Mazda kwanini hazipendwi Tanzania ilhali bei yake ipo chini?

Mazda kwanini hazipendwi Tanzania ilhali bei yake ipo chini?

Hapo uliposema toyota nyingi hazisumbui napinga kidogo....
Toyota zinasumbua kama magari mengine ya Kijapan yanavyosumbua...

Unafuu wa Toyota unaoneka pale ambapo kuna winging wa spea feki za kichina kila kona ya mji/majiji...

Mtu anamiliki mathali Corrolla, anauziwa Wheel bearing elfu 35..

Nadhani kwa kusema Spare za toyota zipo kibao (hata zile kanjanja) itakuwa umejibu tayari kwa upande mmoja. Watanzania wengi hatuna uwezo wa kutumia baadhi ya magari kwa sababu ya upatikanaji wa spare kwa urahisi tena za bei nzuri. Mafundi wazuri wa haya magari mengine na gharama za jumla za kuhudumia ni Tatizo.

Pia kuna kauli huwa naipenda, “hata nikiwa na hela, gari fulani siwezi kununua”. Naipenda kwa sababu kuna gari hata ukiwa na hela fundi mtaonana mara kwa mara tu especially kwa hizi barabara zetu na mazingira ambayo huwezi kuyabadili.

Mfano tu nitachukua Landcruiser VX badala ya range rover wakati wote (hapa nina experience, japo kidogo sana), prado badala ya discovery, Rav 4 (au suzuki Escudo/Vitara, au Subaru Forester) badala ya BMW X3. Na issue hapa itakuwa siyo hela ila ni reliability.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nadhani hata mafundi wetu ambao tunao mtaani wamechangia watu kuwa waraibu wa matoyo hawajiongezi kutafuta maarifa ya kutengeneza magari tofauti na Toyota , wengi ni gonga nyundo na wanafanya kazi kwa mazoea hata mashine za kitaalamu kugundua tatizo la gari hawana,mfano unakuta ni sensor tu, ila fundi anakimbilia kufungua gear box,
 
Nadhani kwa kusema Spare za toyota zipo kibao (hata zile kanjanja) itakuwa umejibu tayari kwa upande mmoja. Watanzania wengi hatuna uwezo wa kutumia baadhi ya magari kwa sababu ya upatikanaji wa spare kwa urahisi tena za bei nzuri. Mafundi wazuri wa haya magari mengine na gharama za jumla za kuhudumia ni Tatizo...
Umeeleza vizuri..
Ila mimi niliegemea zaidi kwenye Japanese cars..
The way ulivyoeleza, ni wazi kabisa tunapogusia suala la reliability, nadhan kwa mazingira ya kitanzania na uchumi wetu, ni rahisi zaidi kumiliki most of Japanese cars kulinganisha na European car ambazo zinataka wallet iwe na mabvu nene zaidi ndiyo utafurahia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile kasumba ya kuaminishwa Toyota ndiyo kila kitu inaanza kupotea ndiyo maana sikuhizi utaona Magari tofauti mengi tu.

TATIZO la brand nyingine tofaut na Toyota ni pale utapoamuwa kuuza utapata usumbufu Sana mpaka uliuze Hilo gari.

Kuna brand ya honda crossroad yameanza kuingia Kwa fujo Tanzania ni bonge moja la gari alafu CC za haya Magari ni ndogo Tu yaani Cc 1790 na 1990 View attachment 1419207View attachment 1419206
Hii honda ni gari ya ndoto yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me binafsi nimetokea kuipenda mazda 2 kwan nahisi ata being yake ni nafuuu naomba kujua bei yake paka ikufikia mkononi na niwapi sahihi pa kuliagiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uku kwetu gari ni Toyota.hizo aina zingine za magari kwa haya mazingira yetu kwa sasa ni presha tupu.Vinginevyo ukiyanunua uwe na uhakika wakukaa miji mikubwa tu.
 
Umeeleza vizuri..
Ila mimi niliegemea zaidi kwenye Japanese cars..
The way ulivyoeleza, ni wazi kabisa tunapogusia suala la reliability, nadhan kwa mazingira ya kitanzania na uchumi wetu, ni rahisi zaidi kumiliki most of Japanese cars kulinganisha na European car ambazo zinataka wallet iwe na mabvu nene zaidi ndiyo utafurahia..

Sent using Jamii Forums mobile app
HAta huko nchi zilizoendelea kama Marekani, Canada Au hata Europe ukiuliza gari ambayo ni reliable watakwambia go for Toyota or Honda.
 
DOMINIQUE MAGHUWA ndo unamuona anauzoefu katika kuchambua magari msachi face book Mkuu

mwongo atofautiani Na mchawi
 
Na siku hizi hazichukui muda kufika
Oil filter tu unapaki siku tano hadi wiki moja na pengine hadi mwezi kuisubiri kutoka german , britain au korea nk wakati toyota siku hiyo hiyo spare inafungwa unaendelea na safari na ndio maana kuna kitu inaitwa user friendly.

Kwa tanzania gari ya mjapani ni user friendly kuliko kampuni nyingine , nyie mnao ongelea habari za spare za mitandaon huenda hamna uzoefu mnaleta story za vijiweni yaani plug tu unapaki gari siku tatu hadi wiki na pengine mwezi kuisubiri ifike halafu unaniambia hiyo gari ni user friendly wakati mambo yangu yamesimama siku tatu au wiki kusubiri plug itoke ulaya

kama nipo kishumundu huku spare hadi itoke dar wakati nikiwa na toyota ya kawaida spare hapo hapo nilipo naipata na mambo mengine yanaendelea ,achen story za vijiweni. Tafuta gari inayo cover mazingira uliyopo
 
Oil filter tu unapaki siku tano hadi wiki moja na pengine hadi mwezi kuisubiri kutoka german , britain au korea nk wakati toyota siku hiyo hiyo spare inafungwa unaendelea na safari na ndio maana kuna kitu inaitwa user friendly..
% kubwa ya wanaomiliki European hawana gari moja.

Wanayo hata mawili au matatu.

Moja ipo service nyingine inafanya kazi.

Naongelea kwa wale ninao wafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna thread moja huku nilikutana nayo actually ilikua inahusu mazda rx 8 the main point ambayo niliipata kuhusu ile gari ni aina ya engine ambazo ni Rotary na zinakua zinahitaji a lot of power na other thing ambach binafsi kilinikatisha tamaa ni kwamba Zinakua na limited time according to kilometres run.

so thats means ile engine yake ikifikisha kilometres flan inakufa kabisa unless other wise uwe unaenda kwa mechanic every month ku ongeza maisha ya engine or ujifunge mkanda ubadilishe na kuweka engine mpya ya toyota may be

Me naona sana sana ni kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazda

tusubirie wajuzi
 
% kubwa ya wanaomiliki European hawana gari moja.

Wanayo hata mawili au matatu...
Uko sahihi kabisa sasa mtu ndo unataka kununua gari ya kwanza eti unakimbilia LAMBORGIN au BENZ Hahaaaa lazima uombe poo iseee
 
Oil filter tu unapaki siku tano hadi wiki moja na pengine hadi mwezi kuisubiri kutoka german , britain au korea nk wakati toyota siku hiyo hiyo spare inafungwa unaendelea na safari na ndio maana kuna kitu inaitwa user friendly....
Mawazo ya kimasikini haya,ukiwa huna hela lazima uteseke tu maana unategemea IST moja tu ikibuma ndio basi tena,kwa style hii mlundikano wa IST utakuwa mkubwa sana
 
Mawazo ya kimasikini haya,ukiwa huna hela lazima uteseke tu maana unategemea IST moja tu ikibuma ndio basi tena,kwa style hii mlundikano wa IST utakuwa mkubwa sana

Sio suala la mawazo ya kimaskini. Tunaongelea hata mtu ana milioni 20 hadi 25 hapo anawaza anunue BMW, Benz, au Toyota. Akinunua toyota bado mtamwita maskini? Ukweli ni kwamba suala la kusubiri spare itoke nje ya nchi tena Ulaya ni stress tu hata kama una hari nyingine ya backup


Sent using Jamii Forums mobile app
 
BMW 7 series kwa $1500? Acha kutufunga kamba basi

Hizo gari ni ngumu zaid ya mitoyota lakin kwel spare zake ni ghali lakin nying ni genuine tofaut na mitoyota spare zake fake kila mwaka unafunga.



Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ukinunua spare za mtumba zinadumu mkuu hasa zinazotoka kwenye gari zilizokatwa
 
Back
Top Bottom