Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.
Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.
Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.
Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?
Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?
Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.
Hongera sana Selemani Jafo, PhD.