Mazishi ya Kanumba, kamati yapiga hela ndefu

Mazishi ya Kanumba, kamati yapiga hela ndefu

Ahsante kwa kuliona hilo. Binadamu hatukosi neno hata kama ungemfanyia nini bado tu angekulaumu. Kwanza wafiwa ndio walitakiwa kulipia ile coverage, ijuavyo. Tv zinafaidika sana na matangazo sasa siku ile kulikuwa Na matangazo gani?
Mkuu! Kweli kabisa Wanadam hatuna jema, wasingetangaza tungelalamika wanabifu na marehem au wasanii wa bongo movie, wametangaza yanazuka mapya.

Kweli kati ya Mvua na Jua bora nini...majibu yote yana utata maana ikinyesha mvua mtalalamika mafuriko, likiwaka jua mtasema ukame.

Clouda wamefanya vyema kwani hata akina sie ambao hatukuwepo dar wakati wa msiba huo walau tulifahamishwa nini kilikua kinaendelea na isitoshe umati ule mkubwa wa watu waliohudhuria mazishi ulijitokeza kutokana na vyombo vya habari kuhamasisha na kutoa taarifa kamili.

Big Up Clouds na vyombo vyote vya habari, endeleeni kutujuza matukio yote muhimu yanayo husu Taifa letu maana ndio kazi yenu kutupasha habari, tena vyombo binafsi vimekua vikifanya vyema kuliko chombo chetu cha serikali TBC.
 
Lakini tusiwahukumu kamati kwani sikuhizi kila kitu hela,usije ukashangaa ata nguo walizovaa wanakwaya kamati ndiyo imenunua?Mimi nashangaa kwanini mjomba wake SK akuwa mweka hadhina wakati yeye ndiye aliyetaka msiba ukafanyike kwake .
Ndugu ni ndugu 2 ata kama ana kitu ni vizuri tukaishi nao vizuri wkt wote.
 
Kamati ya fedha iliongozwa na Ruge wa Clouds..ukimwona Ruge kajichomeka sehemu ujue watu muda wowote wanalizwa....nakumbuka michango ya mahafa ya kilosa waliochangisha redioni kwao,Kilosa zilifika nguo tu walizochangiwa na wasamalia..mamilioni hayajulikani mpaka kesho kina Ruge waliyapeleka wapi..
 
Lakini tusiwahukumu kamati kwani sikuhizi kila kitu hela,usije ukashangaa ata nguo walizovaa wanakwaya kamati ndiyo imenunua?Mimi nashangaa kwanini mjomba wake SK akuwa mweka hadhina wakati yeye ndiye aliyetaka msiba ukafanyike kwake .
Ndugu ni ndugu 2 ata kama ana kitu ni vizuri tukaishi nao vizuri wkt wote.

mtunza fedha alikuwa Ruge wa clouds.
 
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Ruge kushoto na Shigongo kulia, kweli Kamati yao imechakachua fedha za msiba wa Kanumba?

Asha Baraka na Ubunge na bado anakimbilia pesa za kilio.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MAJINA ya watu mashuhuri nchi hii, Erick James Shigongo na Rugemarila ‘Ruge’ Mutahaba- wote wakiwa ni wadau wa tasniya ya Habari yako hatarini kuingia doa.

Kwa nini? Hiyo inatokana na kuwamo kwao kwenye Kamati ya mazishi ya mwigizaji Steven Charles Kanumba, ambayo imeingia kwenye kashfa ya kuchakachua michango ya msiba.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini leo vimeripoti kuwa, habari kutoka ndani ya familia ya Kanumba, imeituhumu Kamati hiyo kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.

Kamati ya Mazishi ilikuwa inaundwa na Mwenyekiti Gabriel Mtitu, Makamu Mwenyekiti, Jacob Steven ‘JB’, Katibu, William Mtitu na Wajumbe Issa Mussa ‘Cloud’ (Mweka Hazina), Kimosa, Vincent Kigosi ‘Ray’, Single Mtambalike ‘Richie’, Dilesh Solanki, Millenne Happiness Magesse, Adele Kanumba (dada wa marehemu), Hartman Mblinyi, Ruge, Ally Choky, Simon Mwakifamba, Eric Shigongo, Steve Nyerere, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ na Mama Nassor, mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi Kanumba.

Je, ukweli ni upi. Ni matarajio sasa wahusika wataibuka kujibu tuhuma hizi, hasa ikizingatiwa Kamati iliundwa na watu watu wazito kama Eric Shigongo, mmiliki wa Global Publisher, Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media
 
mkuu inawezekana ni matumizi mabaya ya hela,pia msimba mkubwa kama ule nadhani pia matumizi yatakuwa mengi...ila kama kweli kuna hujuma imefanyika basi ubinadam kazi
 
Wala si dawa,maana risiti ziko bwerere tu.Mi nilishangaa pale kamati zilipokuwa zimeshaundwa kabla hata hakujapambazuka.

Ha ha haaaaaaaaaaaa.mdau umetisha,kweli lakini hivi walikua na haraka gani hasa?
 
Kumbe Asha Baraka ni mbunge tunashukuru mkuu kwa taarifa muhimu...katoka jimbo gani mkuu?
 
Laaaa! Kweli hawa magamba wanahitaji utakaso wa damu ya yesu and not otherwise, hiv how comes mtu na utajiri wote kama shigongo then unachakachua michango ya msiba! Kama hii habari ni ya ukweli basi inabidi serikali itangaze maombi ya kufunga na kuomba even kwa mwaka mzima kwani mahali popote walipo watu wa magamba basi ubadhilifu haukosi kwani siku hizi magamba wanaiba fedha hadi na haki za watu kama walivyomfanyia Lema.
"JESUS PLEASE JUST TOUCH THEM MAGAMBAS" amen
 
Mimi nilishangaa jinsi watu hawa walivyoiteka shughuli na kifanya ya bongo movie utadhani Kanumba hakuwa na ndugu au alikuwa brigedier general. Ninavyojua kuna watu huzikwa na taasisi au jumuia zao kama wanajeshi, polisi, mapadre n.k. Huyu Ruge si ndio alikuwa analalamikiwa kuwa kapola studio iliyotolewa na mkulu au siyo yeye? Mtu hana hata single inakuwaje awaingilie na kuwapangia wenye fani yao? Wasi wasi wangu unaanzia hapo. Pia si ndio huyu huyu aliye mchakachua Mh. Joseph Mbilinyi lile deal la maleria no more au? What do you think mpaka hapo? Kwa shigongo sidhani kama anaweza kushiriki deal chafu kama hiyo
 
Back
Top Bottom