Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Sasa kama unaweza kumlipa mtu hadi m5 akuandikie PhD thesis utashindwa kutoa m2 ili uandikiwe machapisho mawili tu? Mbona kazi rahisi sana hiyo!?
Kaka usifanye mchezo na "chapisho kwenye reputable journal", hakuna janjajanja, Editors and Reviewers wapo makini haswaa!! Sababu kubwa ya watu kushindwa kumaliza PhD ni publications! Mimi binafsi siwezi kuchukua hela yako na kukuahidi tutatoa chapisho kwenye journal inayoeleweka, hata kama hiyo field nipo mtabe kupita maelezo
 
Yote ni ma CCM . Kuna huyu pro pesa Lipumba anatembea Na miswaki Na Taula kwenye briefcase , laana ya kushirikiana Na CCM

Taratibu mkuu. Profesa Lipumba ni profesa kweli kweli. Ni mmoja wa econometricians wazuri sana nchini. Huko nyuma nilibahatika kuhudhuria wasilisho lake moja la kitaaluma katika mhadhara mmoja huko nje uliohudhuriwa na mabingwa wa uchumi nilijisikia proud kuwa Mtanzania. Very impressive. Watu walimvulia kofia.

Siku hizi namuangalia profesa na kujiuliza nini hasa kilichomtokea? Nchi hii sio nzuri kwa wasomi. Si viongozi; si wananchi hawana namna ya kupima na kuthamini kazi za wasomi. Bali wanachangamkia zaidi propaganda za nguvu toka kwa wanasiasa. Profesa naye akaona heri ajitose huko (kwenye siasa) akitegemea kuambua ukwasi na umaarufu.

Bahati mbaya huko kuna wenyewe. Alisahau ile hekima inayosema: β€œnever argue with fools, β€˜cause they will drag you down to their level and beat you with experience”! Angebaki tu kwenye maisha ya kitaaluma. He has been doing fine. Bado ni consultant mzuri; familia iko ok. Siasa imechafua sana taswira yake. What for? I’m puzzled.
 
Ni sawa na Masters ya Aloyce Kwezi hapo Tumaini Iringa. Alikuwa anasoma jioni. Jamaa hawezi hata kuongea na kuandika jina lake anapewa na A tu. Maisha haya.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jana Aweso nae kapata master ZnZ. Anadai alipata bachelor UD. Sasa uwezo wa kurudi UD umekwenda wapi hadi akakimbilie Open University tena ZnZ?
 
Una paper ngapi Chief?
Nina Paper 4 , 2 mimi ndio author wa kwanza kwa sababu nilikuwa PI na hizo 2 nyingine ni co-author ila journal zote ni SCI Indexed...kama ni kusaidia watu kuandika basi nimefanya za kutosha na kuchagua kutotokea kwenye majina kwa sababu ni papers za watu wanaoenda kugraduate na mimi nakuwa nipo nyuma kama ghostwriter, na kwangu mimi sasa sina manufaa hata nikitokea.

Kuandika paper na kuwa published kama upo focused its not a big deal the big deal ni citation impact ya ulichoandika....kuna kipindi nilitaka kuingia kwenye academics lakini niliishia kuona ni system ambayo inazidi kuharibiwa kutokana na politics kwenye institutions zetu nyingi . Field yangu ya specialization ni Computer Engineering japo nimeingia zaidi kwenye upande wa IT kutokana na kupata opportunities nyingi upande huo.
 
Aah kuwa na phd sio tija kwa sasa,maisha sio vyeti, vyeti mapambo
 
Hongera sana Kiongozi, najua unajua furaha unayopata siku waheshimiwa waki-accept paper yako, na unajua pia email ya Rejection inavyouma, All in all siyo jambo rahisi
 
Nimerudia tena maandishi yako nakuona kama bwege vile! Hapa siyo jukwaa la kusifu watu. Hiyo Ph.D unayo? Kama unayo, iweke hapa ili tukusaidie kuonesha kwamba imekopiwa au la! Hizi ni enzi za e-life!
 
Kupublish paper kwenye reputable journals hata sio kazi kivile tusitishane[emoji205]
Inategemea journal gani...Science? Nature? Lakini MalariΓ  Journal one can attempt ( impact factor???)
 
Selemani Jaffo na kete ya Urais wa nchi 2030 kama CCM itafanikiwa kuzima vuguvugu la katiba hadi wakati huo.
Kwahyo Sasa tunatafta PhD nyingine ya Urais ka ya Ile ya maganda ya korosho tena
 
Jana Aweso nae kapata master ZnZ. Anadai alipata bachelor UD. Sasa uwezo wa kurudi UD umekwenda wapi hadi akakimbilie Open University tena ZnZ?
Open university ni chaka la degree hewa wanasiasa wanaipenda kweri kweri in JPM voice.
 
Open university ni chaka la degree hewa wanasiasa wanaipenda kweri kweri in JPM voice.

Huko ukiandika thesis ya mbio za mwenge kesho unapewa phdπŸ˜›
πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›
 
Kina mtu alitegemea waziri akose PHD??? Serious.
Tena udom
Kheeee
 
Nenda pale UDSM kaulizie. Au fanya search tu kwenye google utaona. Kama hilo pia huna muda, fuata hii link hapa halafu tazama namba 16: https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/colleges/coss/postgraduate-programmes
Kwamba Wakishamaliza course work unaondoka? No research? jibu hili swali..
Kwanza kwa Tanzania hakuna chuo kitakutunuku PhD kama hujasoma angalau miez 30.
Sasa Ina maana muda wote huo ni course work tu. Eti nikaulize UDSM we jamaa.
Na kwa regulation mpya za TCU hakuna mtu atagraduate masters/ PhD bila kupublish research yake ule muda wa kukusanya dissertation na kuondoka umepita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…