewa kuwa changamoto zote unazoziona ni za kimfumo! Kuanzia katiba hadi sheria zake.
Mfano tu hapa.....Donald Trump angekuwa kiongozi wa hovyo sana kwa tabia zake kule USA. Hata matokeo ya uchaguzi angeweza kugomea.Lakini kilichosaidia ni uimara wa mifumo yao.
 
Wewe tangu kujitambua kwako umepigia kura marais wangapi? Ni nani kati yao kaifata na kaisimamia hiyo sheria?


Rais ni mtumishi wa Ummah ama Serikali?

Mipaka ya ummah na serikali iko wapi na inalindwa na nani?
kama huelewi kitu Bora unyamaze, hivi unafikiri waliowekwa hizo Sheria ni wajinga?
 
Back
Top Bottom