Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Ukihisi haiko sahihi kumlaza na wanao basi juwa kuwa si sahihi kumlaza na wanao. Siku zote nafsi zetu hutuonya kwa ile hali tunayosema ni wasiwasi na ndio maana waswahili wakasema wasiwasi ni akili.

Kuliko kuja kujuta baadae ondoa hiyo kupe inayojiita shemeji kwako haraka sana. Kama anakwenda na kurudi mjini inamaanisha ana mitikasi ya maana hivyo kumudu kulipia lodge.

Aje hapo kwako adoee msosi akatafute sehemu alale. Jitu la miaka 30 halioni haya kubanana na vitoto, mwisho likojolewe halafu lionekane lenyewe ndio kikojozi.
 
Ova my dead body!mwanangu awe wa kike au wa kiume kulalala na mtu wa jinsia me ni big no. ni hatari is your mithilika ,huyo alale sebuleni ,huko lodge utalipa mpaka lini? kama anakaa wiki tatu itakuwaje?
 
Usijaribu kumlaza ndugu yako wa kiume na mwanao, bora umchukue binti yako ukalale nae mwenyewe. Hao maanko ndo wanaharibu watoto iwe wa kiume ama wa kike, mlaze sebuleni ama lodge ya karibu.
 

Dah, afadhali kabisa, hana aibu kabisa, siku nyingine usirudie hilo kosa kubwa namna hiyo, hata kama angekuwa mtoto wa kiume, big no!!
 
ALALE SEBULENI.

TENA CHINI KWENYE MKEKA

UNAANZAJE KUMLAZA MTOTO NA JITU ZIMA LA MIAKA 30

WANAOBAKA NA KULAWITI WATOTO HUWA HAO HAO WATU WA KARIBU

BABA NDIO MLINZI WA WANAO.

KWANZA JITU LA MIAKA 30 LINAENDAJE KULALA KWA MTU ASIYEKUWA NA NAFASI?????

ACHA KULEA UPUUZI

UMENIUDHI ULIPORUHUSU ALALE NA MTOTO
 
Yaani katika mambo ya ajabu ni haya tuna familia Moja hapa kijijini kwetu Walikuwa wanatembelewa na ancle kama hivo hivo so akawa analala chumba Cha mtoto wa kiume ebhanae Leo huyo mtoto ni shoga na anaelezea wa Kwanza kumfanyia hivo ni huyo mjomba
 
Mijitu mingine mingese kweli yan unaenda kwa mtu na unajua hakuna vyumba vya kutosha bado unaenda na mibegi yako unaweka Kambi kabisa upumbavu mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…