Kam unaamini unaweza kuwa mjasiriamali na unaweza kuhangaika kweli acha kazi rudi Dar ukakae na familia yako, riziki ipo kote, wapo waliojiajiri na maisha yao yanaenda tu, muhimu fikiria kwanza ni ujasiriamali wa aina gani utakaofanya na uwe na akiba (mtaji wa kutosha) ili hata ikitokea biashara isipoenda vizuri usiyumbe sana kiuchumi.
Muhimu zaidi ni kumpanga mumeo akuelewe, anaonekana mindset yake ameiwekeza sana kwenye kuajiriwa, lakini pia kubwa zaidi, unaweza kuja kutafuta kazi ya kufundisha hata huku Dsm shule binafsi zipo nyingi hasa ukiwa na experience hutachelewa kupata kazi.
Mimi nilikuwa nabishana na mwenzangu hivyo hivyo, alikuwa anafundisha Kahama lakini mazingira ya kule akawa hayataki kabisa, kila nikimwambia asiache kazi anatulia siku mbili nikidhani amenielewa ghafla analipuka tena, anataka kurudi Dar tuwe wote, baadae nikaona isiwe kesi bora arudi aje afanye hata biashara nae alikuwa anapenda ujasiriamali.
Matokeo yake amerudi Dar hajakaa muda mrefu aka apply Zanzibar aliona kuna nafasi za kazi akapata, sasa yuko Znz anaendelea na kazi yake lakini ni private school, akitaka kuja Dsm boti Azam marine 25,000/= safari saa moja na nusu amefika Dar, maisha wakati mwingine ni alternatives tu, unaweza kuogopa kufanya jambo kumbe mbele yako bado kuna riziki yako.