KERO Mawaziri wa Elimu na TAMISEMI, Shule ya Msingi Nyerere, Moshi kuna shida kubwa. Tunaomba mtusaidie

KERO Mawaziri wa Elimu na TAMISEMI, Shule ya Msingi Nyerere, Moshi kuna shida kubwa. Tunaomba mtusaidie

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Elimu NI pesa.Hakuna Elimu bure.ndo muelewage.ndo maana wakwao hutawakuta huko mnakoambiwa elimu bure.akili za kuambiwa changanya na zako.mtabakia kuwa na watu wanaojua kupiga kura tu.wenzenu wanatengeneza wapigiwa kura.
Ni kweli hakuna elimu bure. Lakiji wanancjo ndio wanaolipia kupitia kqenye kodi wanazolipa, Wasimamizi wake hawawezi kugeuza jambo hili kuwa wanatufanyia hisani.
 
Unalijua eneo husika na makazi ya wazazi? Hili jambo lilitakiwa lifanyike mwaka jana kabla ya shule kufunga.
Isingeleta tofauti, umbali utazingatiwa, wasiliana na mkuu wa shule na Afisa Elimu Kata kwa usaidizi zaidi.
 
Mkuu.

Pole kwa masaibu yaliyokukuta. Nchi hii hawa watu wanaojiita watoa maamuzi wanaipeleka ndiko siko.
Wanawageuza watanzania kama wakufanyia majaribio. Wiki iliyopita maafisa elimu kata na wilaya 1750 kutoka mikoa sita nchini, walikuwa Butimba kwa semina ya siku mbili juubya mtaala mpya!

Maafisa hawa walipaswa ndani ya wiki hii kuwakusanya aalimu wa maeneo yao na kuwaelekeza juu ya nini cha kwenda kufanya kuhusu mtaala mpya! Hakuna maandalizi kama inavuotokea kwa jizo English Medium, ingawa siziungi mkono
Ndugu John Maviatu, mtaala mpya hauanzi mwaka huu, mbona huelewi? Huko shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Habari kaka? Sisi ni wazazi wa watoto wanaosoma shule ya msingi JK Nyerere, iliyopo Manispaa ya Moshi. Mwaka jana uongozi wa shule uliitisha kikao cha wazazi na kueleza nia ya serikali ya kuigeuza shule hiyo kuwa ya mchepuo wa kiingereza (English Medium school).

Katika kikao hicho wazazi tulihoji hatma ya watoto wetu wanaosoma hapo. Tukajibiwa hakuna athari zozote zitakazotokea kwani wanafunzi wa darasa la pili hadi la 7 wataendelea na masomo yao katika mchepuo wa Kiswahili, isipokua wale watakaodahiliwa darasa la awali na la kwanza ndio wataanza na mchepuo wa kiingereza.

Lakini jana tumepigiwa simu kwamba kila mzazi mwenye mtoto shuleni aende akajaze fomu ya kumhamisha. Tukauliza kwanini wahamishwe wakati tuliambiwa wataendelea na masomo hapohapo. Na kwanini iwe ghafla hivi? Tukajibiwa DEO amesema watoto wote waondolewe.

Tukampigia simu hakupokea. Leo tumefika shuleni tukapewa hivi vikaratasi tujaze ili kuhamisha watoto wetu. Unajaza jina la mwanafunzi, darasa alilopo na shule unayotaka ahamie. Shule nyingi ziko mbali na mtoto atalazimika kupanda gari mbili kufika. Huu usumbufu ni kwa gharama ya nani?

Sisi wazazi tunaona hatujatendewa haki. Kwanini hatukushirikishwa mapema? Kama mpango ulikua ni kuondoa wanafunzi wote si wangetuambia tangu mwaka jana ili wazazi tujipange? Wanakuja kutuambia leo, zimesalia siku mbili shule zifunguliwe, wanataka tufanyeje?

Na bahati mbaya hakuna wa kutusikiliza. Hata ofisi ya Mbunge tumeenda lakini hatujasikilizwa. Tumeomba kikao na Afisa elimu lakini amekataa na kusema maelekezo aliyotoa hayana mjadala. Kama mwanzoni aliitisha kikao na wazazi, kwanini sasa hivi anaogopa kuitisha kikao kutueleza mabadiliko yaliyojitokeza? Kuna siri gani nyuma y pazia?

Hivi mtoto wa darasa la 7 unamtoa leo kumpeleka shule nyingine ataweza fanya vyema? Kwanini hili suala wamefanya kwa mabavu? Halafu kama watadahili darasa la awali na la kwanza tu kama walivyoeleza, hayo madarasa mengine yatatumika kwa ajili ya nini? Je yatabaki wazi kwa miaka 6 ijayo? Si yatageuka magofu? Kwahiyo wameona bora yageuke magofu kuliko watoto wetu waendelee kusoma hapo?

Tunaomba utusaidie kupaza sauti.

View attachment 2862256
Nendenikwamkuuwamkoaaaa acheniujinga

Wawilayaa hana.msaadaa kwahili
 
Afisa elimu amechukua ushauri toka kwa mchepuko wake ambaye hajasoma.
Hivi hivyo vyumba vingine alitaka mchepuko wake ufanye sehemu ya mamma ntilie?
Hawa watu wasio na upeo wanapewaje vyeo?
Hebu hamisheni huyo mtu kwenda wilaya ya same kule Chome au Mbaga.
 
Elimu NI pesa.Hakuna Elimu bure.ndo muelewage.ndo maana wakwao hutawakuta huko mnakoambiwa elimu bure.akili za kuambiwa changanya na zako.mtabakia kuwa na watu wanaojua kupiga kura tu.wenzenu wanatengeneza wapigiwa kura.
Kuongea kiingereza kwako ni elimu na inatakiwa ilipiwe zaidi! Nyerere angekuwepo angesema neno moja tu "UPUMBAVU", yaani kusema "yes sir" nilipie! Nchi ya majuha tumefanya kusema kiingereza ni sawa na kuangalia mechi ya ManU na Man City! Tulipie.
 
Afisa elimu amechukua ushauri toka kwa mchepuko wake ambaye hajasoma.
Hivi hivyo vyumba vingine alitaka mchepuko wake ufanye sehemu ya mamma ntilie?
Hawa watu wasio na upeo wanapewaje vyeo?
Hebu hamisheni huyo mtu kwenda wilaya ya same kule Chome au Mbaga.
Hayo si maamuzi yake yeye anatekeleza maagizo ya mama.
 
Kuongea kiingereza kwako ni elimu na inatakiwa ilipiwe zaidi! Nyerere angekuwepo angesema neno moja tu "UPUMBAVU", yaani kusema "yes sir" nilipie! Nchi ya majuha tumefanya kusema kiingereza ni sawa na kuangalia mechi ya ManU na Man City! Tulipie.
Kwenye mchango wangu nimezungumzia kiingereza?kiingereza NI lugha Tu kama kisandawe.mi nimesema elimu inahitaji pesa kama mnalijua Hilo waacheni watt wenu hapo na mlipie au wahamisheni kama mlivyoambiwa,wapelekeni kule kwa bure.
 
Mleta Mada ameelekeza swala lake kwa Waziri TAMISEMI.
Yupo sahihi kwa mtazamo wangu,aingilie kati kuepusha usumbufu kwa wazazi.
Halmashauri ya manispaa Ina maeneo mengi,wajenge Shule mpya kuepusha kadhia kwa wazazi.
Afisa Elimu anatekeleza maagizo toka kwa mwajiri wake,hawezi kwenda tofauti na maelekezo aliyopewa
 
Mabadiliko ni Jambo la kawaida katika harakati za maendeleo shida inayooneka hapa ni ucheleweshwji wa Taarifa ya kuhamisha wanafunzi wakati shule zinakaribia kufunguliwa.
kwa hakika mabadiliko hayakwepeki. Lakini je? Hayo mabadiliko yamelenga nini? Ni mabadiliko kutoka hasi kwenda chanya?

Na je, na hili mi la msingi. Ingekuwa mabadiliko ndani ya famolia ya DED hakuna ambaye angehoji. Lakini kwa kuwa yanahusisha jamii, hakuna budi kuwa SHIRIKISHI. Haipendezi kwa wanaojiita maofisa kutoa maamuzi bila kuwashirikisha wananchi ambao ndio wanufaika.
 
Kwenye mchango wangu nimezungumzia kiingereza?kiingereza NI lugha Tu kama kisandawe.mi nimesema elimu inahitaji pesa kama mnalijua Hilo waacheni watt wenu hapo na mlipie au wahamisheni kama mlivyoambiwa,wapelekeni kule kwa bure.
Hoja, yaani walipie kwa ajili ya kiingereza tu! Ni upumbavu. Mimi sikubaliani na kuwaambia walipie ili wajue kiingerza au wawsondoe watoto wao kama hawana hela ya kujifunza kiingereza wawaondoe wawapeleke uswahilini!
Wewe unaposema waioweza kulipa wawaondoe watoto wao ni kuunga mkono biashara ya lugha ya kiingereza kuwa ni elimu.
 
Back
Top Bottom