Mawazo yenu tafadhali, nakaribia kuacha kazi

Humu wengi wanakushauri ni wafanyakazi uoga umewatawala
Ila japo kama umri wako ushapita 40 endelea na kazi
Sababu kuu umri huo nguvu zishaanza kupungua
Hapo inakubidi akili itumike zaidi
 
Ndo hapa watu wajue maisha ni zaidi ya pesa. Si pesa unapata lakini hauna amani unaona Bora ujikalie zako ukila mihogo Ila amani iwepo moyoni
Binafsi jikaze upate hela hapo ulipo.kopa mkopo benki afu sepa kanunue ng'ombe zako za maziwa Anza kukomaa.usiogope mama.ama ukafungue kibanda Cha urembo ama mpesa ukomae mbona iyo hela utakuwa unajilipa.jaribu kuwaonyesha kuwa imekubaliana na Hali ya huko. Anza kuonyesha upendo fake kabisa.
Baadaye kopa sepa basi.
Si hawakuelewi.
 
Ukiacha KAZI unaenda kufanya nini cha kuzalisha kipato unachokiacha na zaidi yake? Tafakari Sana.
 
Labda upweke unakusumbua au wivu kwa umpendaye yote yanawezekana.kipimo kidogo kwakuwa unapata kiburi na mshahara ulio nao kwa sasa unaona maisha simple tu zingatia ushauri wa Adolfms #39 sasa anzisha kitu ambacho utakiona ukiacha kazi utakifanya,alafu endelea na kazi miezi kama 6 bila kuchukuwa mshahara wako ukiishi kwakutegemea ulichokibuni ukiona umeweza Ku- savaiv jua mtihani umeshinda ila...ilaa..ilaaa...heshimu panapo kupa heshima
 

It's better! My advice, bora utafute shughuli ya kipato, lakini uwe karibu na familia yako.

mama D


DOGO MIMI DADA YAKO NAKUOMBA USIACHE KAZI

Badala yake tafuta vitu vya kukukeep busy baada ya kazi ili uondoe upweke na kuiwaza sana familia. Narudia tena kukuomba usiache kazi.

Kama unadhani unaweza kufanya ujasiriamali anza kuufanya sasa ukiwa kazini, ukiona imekupendeza na kukulipa; ukaona una uhakika unachokifanya kina msingi wenye maisha marefu na faida kwako ndio uache kazi
 
Fika TAMISEMI DODOMA Mji Wa Serikali Ukiwa Na Copies Za Barua Zako Ambazo Umeshaomba Zamani, Uone Iwapo Zimefika Ama Ziliishia Ulipo
SINGIDA Upo Mbona Ni Pazuri Tu
Chapa Kazi
 
Kam unaamini unaweza kuwa mjasiriamali na unaweza kuhangaika kweli acha kazi rudi Dar ukakae na familia yako, riziki ipo kote, wapo waliojiajiri na maisha yao yanaenda tu, muhimu fikiria kwanza ni ujasiriamali wa aina gani utakaofanya na uwe na akiba (mtaji wa kutosha) ili hata ikitokea biashara isipoenda vizuri usiyumbe sana kiuchumi.

Muhimu zaidi ni kumpanga mumeo akuelewe, anaonekana mindset yake ameiwekeza sana kwenye kuajiriwa, lakini pia kubwa zaidi, unaweza kuja kutafuta kazi ya kufundisha hata huku Dsm shule binafsi zipo nyingi hasa ukiwa na experience hutachelewa kupata kazi.

Mimi nilikuwa nabishana na mwenzangu hivyo hivyo, alikuwa anafundisha Kahama lakini mazingira ya kule akawa hayataki kabisa, kila nikimwambia asiache kazi anatulia siku mbili nikidhani amenielewa ghafla analipuka tena, anataka kurudi Dar tuwe wote, baadae nikaona isiwe kesi bora arudi aje afanye hata biashara nae alikuwa anapenda ujasiriamali.

Matokeo yake amerudi Dar hajakaa muda mrefu aka apply Zanzibar aliona kuna nafasi za kazi akapata, sasa yuko Znz anaendelea na kazi yake lakini ni private school, akitaka kuja Dsm boti Azam marine 25,000/= safari saa moja na nusu amefika Dar, maisha wakati mwingine ni alternatives tu, unaweza kuogopa kufanya jambo kumbe mbele yako bado kuna riziki yako.
 
Kunjuwa mkono mkuu..toa rushwa uone kama hupati uhamisho fastaaaa.....yaani ukitoa pesa hata kama ungetaka kuajiriwa nyumbani ulikozaliwa unapata....
 
Endelea kupambana kuomba uamisho halafu kwa Mwanamke tena mwanandoa ni rahisi tatizo unafuatilia kiswahili
 
sijajua upo kijijini kiasi gani ila komaa huko huko ukiacha utasota baadae, NB kama issue ni Dar es salaam omba hata mikoa ya Jirani kama Pwani au Tanga ila kama unataka tu Dar utasota sana sogea hata jirani mambo mengine mbele kwa mbele
 
Vuta mkopo wa maana hata 20M then sepa zako ukapambane kivingine au chukua ndinga hata IST kila mwisho wa mwezi uko dar.
Nb. Za kuambiwa changanya na zako
Mkopo mil 20 kwa mshahara upi wa mwalimu
 
Uongea na daktari ... jifanye unaumwa , chukua likizo ya ugonjwa hata miezi mi 2 . Nenda huko Dar katulize kichwa ukiwa unafikiria “ if you really need that job” ... ukiona mambo hayaendi rudi kazini , ukiona unaweza endelea kuumwa for the rest of your life.
 
Asante
Nashukuru Sana.
 
Humu wengi wanakushauri ni wafanyakazi uoga umewatawala
Ila japo kama umri wako ushapita 40 endelea na kazi
Sababu kuu umri huo nguvu zishaanza kupungua
Hapo inakubidi akili itumike zaidi
Sijafika huko kabisa mkuu wangu.

Asante
 
[emoji24]

Nashukuru Sana mkuu.
Barikiwa.
 
Noted mkuu.

Barikiwa Sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…