Mawazo yenu tafadhali, nakaribia kuacha kazi

Mawazo yenu tafadhali, nakaribia kuacha kazi

Too face

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
223
Reaction score
199
Kwenu wakuu I hope mko salama..

Nianze kwa kusema mi ni mtumishi idara ya elimu halmashauri flani SINGIDA.

SHIDA YANGU KUU NI UHAMISHO kutoka SINGIDA KURUDI DAR WILAYA YOYOTE ILE HATA PEMBEZONI MWA MJI TU!!

Nimejaribu Mara kadhaa kufanya process za uhamisho lakini zinadunda kila nikiandika barua zinafika hatua flani zinakwama kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupotezwa kwa barua masjara,Mara sijui madiwani wamesimamisha uhamisho, Mara ya mwisho nikaambiwa nitafute wakubadilishana naye,

Nimejaribu Mara nyingi kuweka matangazo ya kutafuta watu wa kubadilishana lakini wapi.. hata humu JF Nimejaribu kuweka matangazo yangu since 2016 nimeambulia patupu.

Imefika mahali sasa Sina mood kabisa ya kufanya kazi kwasababu:
familia yangu yote ipo dar akiwemo mume,mzazi,.na watoto ambao imenilazimu kuwaacha huko angali wadogo kutokana na changamoto zinginezo.

Kutokana na kukosa huko kwa morale ya kufanya kazi najikuta nashindwa kufanya kazi kwa ufanisi Hali inayopelekea kuonekana mzembe kazini n.k. hivyo kujikuta napata barua za maonyo mbalimbali na changamoto zingine.

Kwa Hali hiyo Basi NAONA NI BORA NIACHANE KABISA NA KAZI HII nirudi dar japo mzazi na Mume wamenisihi nisiache lakini kwa upande wangu naona kadri siku zinavyoenda mazingira ya kazi yanazidi kuwa magumu kwangu..

NAOMBENI USHAURI WENU tafadhali..
Au Kama Kuna anayeweza kunisaidia kutoka huku NITASHUKURU SANA.

Asante.
 
Kwanini mumeo asije huko uliko? Nani kakwambia maisha ni Dar???. Acha kazi uone ilivo kazi kutafuta kazi? . acha utoto. Elimu haijakukomboa wewe.. Fanya kazi kubari mazingira fanya kazi kwa upendo. Then mpe nafasi Sir God. Hope utapata hiyo nafasi. :But siyo kwa huo utaratibu.
 
Nature ya kazi yake haimruhusu kuja nilipo pia Ni mgonjwa anaclinic Moi.
 
Utakachoambulia huku ni kutapeliwa tu na watu watakaodai kuwa na connection za suala lako.

Sasa hivi una ajira ila huna morale ukiacha kazi ukaenda Dar utakosa vyote.

Unaowafuata Dar kama utakuwa jobless,utaenda kuwakosesha morale ya kuwa karibu na wewe.

Acha kazi ukiwa tu na uhakika wa ku-survive nje ya ajira zaidi ya hapo unaenda kuwa na morale ya kurudi kazini Singida.
 
Sawa.
Asante
 
254A0F21-A713-49BC-B51A-27C1473235CE.jpeg
 
Back
Top Bottom