Mawaziri Wakuu wa Israel na Uingereza wabwatukiana!

Mawaziri Wakuu wa Israel na Uingereza wabwatukiana!

Uingereza kusitisha mazungumzo ya biashara huria na Israel; Wizara ya Mambo ya Nje yasema hatua hiyo 'haitaizuia' Israel katika 'pambano lake na Magaidi'

Kufuatia tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy mapema leo la kusimamisha kwa Uingereza mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria na Israel na hatua nyingine za adhabu ikiwa ni pamoja na kuwawekea vikwazo walowezi wa Ukingo wa Magharibi, Wizara ya Mambo ya Nje imesema hatua za London "hazitageuza" Jerusalem hatika kujilinda kijeshi.

Uingereza ilisitisha mazungumzo ya biashara huria baada ya Waziri Mkuu Keir Starmer kusema amesikitishwa na kuongezeka kwa harakati za kijeshi huko Gaza.

Lammy aliliambia Bunge: "Hatuwezi kusimama mbele ya hali hii mbaya ya kuzorota. Hatukubaliani na kanuni zinazosimamia uhusiano wetu baina ya nchi mbili."

Aliongeza: "Kusema ukweli, ni dharau kwa maadili ya watu wa Uingereza. Kwa hivyo, leo, natangaza kwamba tumesitisha mazungumzo na serikali hii ya Israeli juu ya makubaliano mapya ya biashara huria."

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jerusalem inajibu hivi: “Mamlaka ya Uingereza ( British-Mandate ) yalimalizika miaka 77 iliyopita kwa hiyo wasituletee Shinikizo halitakengeusha Israeli kutoka katika njia yake katika mapambano ya kuwako kwake na usalama dhidi ya maadui wanaotaka kuiangamiza.

Hatua za Uingereza, ambazo ni pamoja na kumwita balozi wa Israel, Tzipi Hotovely, kuzungumzia vita huko Gaza, zinakuja huku kukiwa na hasira ya kimataifa dhidi ya Israel kuhusu mwenendo wake wakati wa vita dhidi ya kundi la kigaidi la Hamas.

"Serikali ya Israel ina jukumu la kuingilia kati na kusitisha vitendo hivi vya fujo," Lammy anasema. "Kushindwa kwao kuchukua hatua mara kwa mara kunaweka jamii za Wapalestina na suluhisho la serikali mbili hatarini."
Jana, viongozi wa Uingereza, Ufaransa, na Kanada walitishia "vitendo halisi" ikiwa Israeli haitasitisha kampeni yake ya kijeshi na kuondoa vikwazo kwa misaada ya kibinadamu. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema mapema leo kuwa Paris inaunga mkono mapitio ya uhusiano wa kiuchumi kati ya Israel na Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na vita.

"Hata kabla ya tangazo la leo, suala hilo lilikuwa halijaendelezwa hata kidogo na serikali ya sasa ya Uingereza," inasema Wizara ya Mambo ya Nje ya Israeli kuhusu hatua za Uingereza, na kuongeza kuwa makubaliano ya biashara "yana manufaa kwa pande zote" na kama, "kutokana na chuki dhidi ya Israel na masuala ya kisiasa ya ndani, serikali ya Uingereza iko tayari kudhuru uchumi wa Uingereza - huo ni uamuzi wake."

Wizara hiyo pia inavitaja vikwazo kwa walowezi vilivyotangazwa mapema leo kuwa "vya kutatanisha, visivyo na msingi, na vya kusikitisha," ikiashiria mauaji ya wiki iliyopita ya Tzeela Gez na gaidi wa Kipalestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi kama ushahidi wa upuuzi wa vikwazo "wakati ambapo Israeli inaomboleza mwathirika mwingine wa ugaidi wa Palestina."

Gez alikuwa mjamzito na akielekea kwenye chumba cha kujifungulia wakati wa shambulio la risasi, na "madaktari bado wanapigania maisha ya mtoto wake mchanga hospitalini," taarifa hiyo inaongeza.

View attachment 3340224
Naomba nikupe Taarifa maana umelala usijuwe kile kinaendelea kwa Taarifa yako too British shemeji ya Israel na Waziri mkuu wa British kwa sasa ameowa mwanamke myahudi yaani unawagusaje mashemeji kama sio kichekesho na mwisho stama ana vina saba vya wayahudi. Kwaheri
 
Kwa maana hiyo unataka kusema mimi ninadanganya?
 
Myahudi mwenyewe kakubali ila echolima sasa

Yedioth Ahronoth, citing a source in the Israeli Foreign Ministry:

We are facing a real tsunami that will get worse.

@ResistanceLounge

Urgent | Yedioth Ahronoth, citing a source in the Israeli Foreign Ministry: We are in the worst situation we have ever been in, and the world is not with us.

Spain washaanza kukata deals na israel,uk wamesema punches zaidi zitafuata ikiwa israel watakaidi
 
Kuna kila dalili ya wapalestina kupata nchi yao,ilipofika uingereza kuwakana makaburu,anguko la ubaguzi wa rangi afrika kusini lilikua dhahiri..sasa ufaransa, uingereza, Canada.. hispania na ireland wao wameshaitambua palestine,hawa wakulungwa watafuata,ile 'concrete actions' waliyoahidi kwenye tamko la pamoja siyo biashara tu

Uingereza iliwahi kuwakana Makaburu wa SA? Lini hiyo? Wakati Mandela anaachiliwa kutoka gerezani na rais Frederick DE Clack nilikua mtu mzima, hata Frederick anaingia madarakani akimpokea Pieter W. Botha pia nilikua mtu mzima, sina kumbukumbu kama Uingereza ya malkia imewahi ku talk shit against boers to-date, nikukumbushe mwaka huo waliowatelekeza Makaburu?
 
🇪🇸🔫🚫🇮🇱- The Spanish Parliament ratifies the proposal to ban the arms trade with Israel

🇬🇧🔫🚫🇮🇱 - Britain stops arms exports that were scheduled to Israel

🇪🇺⁉️🇮🇱 17 EU countries agreed to review the partnership agreement with Israel, while 9 countries refused.

⚜️@TheSimurgh313
 
Pameanza kuchangamka

— 🇬🇧/🇸🇪/🇮🇱 NEW: The United Kingdom has announced the suspension of free trade agreement negotiations with Israel, along with sanctions on Israeli settler leaders and groups in the West Bank, including Daniella Weiss and 'Neria's Farm'

Additionally, Sweden's Foreign Minister Maria Malmer Stenergard stated that they would 'push for EU sanctions' against individual Israeli ministers.

@Middle_East_Spectator
 
Uingereza iliwahi kuwakana Makaburu wa SA? Lini hiyo? Wakati Mandela anaachiliwa kutoka gerezani na rais Frederick DE Clack nilikua mtu mzima, hata Frederick anaingia madarakani akimpokea Pieter W. Botha pia nilikua mtu mzima, sina kumbukumbu kama Uingereza ya malkia imewahi ku talk shit against boers to-date, nikukumbushe mwaka huo waliowatelekeza Makaburu?
Sasa wakati huo vyombo vya habari ni rtd,mzalendo,uhuru, mfanyakazi, daily news, vyombo vya chama na serikali,ungezipatia wapi hizo habari!?..makaburu walikuja na mpango wa kujifanya kama wamemsahau mandela Ili atoroke alimwe shaba,ni waingereza ndiyo waliotoa taarifa kwa front liners wamwambie mandela mpango mzima...uliiona hiyo habari kwenye mzalendo!?...
 
🇪🇸🔫🚫🇮🇱- The Spanish Parliament ratifies the proposal to ban the arms trade with Israel

🇬🇧🔫🚫🇮🇱 - Britain stops arms exports that were scheduled to Israel

🇪🇺⁉️🇮🇱 17 EU countries agreed to review the partnership agreement with Israel, while 9 countries refused.

⚜️@TheSimurgh313
Kwa akili yako kiduchu hicho ndicho kitazuia kipigo kwa magaidi wa Hamas? Huko hakuwezi kuizuia Israel isijilinde na magaidi hao.

Mapigano yanayoendelea hivi sasa ni Israel kutaka watu wake waliotekwa na magaidi wa Hamas na kama magaidi hao watangewaachia tusingefika hapa tulipo!!!
 
Uongo mtupu Netanyau alishasema hata hamasa akiachia mateka wote haondoki Gaza anataka atawale yeye
 
Uongo mtupu Netanyau alishasema hata hamasa akiachia mateka wote haondoki Gaza anataka atawale yeye
Ni kweli Hamas lazima waondoke hawawezi kuwa na Jirani muuaji!!!!
 
Back
Top Bottom