Mkuu! Kweli kabisa Wanadam hatuna jema, wasingetangaza tungelalamika wanabifu na marehem au wasanii wa bongo movie, wametangaza yanazuka mapya.
Kweli kati ya Mvua na Jua bora nini...majibu yote yana utata maana ikinyesha mvua mtalalamika mafuriko, likiwaka jua mtasema ukame.
Clouda wamefanya vyema kwani hata akina sie ambao hatukuwepo dar wakati wa msiba huo walau tulifahamishwa nini kilikua kinaendelea na isitoshe umati ule mkubwa wa watu waliohudhuria mazishi ulijitokeza kutokana na vyombo vya habari kuhamasisha na kutoa taarifa kamili.
Big Up Clouds na vyombo vyote vya habari, endeleeni kutujuza matukio yote muhimu yanayo husu Taifa letu maana ndio kazi yenu kutupasha habari, tena vyombo binafsi vimekua vikifanya vyema kuliko chombo chetu cha serikali TBC.