A
Anonymous
Guest
Mkazi wa Kitongoji cha Nyamaitagi, Kata ya Majimoto, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, amepatwa na taharuki baada ya risasi ya bunduki iliyopigwa na wanajeshi waliokuwa wakifanya mazoezi kutoboa paa la nyumba yake na kuingia ndani.
Tukio hilo lilitokea Agosti 20, 2026. Kwa bahati nzuri, hakuna mtu aliyekuwa ndani ya nyumba wakati risasi hiyo ilipoingia.
Mazoezi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi. Hata hivyo, wakazi wa Nyamaitagi wanaeleza kuwa mazoezi hayo yamekuwa yakisababisha hofu na taharuki, hasa kutokana na milio ya risasi na mabomu.
Wakazi wanaomba mamlaka husika kuchukua hatua kuhakikisha usalama wao unazingatiwa wakati wa mazoezi hayo. Pia, wanaomba mazoezi yafanyike katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli hizo badala ya maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi kwa kilimo na ufugaji.
Aidha, wanaomba wakazi wa maeneo yanayozunguka kambi au maeneo ya mazoezi wapewe taarifa mapema kabla ya mazoezi kufanyika, ili waweze kuchukua tahadhari na kuondoa taharuki miongoni mwao.