Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kituko cha kwanza mazungumzo yanafanyika pasipo wahusika wakuu Ukraine kuwepo katika hayo mazungumzo! Yani ni sawa na umemkamata mgoni anamtafuna mke wako ukazua ugomvi halafu wapatanishi wanakuja wanamchukua mgoni wako wanaenda kukaa naye kikao peke yao wanamuuliza anataka nini kumaliza kesi huku wakiwa hawataki kusikia chochote unachosema!
Kituko kingine ni hiki cha kusema uchaguzi mkuu huru na haki ufanyike Ukraine kama sehemu ya mpango wa amani. Anayepatanisha Saudi Arabia hana hata msamiati wa uchaguzi kwenye kamusi yake, Urusi yenyewe imetawaliwa na mtu mmoja kwa miaka 25 iliyopita wakati Ukraine imebadilisha marais mara tano.
Huu ni wendawazimu!