mi_mdau
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,170
- 1,708
Hapo uliposema toyota nyingi hazisumbui napinga kidogo....
Toyota zinasumbua kama magari mengine ya Kijapan yanavyosumbua...
Unafuu wa Toyota unaoneka pale ambapo kuna winging wa spea feki za kichina kila kona ya mji/majiji...
Mtu anamiliki mathali Corrolla, anauziwa Wheel bearing elfu 35..
Nadhani kwa kusema Spare za toyota zipo kibao (hata zile kanjanja) itakuwa umejibu tayari kwa upande mmoja. Watanzania wengi hatuna uwezo wa kutumia baadhi ya magari kwa sababu ya upatikanaji wa spare kwa urahisi tena za bei nzuri. Mafundi wazuri wa haya magari mengine na gharama za jumla za kuhudumia ni Tatizo.
Pia kuna kauli huwa naipenda, “hata nikiwa na hela, gari fulani siwezi kununua”. Naipenda kwa sababu kuna gari hata ukiwa na hela fundi mtaonana mara kwa mara tu especially kwa hizi barabara zetu na mazingira ambayo huwezi kuyabadili.
Mfano tu nitachukua Landcruiser VX badala ya range rover wakati wote (hapa nina experience, japo kidogo sana), prado badala ya discovery, Rav 4 (au suzuki Escudo/Vitara, au Subaru Forester) badala ya BMW X3. Na issue hapa itakuwa siyo hela ila ni reliability.
Sent using Jamii Forums mobile app