Mazoezi ya kuruka kamba ndiyo mazoezi bora kuliko yote

Mazoezi ya kuruka kamba ndiyo mazoezi bora kuliko yote

Mazoezi ya kuruka kuna mambo ya kuzingatia usije kushtua mgongo ukapata kilema cha kumalizia maisha...anyway kwa waliokula chimvi nyingi the best exervise ni kutembea
 
Binafsi naishi tu sifanyi zoezi la aina yeyote ile zaidi ya tatizo dogo la moyo ambalo ninalo toka nikiwa mtoto. Pamoja na kutambua umhuhimu wa mazoezi lakini naonaga kama nikianza mazoezi najitafutia matatizo.
 
Bro mbona unamtoa akili ndugu huyu!!
Alikua anajaribu kutoa elimu pana ya huu mtazamo wa ndugu aliesema kuruka kamba ndio mazoezi best kulinganisha na mengine ndio amejaribu kudadavua mahitaji ya mazoezi kwa mhusika na amekusudia nini.
Huyo jamaa ana aina fulani ya ukosoaji niite ni ya kishamba sana,yeye mara zote huwa hayupo tayari kukubaliana na mawazo ya mwenzake lazima afanye bullying.

Humu wote tupo tunajifunza,usually siyo wote tunaojua kila kitu na siyo wote hatujui kila kitu na hata vile tunavyohisi tunavijua bado wapo wanaovijua zaidi yetu na wao pia wapo wanaowazidi kuvijua so huo ndiyo ukweli na watu timamu wanaelewa hili but wajuaji kama huyo jamaa dizain ni watu wanaodhani wanajua kumbe wanaendeshwa na stress kufikiri kumkera kila mtu kutawapa faraja.
 
Binafsi naishi tu sifanyi zoezi la aina yeyote ile zaidi ya tatizo dogo la moyo ambalo ninalo toka nikiwa mtoto. Pamoja na kutambua umhuhimu wa mazoezi lakini naonaga kama nikianza mazoezi najitafutia matatizo.
Pole sana.
Sio kila zoezi lina mfaa mtu, linaweza kuwa jepesi lakini kwa mtu mwingine linaweza kuwa na tatizo, ni vuzuri kuwaona wataalamu watakusaidia yale ambayo yanakufaa kwa hali yako.
 
Tupe aidia ya kufanya mazoez simpo tu ili kujiweka sawa kiafya ili kupunguza vitamb vya nyama choma na visungura
Ili kupunguza kitambi, mazoezi lazima yaende sambamba na diet.

Mazoezi mengi yanajulikana, ila watu wanashindwa kufanya kutokana na uvivu tu. Lakini cha muhimu kuzingatia ni kufikia kile kiwango kinacho hitajika, na hii inaweza kupimwa kulingana na zoezi lenyewe.

Mfano kutembea, unaeweza kutumbia app mbalimbali zinaweza hesabu step, na kujiwekea lengo lako utembee step ngapi kwa siku. WHO wana suggest 10,000 steps kwa siku kwa mtu mzima.

Au kukimbia unaweza kuhesabu dakika, na kwa siku angalau dakika 30.

Lakini kwakuwa unataka urahisi nikushauri ufanye zoezi la kutembea, na hakikisha unavuka step 10,000 kwa siku jaribu kufikia steps 12,000, najua sio rahisi lakini inawezekana.(lakini kama huna tatizo la kiafya)

Lakini kumbuka kuzingatia usalama wako pindi ukitembea.
 
Mazoezi ni dhana pana sana, zipo aina nyingi za mazoezi na kila zoezi lina lengo lake.

Hilo unalolisema linaitwa skipping na lina angukia kwenye kundi la aerobic exercises, hivyo lina faida na hasara zake.

Lakini huwezi kusema hilo zoezi ni bora, kwasababu kila zoezi lina lengo lake, leo hii mwakinyo afanye zoezi hilo kwa ajili ya shughuli zake itakuwa si sahihi, lazima atafute muscle power na sio kwa kuruka kamba.

Pia kuna mazoezi tiba kwa ajili ya wagonjwa, huwezi kumrukisha kamba mgonjwa aliye serious lazima akufie, hivyo huwezi Kusema hilo zoezi ni bora kuliko yote.

Kwahiyo zoezi bora ni lile lenye lengo maalumu na lenye kukidhi mahitaji kutokana na uhitaji.
Excited
 
Ili kupunguza kitambi, mazoezi lazima yaende sambamba na diet.

Mazoezi mengi yanajulikana, ila watu wanashindwa kufanya kutokana na uvivu tu. Lakini cha muhimu kuzingatia ni kufikia kile kiwango kinacho hitajika, na hii inaweza kupimwa kulingana na zoezi lenyewe.

Mfano kutembea, unaeweza kutumbia app mbalimbali zinaweza hesabu step, na kujiwekea lengo lako utembee step ngapi kwa siku. WHO wana suggest 10,000 steps kwa siku kwa mtu mzima.

Au kukimbia unaweza kuhesabu dakika, na kwa siku angalau dakika 30.

Lakini kwakuwa unataka urahisi nikushauri ufanye zoezi la kutembea, na hakikisha unavuka step 10,000 kwa siku jaribu kufikia steps 12,000, najua sio rahisi lakini inawezekana.(lakini kama huna tatizo la kiafya)

Lakini kumbuka kuzingatia usalama wako pindi ukitembea.
Step10000 Kwa hatua za mtu mzima sawa na km ngap???

Jina la app inayoweza hesabu hatua tafadhal
 
Kukimbia ndio bora kuliko yote. Sababu unaushughulisha mwili wako wote na sababu ni mazoezi ya umbali mrefu inaondoa stress na uchovu wa akili. Kimbia siku 5 za wiki dak 30 - 60, kunywa kwa uwiano sahihi lita zisizopungua tatu, punguza wanga(kama kazi zako sio ngumu), achana na sukari ya viwandani, tumia sukali ya asili kama asali kwa kiasi, pombe kiasi mls 500 beer au mls 200 pombe kali, isizidi mara tatu kwa wiki tumia maji ya limao, lala masaa 7 hadi 8 usiku, usilale mchana. Kitambi kikiwepo basi huo ni ugonjwa wa kuvimba tumbo.
 
Katika suala mazoezi yapi ni Bora kuliko mengine ..Mimi kama mwanamazoezi nashauri fanya zoezi unaloweza Kwa mwili wako kulimudu,muda ulionao kufanya mazoezi , location Yako na mazingira Kwa ujumla na malengo yako.
Kwa mtu asiyefanya mazoezi siamini kama anakuwa busy na kukosa hata 30 min Kwa siku na kushindwa kuruka kamba au mazoezi ya viungo mepesi nyumbani.
 
Nilimsikia trainer mmoja anaitwa Denzel Alishauri namna bora ya kuruka kamba kwa style tofauti tofauti maana ukiruka kwa style moja ya miguu yote umeonyoka ni hatari kwenye kutingisha moyo ,akasema ukichanganya style ya kuruka it's safe.
Moyo haushtuki kwa mtindo huo. Kama unashida ya moyo kama Angina, BP nk haushauriwi kuanza mazoezi yoyote bila ushauri wa mtaalamu. Unaweza kuufanyisha kazi ambayo haiiwezi na mwisho kuingia matatani
 
Back
Top Bottom