Mawaziri wafanya kikao Lushoto kutafuta suluhu ya migogoro ya Wananchi Mkoani Tanga

Mawaziri wafanya kikao Lushoto kutafuta suluhu ya migogoro ya Wananchi Mkoani Tanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mawaziri saba wa kisekta wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Mbunge wa Lushoto wamekutana wilayani hapo kujadili utatuzi wa changamoto na migogoro inayowakabili wananchi mkoani Tanga ikiwemo ya ardhi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Tanga.
fe71751a-d237-4769-8af0-16207ac55a0d.jpeg

Mwenyekiti wa kikao kazi hicho, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Asiatu Kijaji ameongoza kikao hicho cha viongozi hao na watalaam wa Wizara za Kisekta ambacho kitawasilisha mapendekezo ya utatuzi wa migogoro na changamoto hizo za wananchi kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga, ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki.

Katika kikao kazi hicho wananchi wenye changamoto mbalimbali wamepata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao na kusikilizwa na viongozi hao, ikiwa ni sehemu ya kukiwezesha kikao kazi hicho kuandaa mapendekezo na kutoa ushauri utakaowezesha kupatikana kwa suluhu ya utatuzi wa migogoro na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi mkoani humo kwa muda mrefu.

Ili kutatua changamoto na migogoro ya wananchi, Prof. Shemdoe ameshauri wataalamu wa Wizara za Kisekta kuwa na utamaduni wa kuwashirikisha wananchi ili kuepukana na migogoro inayoweza kuepukika kwa ushirikishaji wa wananchi.
fe011ae7-f2ac-4294-bfee-434c21a6fb3d.jpeg
0aaa6b1c-f29f-4ba0-8f0a-0b3e65338232.jpeg

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao kazi hicho, Prof. Shemdoe amemshukuru Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kuguswa na changamoto na migogoro inayowakabili wanachi wa mkoa wa Tanga na hatimaye kuelekeza Mawaziri wa kisekta kukutana Lushoto ili kusikiliza migogoro ya wananchi na kupendekeza namna ya kuitatua.
28a7b789-9382-49a2-b865-4208a49282a5.jpeg

Mawaziri wengine walioshiriki kikao kazi hicho ni Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mhe. Bashiru Ally Kakurwa, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Waziri wa Ardhi na Makazi Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde na Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali.

OWM - TAMISEMI, Lushoto
 
Hz kero zitaisha lini? Ni kweli huwa zinapatiwa ufumbuzi au ni maigizo? Tuliona kipindi cha mzee Magu, kipindi cha Makonda akiwa mwenezi na sasa Nchemba..Kweli Tz kuna manyanyaso serikali kazeni buti nimefatilia kero za Tanga wale wazee wamenihuzunisha sana.Ingependeza baada ya ufumbuzi wangeletwa tena kutoa ushuhuda wa kero zao zilivotatuliwa.
 
Nchi haina waziri wala mbunge bali ina wahuni, majambazi na wauaji waliopora mamlaka ya wananchi, wakagawana madaraka. Hawa ni aheri ya wakoloni kuliko hawa watumishi wa shetani
 
NAIMANI KERO YA BONDO ITATULIWA BAADA YA WAKAZI ZAIDI YA 7000 KUFUKUZWA BONDO MSWAKI KILINDI TANGA
 
Hamna Waziri wala Mbunge hapo wote ni haramu......tena wao wenyewe wanalijua hilo ndani mwao.
 
Back
Top Bottom