Mawazo yenu tafadhali, nakaribia kuacha kazi

Mawazo yenu tafadhali, nakaribia kuacha kazi

DOGO MIMI DADA YAKO NAKUOMBA USIACHE KAZI

Badala yake tafuta vitu vya kukukeep busy baada ya kazi ili uondoe upweke na kuiwaza sana familia. Narudia tena kukuomba usiache kazi.

Kama unadhani unaweza kufanya ujasiriamali anza kuufanya sasa ukiwa kazini, ukiona imekupendeza na kukulipa; ukaona una uhakika unachokifanya kina msingi wenye maisha marefu na faida kwako ndio uache kazi
Asante mpenzi.
Nilishaanza kidogo kufanya but muda ndo changamoto.

Nashukuru sana kwa MAWAZO yako
 
Fika TAMISEMI DODOMA Mji Wa Serikali Ukiwa Na Copies Za Barua Zako Ambazo Umeshaomba Zamani, Uone Iwapo Zimefika Ama Ziliishia Ulipo
SINGIDA Upo Mbona Ni Pazuri Tu
Chapa Kazi
Mmhh kiufupi zinaishia nilipo.
 
Kwenu wakuu I hope mko salama..

Nianze kwa kusema mi ni mtumishi idara ya elimu halmashauri flani SINGIDA.

SHIDA YANGU KUU NI UHAMISHO kutoka SINGIDA KURUDI DAR WILAYA YOYOTE ILE HATA PEMBEZONI MWA MJI TU!!

Nimejaribu Mara kadhaa kufanya process za uhamisho lakini zinadunda kila nikiandika barua zinafika hatua flani zinakwama kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupotezwa kwa barua masjara,Mara sijui madiwani wamesimamisha uhamisho, Mara ya mwisho nikaambiwa nitafute wakubadilishana naye,

Nimejaribu Mara nyingi kuweka matangazo ya kutafuta watu wa kubadilishana lakini wapi.. hata humu JF Nimejaribu kuweka matangazo yangu since 2016 nimeambulia patupu.

Imefika mahali sasa Sina mood kabisa ya kufanya kazi kwasababu:
familia yangu yote ipo dar akiwemo mume,mzazi,.na watoto ambao imenilazimu kuwaacha huko angali wadogo kutokana na changamoto zinginezo.

Kutokana na kukosa huko kwa morale ya kufanya kazi najikuta nashindwa kufanya kazi kwa ufanisi Hali inayopelekea kuonekana mzembe kazini n.k. hivyo kujikuta napata barua za maonyo mbalimbali na changamoto zingine.

Kwa Hali hiyo Basi NAONA NI BORA NIACHANE KABISA NA KAZI HII nirudi dar japo mzazi na Mume wamenisihi nisiache lakini kwa upande wangu naona kadri siku zinavyoenda mazingira ya kazi yanazidi kuwa magumu kwangu..

NAOMBENI USHAURI WENU tafadhali..
Au Kama Kuna anayeweza kunisaidia kutoka huku NITASHUKURU SANA.

Asante.
hapo cha kwanza siyo lazima kupata dsm kabisa unaweza kupambana ukasogea karibu (moro, pwani-bagamoyo, chalinze, mkuranga) then utaendeleza harakati. (Unapoandika tangazo la kutafuta wa kubadilishana naye ainisha kabisa kuwa utampa muhusika senti ya kusafirisha mizigo mchakato ukikamilika) pia kuwa makini na matapeli

2. Inawezekana unachopitia ni kuboreka na kazi ya aina moja kwa muda mrefu pia. Omba kuingia katika mpango wa masomo, then kasome, ubadili kidogo upepo pia upate mpango mpya wa fikra

3. Tafuta koneksheni (ila kuwa makini sana na wapigaji)

4. Anza kuomba kazi private institutions za dsm ili ukiacha kazi uwe na mahali pa kupata senti AU jichange mtaji kabisa ili ukijilipua uwe na cha kufanya kuingiza chochote
NB: kama ukiamua kuacha usiache kienyeji, soma mkataba wako au stansing order acha kwa utaratibu rasmi
 
Kam unaamini unaweza kuwa mjasiriamali na unaweza kuhangaika kweli acha kazi rudi Dar ukakae na familia yako, riziki ipo kote, wapo waliojiajiri na maisha yao yanaenda tu, muhimu fikiria kwanza ni ujasiriamali wa aina gani utakaofanya na uwe na akiba (mtaji wa kutosha) ili hata ikitokea biashara isipoenda vizuri usiyumbe sana kiuchumi.

Muhimu zaidi ni kumpanga mumeo akuelewe, anaonekana mindset yake ameiwekeza sana kwenye kuajiriwa, lakini pia kubwa zaidi, unaweza kuja kutafuta kazi ya kufundisha hata huku Dsm shule binafsi zipo nyingi hasa ukiwa na experience hutachelewa kupata kazi.

Mimi nilikuwa nabishana na mwenzangu hivyo hivyo, alikuwa anafundisha Kahama lakini mazingira ya kule akawa hayataki kabisa, kila nikimwambia asiache kazi anatulia siku mbili nikidhani amenielewa ghafla analipuka tena, anataka kurudi Dar tuwe wote, baadae nikaona isiwe kesi bora arudi aje afanye hata biashara nae alikuwa anapenda ujasiriamali.

Matokeo yake amerudi Dar hajakaa muda mrefu aka apply Zanzibar aliona kuna nafasi za kazi akapata, sasa yuko Znz anaendelea na kazi yake lakini ni private school, akitaka kuja Dsm boti Azam marine 25,000/= safari saa moja na nusu amefika Dar, maisha wakati mwingine ni alternatives tu, unaweza kuogopa kufanya jambo kumbe mbele yako bado kuna riziki yako.
[emoji24]

Kiukweli ujasiriamali nauweza ,naupenda na Niko tayari kupambana.

Anyway Nashukuru sana kwa USHAURI wako
 
sijajua upo kijijini kiasi gani ila komaa huko huko ukiacha utasota baadae, NB kama issue ni Dar es salaam omba hata mikoa ya Jirani kama Pwani au Tanga ila kama unataka tu Dar utasota sana sogea hata jirani mambo mengine mbele kwa mbele
Mkuu shida comment inakuja "tafuta wa kubadilishana naye"

Nimejaribu namna nyingi mno nimeshindwa mkuu.
 
Uongea na daktari ... jifanye unaumwa , chukua likizo ya ugonjwa hata miezi mi 2 . Nenda huko Dar katulize kichwa ukiwa unafikiria “ if you really need that job” ... ukiona mambo hayaendi rudi kazini , ukiona unaweza endelea kuumwa for the rest of your life.
Sawa.
 
Baba ndie wa kufanya kaz na kuleta chakula ndani..!!!

Kabla ya kuacha kazi jiulize hili:
A) Mshahara wako una effect yeyote katika familia yako,namaanisha kwa mumeo na watoto wako na upande wa ndugu zako je wanakutegemea..? Kama ni ndio hapo kuacha kaz inabidi uwe na plan B ambayo itakua ina uwezo wa kukutengenezea kiasi kile cha mshahara wako ama zaidi kwa kuwa tayar mshahara ushaingia kwenye damu,una mahitaji binafsi huwa unacover pasipo mjulisha ama kumuomba Mr..!!
Otherwise mwanamke anatakiwa awe na familia yake ni kawaida mwanaume akakaa mbali na familia lakini sio mama kwanza aliewaambia wanawake mnatakiwa mfanye kazi nani mbona mnajipa mizigo(western culture)[emoji52] Mama anatakiwa aangalie familia inaendeleaje nyumban..
Sikatai, someni hata mmalize elimu yote but sio lazima kufanya kazi b'ze ajira ni mume wa pili how can you manage..??
Kama mume anaingiza hela kazini au kwenye biashara inatosha mwanamke ukijitahidi saaana anzisha ka kitu kakuingizie pesa but sio kakutinge mpaka ukose muda wa kuangalia familia..
Ndo maana familia za siku hizi kitoto mwaka na nusu kinaenda shule..!!!

My Opinion
Kama utakua una kitu cha kufanya kikuingizie fedha kwa kua ulishazoea kila mwisho wa mwezi kukinga Piga chini hiyo kaz kalee wanao
Lakini kama hutakuanacho bas pima kama kazi ni bora kuliko familia yako au familia ni bora kuliko kazi..!!
Sorry kwa Gazeti[emoji41][emoji41]

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Unaacha kazi ili urudi daslam siyo? Nikajua unaacha kazi kwaajili unabiashara zako zinakulipa na unakosa muda wa kutosha..

Hta hvyo watu wanatofautiana maisha wengine wa kishua acha tu kazi urudi daslam maana itakua umemiss sana KFC
Na burger [emoji488] points, na si unajua vile ice cream [emoji509] ilivyo tamu? Eeeh aacha tu urudi daslam maisha ni rahisi sana
 
[emoji38] mkuu ninahuzuni Ila umenifanya nicheke kwa sauti.
 
Vuta mkopo wa maana hata 20M then sepa zako ukapambane kivingine au chukua ndinga hata IST kila mwisho wa mwezi uko dar.
Nb. Za kuambiwa changanya na zako
Unataka kumuua mtt wa watu ww 😃😃🙃
Yaaan na ist kila wikend dar na kurud
 
Baba ndie wa kufanya kaz na kuleta chakula ndani..!!!

Kabla ya kuacha kazi jiulize hili:
A) Mshahara wako una effect yeyote katika familia yako,namaanisha kwa mumeo na watoto wako na upande wa ndugu zako je wanakutegemea..? Kama ni ndio hapo kuacha kaz inabidi uwe na plan B ambayo itakua ina uwezo wa kukutengenezea kiasi kile cha mshahara wako ama zaidi kwa kuwa tayar mshahara ushaingia kwenye damu,una mahitaji binafsi huwa unacover pasipo mjulisha ama kumuomba Mr..!!
Otherwise mwanamke anatakiwa awe na familia yake ni kawaida mwanaume akakaa mbali na familia lakini sio mama kwanza aliewaambia wanawake mnatakiwa mfanye kazi nani mbona mnajipa mizigo(western culture)[emoji52] Mama anatakiwa aangalie familia inaendeleaje nyumban..
Sikatai, someni hata mmalize elimu yote but sio lazima kufanya kazi b'ze ajira ni mume wa pili how can you manage..??
Kama mume anaingiza hela kazini au kwenye biashara inatosha mwanamke ukijitahidi saaana anzisha ka kitu kakuingizie pesa but sio kakutinge mpaka ukose muda wa kuangalia familia..
Ndo maana familia za siku hizi kitoto mwaka na nusu kinaenda shule..!!!

My Opinion
Kama utakua una kitu cha kufanya kikuingizie fedha kwa kua ulishazoea kila mwisho wa mwezi kukinga Piga chini hiyo kaz kalee wanao
Lakini kama hutakuanacho bas pima kama kazi ni bora kuliko familia yako au familia ni bora kuliko kazi..!!
Sorry kwa Gazeti[emoji41][emoji41]

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Nitafanyia kazi .

Asante .
 
Badili changamoto kuwa fursa. Nunua mazao weka dawa bei ikipanda uza, Huko kuna alizeti tumia ajira kama kinga kopa jiongeze .
 
Back
Top Bottom