Sina ushabiki maandazi wa hizi timu zenu ila siwezi kumdharau Mayele. Kwa mfumo aliochagua kocha wake Jana, mtu aliyemwangusha ni Fei ambaye alichagua kutoambatana naye. Otherwise yeye alitimiza jukumu lake vema na makosa machache ya kibinadamu. Tuliocheza mpira tunaelewana, wasioelewa usiwalazimishe. Kuna kipindi mashabiki wa Yanga walimponda Kagere nikasema binafsi nisiye na upande nawachuja kwa kutojielewa. Kila striker ana namna inayomtambulisha uawanjani. Kagere halisi hakuwa na mambo mengi ila alijua kukaa mahali sahihi kwa muda sahihi. Yaani alijua kwa mwenendo huu mpira utakuwa mahali fulani baada ya muda Fulani na kweli ikatokea na akascore kilaini. Sasa mpe a dribble kama Mayele utamkosoa kwa sababu siyo kipaji chake. Nafasi 3 alizopata Mayele Kagere angeweza kutumia ugumu uleule kuscore lakini kazi aliyoifanya dhidi ya beki ya Simba kwa Jana ilikuwa nzito. Wanaowsifu Inonga na Onyango hawawasifu kwa sababu ya kumzuia Fei na wengine. Yaani ukisikia mtu anaisifia beki ya Simba kwa Jana anaisifia kwa matukio ya kumdhibiti mtu mmoja tu na mtu huyo ni Fiston Mayele.