Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.

Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.

Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.

Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.

Hongera sana Selemani Jafo, PhD.
Title hii hapa
jafo.jpeg
 
Nimeweka title ila mh!!!! siweki neno langu
Hyo title ka ya wakenya tu ingawa watu wanatetea sisi ilikuwa title au proposal ikiingizwa kwa plagiarism u copy utajua hujui moto wake ila vile mwanasiasa atapata watetezi. Hyo disertation ni editing nothing new labda na Ku change sample size, location na methodology basi
 
Hivi kweli ndizo PhD za siku hizi zilivyo?
 
PHD za bongo za wanasiasa ni chenga tu,wanachojali ni heshima tu,hakuna manufaa yoyote ukilinganisha walipokuwa na shahada na sasa Wana PHD!!ni mbwembwe tu,
Watu wangapi wanajua DP William Ruto ni PHD holder!!wachache sana,kwa sababu yeye anajari hiyo PHD inafanya nini,sio kuitumia kama cheo,
Kuna mbwiga mmoja,alitaka tuamini anayoyasema kuhusu uchumi!kwa vile tu ni Dokta wa uchumi!!hajawahi hata kushauri au kuendesha kampuni,kisa kadesa na kupata PhD,anataka tutetemeke
"VP" hapo kwa Ruto. Huyo mbwiga mmoja bila shaka ni Lameck Madelu aliyetuambia tuhamie Burundi.
 
Jana Aweso nae kapata master ZnZ. Anadai alipata bachelor UD. Sasa uwezo wa kurudi UD umekwenda wapi hadi akakimbilie Open University tena ZnZ?
Apewe uwaziri wa maji huko huko Zanzibar.
 
Garissa na Tanzania wapi na wapi case kufanana sio hoja data zitakuwa tofauti kabisa Jafo zake za Tanzania huyo zake za Kenya huwezi kusema Ni copy and paste mfano mmoja akifanya case study ya Covid 19 ujerumani na mwingine akafanya case study ya Covid 19 Tanzania huwezi sema wa Tanzania ka copy and paste case study ya ujerumani .Ni case tofauti zenye Takwimu tofauti
Hata kama "data collection" zimefanyika katika sehemu mbili tofauti, lakini kama kuna mfanano wa "title, problem statement, research questions & objectives" na pia kwa "research design" basi hiyo kitaaluma ndiyo "plagiarism" yenyewe.
 
Ninafuraha sana kuona watu wanaweka juhud katika elimu, kutafuta mafanikio katika maisha & kufanya ibada hii inanipa nguvu ya kutimiza malengo yangu na kuamini hakuna kinacho shindikana wala sijachelewa
 
Garissa na Tanzania wapi na wapi case kufanana sio hoja data zitakuwa tofauti kabisa Jafo zake za Tanzania huyo zake za Kenya huwezi kusema Ni copy and paste mfano mmoja akifanya case study ya Covid 19 ujerumani na mwingine akafanya case study ya Covid 19 Tanzania huwezi sema wa Tanzania ka copy and paste case study ya ujerumani .Ni case tofauti zenye Takwimu tofauti
Unajua maana ya PhD wewe. Acha kitu hujawahi fanya, PhD ni kuongeza knowlege katika ulimwengu wa elimu bwashee
 
Hata kama "data collection" zimefanyika katika sehemu mbili tofauti, lakini kama kuna mfanano wa "title, problem statement, research questions & objectives" na pia kwa "research design" basi hiyo kitaaluma ndiyo "plagiarism" yenyewe.
PhD lazima kwanza ufanye literature review ili ikusaidie kukuonesha kuwa hiyo kitu unayotaka kufanya haijawahi fanyika popote duniani na kama ilishafanyika ni nini kilikosekana ili wewe ujazie. cariha njoo uwasiadie hawa marafiki zangu akina YEHODAYA (wangekuwa ni akina brazaj wangenikoma)
 
Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.

Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.

Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.

Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.

Hongera sana Selemani Jafo, PhD.

Hizo PhD za kisiasa peleka huko!! Hakuna profesa hata mmoja aliyewahi ku-deliver nchi hii!! prof Kapuya alitumia helkopta ya jeshi kwenda kusalimia majirani zake Tabora! Profesa Mhongo/mwongo alisema pesa za escrow si za umma wakati ni za umma na zilikuwa zinatunzwa benki kuu, Profesa Lipumba alitumika kusambaratisha chama kikubwa cha upinzani kisha akajikuta ametumika kama ............ kisha kutupwa kwenye dust bin!!! Profesa Kawambwa alichofanya kwenye wizara ya elimu anakijua mwenyewe!! Kwa hiyo hatutegemei msomi wa bongo aliyesoma akiwa na malengo ya kufaulu tu na kufaulu kukawa ndio mwisho wa upeo wake, anaweza kuwa na jambo lolote la maendeleo!!
 
Andikiwa na wewe ukachukue mkuu
Dada mbona unawaka hivi huyu jamaaa akiambiwa ukweli!?
Hivi nani asiyezijua hizi PhD za viongizi wetu!??/
Labda uwe kilaza lakin sisi tuliofuta ujinga tunazijua!!!
Halafu kwa taarifa yako hazina mchango wowote kwa maendeleo ya taifa!!!! In shirt niushamba tuuu!!!
Nikutakie jion njema !!! Anti
 
Hizi. PhD ni feki na hazina msaada kwa nchi wala wananchi!!
Zingekuwa ni fruitful tusingekuwa na shida ya maji,umeme,ajira nk
Kwa kifupi ni useless
 
hizo PhD zinaweza kupunguza watu wa majajalani kama yule Kaboud
 
Nimerudia tena maandishi yako nakuona kama bwege vile! Hapa siyo jukwaa la kusifu watu. Hiyo Ph.D unayo? Kama unayo, iweke hapa ili tukusaidie kuonesha kwamba imekopiwa au la! Hizi ni enzi za e-life!
Wewe ndiyo bonge ya bwege.
 
Kwamba Wakishamaliza course work unaondoka? No research? jibu hili swali..
Kwanza kwa Tanzania hakuna chuo kitakutunuku PhD kama hujasoma angalau miez 30.
Sasa Ina maana muda wote huo ni course work tu. Eti nikaulize UDSM we jamaa.
Na kwa regulation mpya za TCU hakuna mtu atagraduate masters/ PhD bila kupublish research yake ule muda wa kukusanya dissertation na kuondoka umepita.
Mkubwa nimekuwekea link hapo, kama haijakutosha waulize wenyewe.
 
Hawa wanapewaga tu hizo PhD. For prefix use only, kichwani weupee.

Reseach wanaandikiwa wanaenda kuwasilisha tu.

Au kadesa kama jiwe
mzee PHD sio masters nenda wewe kajaribu uandikiwe afu uone mziki wake, hupewi ng'oo lazima ubukue na huipati hivi hivi, labda katika vyuo visivyofahamika huko mashinani ila kwenye vyuo credible mzee hutoboi, na ndio maana huwachukua muda
 
Back
Top Bottom