Mazungumzo ya Ndg. Polepole leo 31 Agosti 2025 na umma

Asubuhi nimemwambia huyo Mwandishi ni bomu kabisa. Anatumia google kujibu hoja wakati ana simu na Anaweza kupata facts kutoka source? Si angeenda tu hata ubalozi wa Cuba kuuliza?

Tuna Waandishi wa habari vilaza kabisa.
Hii ndio reflection ya waandishi ambao tunawategemea katika kupata maarifa...sasa ona jinsi Ndugu Polepole alivyomvua 'msuli' mbele ya wakweze!
 
Toa facts mbadala ili waTanzania tupate Elimu.
Umekimbilia kum attack badala ya kutoa facts zako!
 
Write your reply...daa inasikitisha hii bandari ya kwara aliaanza jenga jpm pia huyu polepole anasema tanzania tunayo gas ya lpg? Aisee huu uongo umekithiri
 
Pole pole namwelewa sana ila issue ya gesi Bora asingeijibu kwasababu alishazingua Cuba serikali inatoa kitu kama ruzuku kwenye gesi na mitungi inayopatikana ni 10kg hakuna 20kg ukitaka zaidi ya 10kg ununue kwa magendo (black market) ambayo ni kweli inapatikana ila bei yake ni zaidi ya 100k tsh na ukikamatwa nayo una kesi ya kujibu maana Bado wapo kwenye uchumi wa kijamaa. Hii ya gesi Bora angekaa kimya itamharibia otherwise👍
 
Narudia, hakuna kazi rahisi kama kuwakamata akili nyumbu. We wazuge tu kuwa unamchukia Samia, humpendi jk basi. Utakula tone tone Hadi ushangae.
 
Hivi hii LAANA ya watu weusi alitupa nani!?
Maana jamaa anatufumbua hapa, lakini bado kuna kennge zinasapoti hayo mafisadi.
Ni nini Africa!??
 
Fungua kesi mkuu, sio kukaa kimya na ulitakiwa kutoka nje kupiga kelele mpaka akamatwe mwizi wa mali za taifa ila bado hujachelewa.Kuna jamaa alimuuliza hakimu hivi wewe hakimu unanihukumu kwenda jera miaka yote hiyo kwani wewe hujawahi kukosea? Na wewe hauna tofauti na huyo jamaa.
 
Kumbe hujamwelewa Polepole. Kwanza yeye kaongelea gas kwenye mfumo wa ruzuku ya serikali. Ni gas ambayo serikali hu subsidize ili kupunguza makali ya bei. Ni sawa na Tanzania tunavyofanya kwenye mbolea.

Pili katumia mtungi wa kilo 20 for comparison reasons. Anataka kulinganisha na mtungi wa kilo 15 wa Tanzania. Lakini melezo yake katumia mtungi wa kilo 10 na baadaye kazidisha mara mbili.
 
Campaign nzima ya clean energy ni utapeli mtupu wa kuzidi kuwanyonya kabisa. Tofauti ya wanamtandao na wakoloni ni rangi ya ngozi tu.
 
... unapoamua kupokea ukweli usichague muhabarishaji!
 
Vp kama kakupiga fix au yeye kapigwa fix?
sijaelewa, nani alimpiga fix nani?

kama ni bei ya gesi Cuba, wewe nenda tu chatgpt utapata taarifa zote.

Ikiwa huna hiyo app hebu jaribu kudownload ni bure.
 
nimeandika Cuba sijasema ulimwengu mzima, hebu nenda ukaulize kuhusu Cuba utapata taarifa kibao mbona unaogopa kuuliza?
haya kamuulize huyo chatgpt wako ,habari za Korea kaskazini kama utapata! Sio kila kitu chatgpt imejifunza tayari! Hasa hizi nchi za kijamaa, taarifa zao sio nyingi kwenye archives za mitandaoni!
 
sijaelewa, nani alimpiga fix nani?

kama ni bei ya gesi Cuba, wewe nenda tu chatgpt utapata taarifa zote.

Ikiwa huna hiyo app hebu jaribu kudownload ni bure.
Yeye anapewa taarifa na binadamu kama wewe,so anaweza pia kupewa taarifa za uongo
 
Yeye anapewa taarifa na binadamu kama wewe,so anaweza pia kupewa taarifa za uongo
Kweli kabisa lakini yeye anaitumia kama basis of his argument. Pia amezungumzia ration cards wanazopewa waCuba kila miezi 3, sijui anataka turudie ule ukomunist wa enzi za Nyerere na Karume?

Wenzake tulishapitia huko tukiziita kadi za ukoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…