Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Habar ya leo
Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume ( miaka zaidi ya 30) na alilala chumba Cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"

Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumban.
Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu

WANDUGU
Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani.
Nipo sahihi au inakuwaje?
Ukihisi haiko sahihi kumlaza na wanao basi juwa kuwa si sahihi kumlaza na wanao. Siku zote nafsi zetu hutuonya kwa ile hali tunayosema ni wasiwasi na ndio maana waswahili wakasema wasiwasi ni akili.

Kuliko kuja kujuta baadae ondoa hiyo kupe inayojiita shemeji kwako haraka sana. Kama anakwenda na kurudi mjini inamaanisha ana mitikasi ya maana hivyo kumudu kulipia lodge.

Aje hapo kwako adoee msosi akatafute sehemu alale. Jitu la miaka 30 halioni haya kubanana na vitoto, mwisho likojolewe halafu lionekane lenyewe ndio kikojozi.
 
Habar ya leo
Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume ( miaka zaidi ya 30) na alilala chumba Cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"

Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumban.
Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu

WANDUGU
Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani.
Nipo sahihi au inakuwaje?
Usijaribu kumlaza ndugu yako wa kiume na mwanao, bora umchukue binti yako ukalale nae mwenyewe. Hao maanko ndo wanaharibu watoto iwe wa kiume ama wa kike, mlaze sebuleni ama lodge ya karibu.
 
MREJESHO

Kabla ya kupiga msos niliamua kumueleza wife kuwa "uncle" naenda kumlaza lodge na siwez kumuweka rehani cute girl wangu. Wife alikubali kwa shingo upande.

Fasta nikawacheki wadau wa boda waniangalizie chumba logde za uswazi.

Wakati wa kupiga msosi nikaamua kumchana "uncle" jinsi Dunia ilipofikia na maamuz yangu kwa wakat huo. Jamaa kwanza hakuamin kama nampeleka nje kulala kwa kuwa alijua tayar kafika.

Kiufupi, kalala logde ya kawaida sana (Bei kapuni) tofauti na kitambi kinavyomuonesha.

Nashukuru sana kwa msaada wa mawazo yenu. Linda familia yako bila kujali lawama zotakazo tokea

Dah, afadhali kabisa, hana aibu kabisa, siku nyingine usirudie hilo kosa kubwa namna hiyo, hata kama angekuwa mtoto wa kiume, big no!!
 
ALALE SEBULENI.

TENA CHINI KWENYE MKEKA

UNAANZAJE KUMLAZA MTOTO NA JITU ZIMA LA MIAKA 30

WANAOBAKA NA KULAWITI WATOTO HUWA HAO HAO WATU WA KARIBU

BABA NDIO MLINZI WA WANAO.

KWANZA JITU LA MIAKA 30 LINAENDAJE KULALA KWA MTU ASIYEKUWA NA NAFASI?????

ACHA KULEA UPUUZI

UMENIUDHI ULIPORUHUSU ALALE NA MTOTO
 
Yaani katika mambo ya ajabu ni haya tuna familia Moja hapa kijijini kwetu Walikuwa wanatembelewa na ancle kama hivo hivo so akawa analala chumba Cha mtoto wa kiume ebhanae Leo huyo mtoto ni shoga na anaelezea wa Kwanza kumfanyia hivo ni huyo mjomba
 
Mijitu mingine mingese kweli yan unaenda kwa mtu na unajua hakuna vyumba vya kutosha bado unaenda na mibegi yako unaweka Kambi kabisa upumbavu mtupu
 
Back
Top Bottom