Mayele Kuuzwa Bilioni 3.6 AS Vita Kuchota Milioni 800

Mayele Kuuzwa Bilioni 3.6 AS Vita Kuchota Milioni 800

Mashabiki wa Simba kwa WIVU, yaani kila jema linalozungumzia Yanga au mchezaji wa Yangu utaona comment za Makolo zenye VIJIBA ROHONI.
 
Tafsiri kamili na sahihi ya hiyo post ni hii hapa chini ingawa sina uhakika wa chanzo cha hiyo taarifa iliyoambatanishwa.

Yanga walimpata Mayele kwa pesa ndogo au bure kutoka Vita (au wengine tumekuwa tunasema muda mrefu kwa mkopo halafu tunabezwa), wakawekeana kipengele hicho cha sell-in-clause kwamba ikitokea Mayele ameuzwa, Vita atapata mshiko wake wa kutosha tu kutoka kwenye hayo mauzo. Taarifa hiyo hapo juu haijasema asilimia ngapi kila upande unapata.

Gharama za jumla za mauzo (transfer fee) ni dola 800,000 ambayo ni kama bilioni 1.8.

Hiyo dola 1.5M aliyosema inajumuisha transfer fee (hiyo dola 800,000) na mshahara wa Mayele. Kwa hesabu za haraka, tukichukulia transfer fee ni dola 1M, Mayele anaenda kupata mshahara wa kama dola 14,000 kwa mwezi (ambayo ni kama shilingi milioni 32).

Wengine siyo vilaza humu kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Tatizo letu ni ushabiki na kutoelewa vitu.
 
Vigogo wote wa afrika kaskazini wakina raja , wydad , Esperance na zamalek wali muhitaji Mzee wa kutetema
Hakika ana dhamani Kubwa Tshs 3.6 bn !!
Tunamwombea mafanikio
Itoshe kusema jamaa ni mpambanaji sana
 
Sioni kama katika siku za hivi karibuni kutatokea na mchezaji nchini Tanzania atauzwa kwa kiasi cha zaidi ya Bilioni 3.6 kumzidi Fiston Kalala Mayele.

Yanga SC wameingiza mpunga mrefu zaidi kwa mauzo ya Mayele kuliko thamani ya Mkataba wa msimu mmoja wa Simba na Sandaland.

3,645,000,000 Tanzanian Shilling: Thamani ya Mayele.Link:

View attachment 2691018
Sell-on clause ni kipengele ambacho kinawanufaisha AS Vita katika mauzo hayo. SaSa watavuna Milioni 800 katika mauzo hayo. Wakati huo huo Yanga SC wataingiza Bilioni 2 na Milioni 800.
View attachment 2691020
We jamaa nani anakudanganya kipumbavu namna hii?

IMG-20230717-WA0139.jpg
 
Hakuna mchezaji wa bei hiyo, hiyo ni bei ya jikoni yani imepikwa.
Ukiyaambia ukweli yanatukana, hiyo bei ni kwaajili ya kuwapoza tu machungu lakini hamna kitu hapo
 
We jamaa nani anakudanganya kipumbavu namna hii?

View attachment 2691248
Habari zenu za kuokoteza hizi kama ingekuwa hivyo Yanga wasinge mwachia,aondoke kwani angebaki alikuwa na uwezo wa kuingiza zaidi ya hiyo hela.

Hiyo Afrika Transfer page ipo chini ya nani au ina milikiwa na nani.


Najua mmefurahi Mayele kuondoka,kwani alikuwa nawaumiza sana mkikutana nae,ila mmekasirika kusikia Yanga imepiga mpunga mrefu.
 
Watakuwa walikuwa wanamlipa kidogo asee sasa kakataa shilingi ngapi akachukue hiyo 32m
Nawaambiaga siku zote hawa puyanga, kusema uongo zama hizi ni kazi bure, kwa huu utandawazi, muda haupiti unaumbuka.

Kimsingi Yanga wameshindwa kumlipa Mayele mshahara wa milioni 32 kwa mwezi au klabu yake Vita imeona ni wakati sasa wa mavuno halafu yanga ikashindwa bei waliyotaka.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Sioni kama katika siku za hivi karibuni kutatokea na mchezaji nchini Tanzania atauzwa kwa kiasi cha zaidi ya Bilioni 3.6 kumzidi Fiston Kalala Mayele.
Rekodi za manunuzi ya wachezaji, credit huwa zinaenda kwa mnunuzi, wala si mnunuaji au mnunuliwaji. Cha msingi hatakuwapo kwenye kikosi cha Yanga, mengine ni makelele ya vyura 😁
 
Back
Top Bottom