Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Ukihisi haiko sahihi kumlaza na wanao basi juwa kuwa si sahihi kumlaza na wanao. Siku zote nafsi zetu hutuonya kwa ile hali tunayosema ni wasiwasi na ndio maana waswahili wakasema wasiwasi ni akili.Habar ya leo
Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume ( miaka zaidi ya 30) na alilala chumba Cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"
Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumban.
Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu
WANDUGU
Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani.
Nipo sahihi au inakuwaje?
Kuliko kuja kujuta baadae ondoa hiyo kupe inayojiita shemeji kwako haraka sana. Kama anakwenda na kurudi mjini inamaanisha ana mitikasi ya maana hivyo kumudu kulipia lodge.
Aje hapo kwako adoee msosi akatafute sehemu alale. Jitu la miaka 30 halioni haya kubanana na vitoto, mwisho likojolewe halafu lionekane lenyewe ndio kikojozi.