Mayele Kuuzwa Bilioni 3.6 AS Vita Kuchota Milioni 800

Mayele Kuuzwa Bilioni 3.6 AS Vita Kuchota Milioni 800

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Sioni kama katika siku za hivi karibuni kutatokea na mchezaji nchini Tanzania atauzwa kwa kiasi cha zaidi ya Bilioni 3.6 kumzidi Fiston Kalala Mayele.

Yanga SC wameingiza mpunga mrefu zaidi kwa mauzo ya Mayele kuliko thamani ya Mkataba wa msimu mmoja wa Simba na Sandaland.

3,645,000,000 Tanzanian Shilling: Thamani ya Mayele.Link:

Mayele.PNG

Sell-on clause ni kipengele ambacho kinawanufaisha AS Vita katika mauzo hayo. SaSa watavuna Milioni 800 katika mauzo hayo. Wakati huo huo Yanga SC wataingiza Bilioni 2 na Milioni 800.
fedha.PNG
 
Yanga nao kwenye mkataba wao kuwe ni kifungu kitakachowanufaisha iwapo Pyramids itaamua nayo kumwuza
 
Ukisoma vizuri utaelewa mtoa mada hakusoma shule.

Imeeleza kabisa kuwa gharama za Transfer na Malipo ya Mchezaji kwa miaka 3 yatakuwa $1.5mil kwa miaka 3

Ambapo Yanga walikubaliana na AS Vita kuwa watalipwa $800,000

Maana yake AS Vita itapokea pesa nyingi kuliko Yanga.

Hiyo ni tasfiri isiyo rasmi
 
Ukisoma vizuri utaelewa mtoa mada hakusoma shule.

Imeeleza kabisa kuwa gharama za Transfer na Malipo ya Mchezaji kwa miaka 3 yatakuwa $1.5mil kwa miaka 3

Ambapo Yanga walikubaliana na AS Vita kuwa watalipwa $800,000

Maana yake AS Vita itapokea pesa nyingi kuliko Yanga.

Hiyo ni tasfiri isiyo rasmi
Nilikaa kimya nione kama kuna mtu mwingine atalisema hili. Taarifa iliyoletwa na yule puyanga mleta mada haifanani na post aliyoambatanisha.
 
Tafsiri kamili na sahihi ya hiyo post ni hii hapa chini ingawa sina uhakika wa chanzo cha hiyo taarifa iliyoambatanishwa.

Yanga walimpata Mayele kwa pesa ndogo au bure kutoka Vita (au wengine tumekuwa tunasema muda mrefu kwa mkopo halafu tunabezwa), wakawekeana kipengele hicho cha sell-in-clause kwamba ikitokea Mayele ameuzwa, Vita atapata mshiko wake wa kutosha tu kutoka kwenye hayo mauzo. Taarifa hiyo hapo juu haijasema asilimia ngapi kila upande unapata.

Gharama za jumla za mauzo (transfer fee) ni dola 800,000 ambayo ni kama bilioni 1.8.

Hiyo dola 1.5M aliyosema inajumuisha transfer fee (hiyo dola 800,000) na mshahara wa Mayele. Kwa hesabu za haraka, tukichukulia transfer fee ni dola 1M, Mayele anaenda kupata mshahara wa kama dola 14,000 kwa mwezi (ambayo ni kama shilingi milioni 32).

Wengine siyo vilaza humu kama baadhi ya watu wanavyodhani.
 
Back
Top Bottom