Mayele kuondoka Yanga, pengo lake linazibika kiurahisi sana

Mayele kuondoka Yanga, pengo lake linazibika kiurahisi sana

Mchezaji anayechangia 25% ni nguzo muhimu kwa timu. Kama huamini toa % ya mchango wake kutoka 78 pts,utabaki na 50 pts
Meaning team ilicheza down to ten man sio [emoji16][emoji16]
 
Kinachojalisha siyo asilimia kaka,kama ilivoelezewa na mchangiaji mmoja hapa kwenye huu uzi ni kwamba Mayele alifunga magoli yaliyoamua matokeo yawe ya kuchukua point 3 au yale ya mechi za mtoano yaliiwezesha timu yake ya Yanga kusonga,unaweza kumpata striker mwingine akafunga magoli mengi kuliko Mayele lakini yasiibebe timu,mfano ni pale mchezaji anapofunga magoli mengi katika mechi moja halafu anacheza mechi kadhaa bila kufunga.
Wazi, ila malengo makubwa hapa ni kwamba team yetu sio dependent we can do better hata akikosa mchezaji mmoja meaning kila mchezaji kwenye team ana contribution proportional na wenzake.
 
Elewa nilichoandika. Hata kama mchango wake ungekuwa chini ya hizo asilimia. Ila magoli yake yalikuwa yanaamua matokeo. Mechi ambazo timu plan imefeli Mayele alitumia uwezo binafsi kuipa Yanga matokeo.

Mfano, ondoa magoli ya Mayele CAF halafu tathimini Yanga ingeishia hatua gani. Likewise kwenye ligi kuna mechi zaidi ya sita Mayele kafunga goli la ushindi na kupeleka alama 3 jangwani.

Acha kushupaza fuvu. Pengo la Mayele lipo
Vipi, pengo bado lipo?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kumbe hata mpira haujui. Mimi naongelea mchango wake Yanga kufika hatua ya fainali CAF. Pia kuchukua ligi angalia mchango wa kupata points 3 kupitia magoli yake. Acha uzwazwa
Kama Aziz Ki asingefunga kule uarabuni huo mchango wa Mayele ungeuona wapi. Hiyo shida ya kumtegemea mchezaji mmoja ndiyo inazisumbua timu nyingi duniani ikiwemo Simba. Sisi tushatoka huko, kwa sasa ukimkaba Konkoni anakufunga Aziz, ukimkaba Aziz anakufunga Max, ukimkaba Max anakufunga Mzize, ukimkaba Mzize beki inapanda inakufunga huo ndiyo mtaji tulionao Yanga ya Gamondi.
 
Back
Top Bottom