Mazungumzo ya Ndg. Polepole leo 31 Agosti 2025 na umma

Kumbe hujamwelewa Polepole. Kwanza yeye kaongelea gas kwenye mfumo wa ruzuku ya serikali. Ni gas ambayo serikali hu subsidize ili kupunguza makali ya bei. Ni sawa na Tanzania tunavyofanya kwenye mbolea.

Pili katumia mtungi wa kilo 20 for comparison reasons. Anataka kulinganisha na mtungi wa kilo 15 wa Tanzania. Lakini melezo yake katumia mtungi wa kilo 10 na baadaye kazidisha mara mbili.
Mpaka mwaka Jana march 10kg ilikua 225CUP (cuban peso) ndo bei rasmi yenye ruzuku sasa change hiyo ndo utanielewa nachomaanisha ni almost ka 23k+ huko
 
Asubuhi nimemwambia huyo Mwandishi ni bomu kabisa. Anatumia google kujibu hoja wakati ana simu na Anaweza kupata facts kutoka source? Si angeenda tu hata ubalozi wa Cuba kuuliza?

Tuna Waandishi wa habari vilaza kabisa.
Mwandishi mwenyewe kanenepeana mashavu hovyo utafikiri anapuliza jiko la kuni, unategemea atakuwa na akili za kwenda kuuliza ubalozini ?
 
Chatgpt bado haina taarifa zote ulimwengu mzima!
Ina taarifa zote Mkuu, inaweza isiwe na accuracy ya 100% lakini ina taarifa nyingi sahihi... alichokisema kamwaga kuhusu black market ya gas mbona hata polepole kakirudia ambako bei ni kubwa sana? Na black market ndio inatoa uhalisia wa bei ambapo Chat GPT imeinarate vizuri kabisa... otherwise mazingira fulani machache anayoyasema Polepole yana subsidy kwa kiwango kikubwa na kwa kuwa CUBA ni nchi ya kijamaa... kamwaga alikuwa sahihi sana.. sema polepole anachota sana watu... anapambana na Rostam lakini ni watu wnagapi wanatumia Taifa gas??? Kwani gas nyingi si inatumika ya Oryx? lake? miham,Manjis??? Na hizi zilianza??? Kwanini attack zote ni kwa Rostam... watanzania hatufatilii vitu between the lines... watu kama kina polepole wanaonekana smart of which they are not....
 
1. Ndugu H. Polepole leo ameanza kuelezea bei ya mtungi wa gesi wa Kilo 20 Cuba ambayo ni 2000/= TZS na kusisitiza hapa Tanzania tunapigwa na Mafisadi, huku Gesi tunayo lakini mtungi ni 60,000/= TZS. Amefanya hivyo kwa kujibu hoja za Bwana Ezekiel Kimwaga aliyemkejeli Ndugu Polepole na kusema muongo kuhusu bei halisia ya mitungi ya gesi Cuba kupitia Press yake aliyoifanya tarehe 29-08-2025.

2. Pia amelezea kuhusu Jiografia ya nchi ya Cuba, kwa kutaja Miji mikubwa, Miji ya Utalii, Miji ya Kihistoria, Balozi na maeneo nyeti ya nchi ya Cuba na huku akifafanua kwa undani kuonyesha Nchi ya Cuba anaielewa kiundani zaidi. Huku akihitaja miji kama Matanzas, Havana (La Habana), Santa Clara, Bayamo, Cienfuegos, Santiago de Cuba, Camagüey, Guantánamo na mingineyo.

3. Pia amegusia kuwa Cuba ni nchi yenye uchumi wa kijamaa (socialist economy) na ndio nchi iliyowekewa vikwazo vigumu na Nchi ya Marekani. Lakini nchi ya Cuba ndiyo rafiki mkubwa wa nchi za Afrika kutoka ukanda wa Western Hemisphere -- akisisitiza Ndugu Polepole.

4. Pia amesisitiza na kupinga vikali swala la Raisi Samia Suluhu Hassan kugombea tena awamu hii, huku akisema hakutakiwa kugombea. Huku akisema Samia akipata Uraisi hata waheshimu na kuwasikiliza raia wake.

5. Amesema Mama samia analazimisha uongozi na kwenye kampeni alipaswa kuwasema akina Salim Mwalimu ambao ndio anagombea nao, sio kuwasema Chadema ambao hawapo kwenye uchaguzi amewapiga pini na kusema wameweka mpira kwapani.

6. Amesema Tanzania ina viongozi wabaya ambao hawaelewi maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

7. Pia amegusua ujenzi wa bandari kavu ya Kwala --- huku akisema tumesha chelewa ilitakiwa iwepo miaka 5 nyuma. Huku akisema Bandari kavu inatakiwa iwepo Morogoro na Dodoma, ilikupunguza msongamano wa Malori barabarani na kuongeza mzunguko wa mapato nchini.

Next Press -->Jumatano, Saa 3:00 Usiku -----> Kaa tayari.

"Ukombozi huanza akilini"

Link Below

View: https://www.youtube.com/watch?v=Uz_tHuV_lbc​

Wa kilo 10 siyo wa kilo 20, tafadhali msikilize tena
 
Alafu Kuna kitu lazma tukielewe hivi hyo huo mtungi wa gesi umetengenezwa shilingi ngapi mpaka ukajazwa na kuuzwa shilingi 2,000?
Sahihi kabisa; mtu hajiulizi kama kuna subsidy tena kubwa... maana yake serikali inanunua hiyo gharama nyingine??? Ama kuna watu wanataka tuishi kijamaa... wakumbuke polepole ni mjamaa na matajiri wote ni wezi tu kwake...
 
Polepole sio kichaa otherwise tuambie kama ni kichaa!
Polepole ana vitu anavifungua kwa Taifa la Tz, tumsikilize na kutafakari kwa KINA.
Nahisi "Novena" zimeanza kujibu.
 
Ina taarifa zote Mkuu, inaweza isiwe na accuracy ya 100% lakini ina taarifa nyingi sahihi... alichokisema kamwaga kuhusu black market ya gas mbona hata polepole kakirudia ambako bei ni kubwa sana? Na black market ndio inatoa uhalisia wa bei ambapo Chat GPT imeinarate vizuri kabisa... otherwise mazingira fulani machache anayoyasema Polepole yana subsidy kwa kiwango kikubwa na kwa kuwa CUBA ni nchi ya kijamaa... kamwaga alikuwa sahihi sana.. sema polepole anachota sana watu... anapambana na Rostam lakini ni watu wnagapi wanatumia Taifa gas??? Kwani gas nyingi si inatumika ya Oryx? lake? miham,Manjis??? Na hizi zilianza??? Kwanini attack zote ni kwa Rostam... watanzania hatufatilii vitu between the lines... watu kama kina polepole wanaonekana smart of which they are not....
Smart labda utakua wewe ambae hujui mihani gas ndio hiyo hiyo taifa gas ya ROSTAM! Kama hujui biashara huwezi kuelewa kazi ya marketing ambayo serikali imemfanyia ROSTAM imemfanya ROSTAM kuwa mfanyabiashara mwenye wateja wengi kuliko msambazi mwingine hivyo anakua mnufaika namba 1 wa biashara ya gas nchini! Halafu nyie mnaojionaga mko smart mbona hatujawahi wasikia mkitatua changamoto za nchi kwa kutumia usmasrt wenu, ila tunakutana huku kwenye reply mkijibizana hoja za kina POLEPOLE?
 
Sahihi kabisa; mtu hajiulizi kama kuna subsidy tena kubwa... maana yake serikali inanunua hiyo gharama nyingine??? Ama kuna watu wanataka tuishi kijamaa... wakumbuke polepole ni mjamaa na matajiri wote ni wezi tu kwake...
Unaonekana kama kwako ujamaa ni ushetani.

Hivi kuwalipa mafao hao wenza wa mnaoita viongozi pasipo kufanya kazi yoyote, au haya mafao mnayowalipa wabunge na serikali ku-subsdize hiyo gesi, ni kipi chenye manufaa kwa wananchi!
 
Smart labda utakua wewe ambae hujui mihani gas ndio hiyo hiyo taifa gas ya ROSTAM! Kama hujui biashara huwezi kuelewa kazi ya marketing ambayo serikali imemfanyia ROSTAM imemfanya ROSTAM kuwa mfanyabiashara mwenye wateja wengi kuliko msambazi mwingine hivyo anakua mnufaika namba 1 wa biashara ya gas nchini! Halafu nyie mnaojionaga mko smart mbona hatujawahi wasikia mkitatua changamoto za nchi kwa kutumia usmasrt wenu, ila tunakutana huku kwenye reply mkijibizana hoja za kina POLEPOLE?
Sasa kama Rostam anatatua changamoto za kupikia kuni hauoni kuwa yeye ni smart kuliko pepole anayepiga maneno... my bad sikuelewa kama Mihan ndio Taifa gas - lakini Taifa gas/ Rostam sio mwenye largest market share ya gas; fanya research yako vizuri.... katika hili Polepole hana hoja... mlinganisho bora wa kuanza nao ni east africa then Africa sio unachukua a socialist economy iliyoko huko mbaaaaali kulinganisha na market dynamics za East Africa... ufananinisho usiofaa...
 
Unaonekana kama kwako ujamaa ni ushetani.

Hivi kuwalipa mafao hao wenza wa mnaoita viongozi pasipo kufanya kazi yoyote, au haya mafao mnayowalipa wabunge na serikali ku-subsdize hiyo gesi, ni kipi chenye manufaa kwa wananchi!
Ndio Ujamaa ni ushetani na ndio huo umetufiiisha hapa kwenye hiyo mifano ya mafao ya wenza... tunatakiwa tuondoke kwenye ujamaa Mkuu; Ujamaa ni wachache wafanye kazi halafu wale wote... hiyo hapana aisee
 
Sasa kama Rostam anatatua changamoto za kupikia kuni hauoni kuwa yeye ni smart kuliko pepole anayepiga maneno... my bad sikuelewa kama Mihan ndio Taifa gas - lakini Taifa gas/ Rostam sio mwenye largest market share ya gas; fanya research yako vizuri.... katika hili Polepole hana hoja... mlinganisho bora wa kuanza nao ni east africa then Africa sio unachukua a socialist economy iliyoko huko mbaaaaali kulinganisha na market dynamics za East Africa... ufananinisho usiofaa...
ROSTAM alitumia rafu kujitangaza sokoni akitumia viongozi wa serikali! Kama haufuatilii haya mambo, ROSTAM hata soko la gesi nchini kenya kapigiwa kelele kutaka kuua wasambazaji wengine waliokuwepo awali! Jielimishe kuhusu namna soko huria wanavoli manipulate kina ROSTAM kwa hila!
 
1. Ndugu H. Polepole leo ameanza kuelezea bei ya mtungi wa gesi wa Kilo 20 Cuba ambayo ni 2000/= TZS na kusisitiza hapa Tanzania tunapigwa na Mafisadi, huku Gesi tunayo lakini mtungi ni 60,000/= TZS. Amefanya hivyo kwa kujibu hoja za Bwana Ezekiel Kimwaga aliyemkejeli Ndugu Polepole na kusema muongo kuhusu bei halisia ya mitungi ya gesi Cuba kupitia Press yake aliyoifanya tarehe 29-08-2025.

2. Pia amelezea kuhusu Jiografia ya nchi ya Cuba, kwa kutaja Miji mikubwa, Miji ya Utalii, Miji ya Kihistoria, Balozi na maeneo nyeti ya nchi ya Cuba na huku akifafanua kwa undani kuonyesha Nchi ya Cuba anaielewa kiundani zaidi. Huku akihitaja miji kama Matanzas, Havana (La Habana), Santa Clara, Bayamo, Cienfuegos, Santiago de Cuba, Camagüey, Guantánamo na mingineyo.

3. Pia amegusia kuwa Cuba ni nchi yenye uchumi wa kijamaa (socialist economy) na ndio nchi iliyowekewa vikwazo vigumu na Nchi ya Marekani. Lakini nchi ya Cuba ndiyo rafiki mkubwa wa nchi za Afrika kutoka ukanda wa Western Hemisphere -- akisisitiza Ndugu Polepole.

4. Pia amesisitiza na kupinga vikali swala la Raisi Samia Suluhu Hassan kugombea tena awamu hii, huku akisema hakutakiwa kugombea. Huku akisema Samia akipata Uraisi hata waheshimu na kuwasikiliza raia wake.

5. Amesema Mama samia analazimisha uongozi na kwenye kampeni alipaswa kuwasema akina Salim Mwalimu ambao ndio anagombea nao, sio kuwasema Chadema ambao hawapo kwenye uchaguzi amewapiga pini na kusema wameweka mpira kwapani.

6. Amesema Tanzania ina viongozi wabaya ambao hawaelewi maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

7. Pia amegusua ujenzi wa bandari kavu ya Kwala --- huku akisema tumesha chelewa ilitakiwa iwepo miaka 5 nyuma. Huku akisema Bandari kavu inatakiwa iwepo Morogoro na Dodoma, ilikupunguza msongamano wa Malori barabarani na kuongeza mzunguko wa mapato nchini.

Next Press -->Jumatano, Saa 3:00 Usiku -----> Kaa tayari.

"Ukombozi huanza akilini"

Link Below

View: https://www.youtube.com/watch?v=Uz_tHuV_lbc​

ccm haina mgombea madhubuti hata kidogo. Mtu mwenyewe inaonekana sio muomini wa itikadi wa chama cha mapinduzi na sio mwanamapinduzi. Ni mwanaharakai aliyekua akifadhiliwa na wazungu wa magharibi hatimae kumshawishi aingie kwenye siasa. Kwa kauli yake mwanzo hakujua hata aingie upande gani wa siasa. Upinzani au chama tawala. ina maana hakua muomini wa ujamaa itikadi kwa nadharia imebakia ya CCM. Kwenye kampeni hadi sasa hakemei ufisadi wala uzembe.
 
ROSTAM alitumia rafu kujitangaza sokoni akitumia viongozi wa serikali! Kama haufuatilii haya mambo, ROSTAM hata soko la gesi nchini kenya kapigiwa kelele kutaka kuua wasambazaji wengine waliokuwepo awali! Jielimishe kuhusu namna soko huria wanavoli manipulate kina ROSTAM kwa hila!
Acha wivu mkuu; kila kitu sokoni kwenye uchumi kiko controlled na kuna manipulations kibao - ni jambo la kawaida kiuchumi..kabla hujamlaunu Rostam ushawahi kujiuliza ni nani anayevontroll soko la vigae Tanzania na Easr Africa nzima? Je soko la float glass?? Tena hii ni East, Central, Sadc na sasa hadi North??? Viwanda hivyo vikonTanzani.. je aoko la mabati? Wako watatu tu, ninaweza kutaja vitu kibao... je bakhresa anacontrol nini na nini? Kwa kuwa yeye hapogiwi kelele tu lakini kuna vingi alivyoshikilia na ana manipulate, vipi kuhusu Sukari?? Na kwenyewe Rostam yupo?? Acha kuingizwa kwenye vita kati ya polepole na Rostamu Mkuu, wahenga wanasema usinunue ugomvi. Biashara ya soko huria is all about controll and manipulation ndio maana dhahabu dunia nzima iko controlled na kampuni chvhe sana, mafuta yko controlled na kampuni chache sana na wanaamua lini wapandiahe bei na wapandishaje... tutafute hela tu Mkuu
 
Ina taarifa zote Mkuu, inaweza isiwe na accuracy ya 100% lakini ina taarifa nyingi sahihi... alichokisema kamwaga kuhusu black market ya gas mbona hata polepole kakirudia ambako bei ni kubwa sana? Na black market ndio inatoa uhalisia wa bei ambapo Chat GPT imeinarate vizuri kabisa... otherwise mazingira fulani machache anayoyasema Polepole yana subsidy kwa kiwango kikubwa na kwa kuwa CUBA ni nchi ya kijamaa... kamwaga alikuwa sahihi sana.. sema polepole anachota sana watu... anapambana na Rostam lakini ni watu wnagapi wanatumia Taifa gas??? Kwani gas nyingi si inatumika ya Oryx? lake? miham,Manjis??? Na hizi zilianza??? Kwanini attack zote ni kwa Rostam... watanzania hatufatilii vitu between the lines... watu kama kina polepole wanaonekana smart of which they are not....

Tumejifunza kutokuwa wadadisi bali tumeamua kuwa oyaoya na kumeza kila uongo.

Kuna mahala umeongea point kubwa sana sijui kwanini watu hawaizingatii.
Kwenye market Kuna Oryxy gas, camel, manjis, mihan na taifa wote Bei zao ni zilezile hazina tofauti yeyote.

Mbaya zaidi hao wengine ukiondoa Taifa wapo kwenye soko siku nyingi kabla ya Taifa gas, Taifa gas imezinduliwa awamu ya tano ilihali hao wengine walikuwepo huko nyuma.

Au labda Bei gas imepanda pale tu Taifa gas ilipoanza kuuza gas?

ndani ya mitaa ya Hodeidah Yemen
 
hakuna mtungi wa gesi wa chini ya dola moja huko Cuba, nimeulizia chatgpt ikanipa figure moja kubwa kidogo
Amesema taarifa nyengine huwezi kuzipata kwenye platform au hizo source

Yeye ameishi Cuba na kwa hadhi yake ya kibalozi alipata taarifa nyingi

Hili nalo mnataka kubishana nae?

Amesema jumatano ni balaa!!
 
Tumejifunza kutokuwa wadadisi bali tumeamua kuwa oyaoya na kumeza kila uongo.

Kuna mahala umeongea point kubwa sana sijui kwanini watu hawaizingatii.
Kwenye market Kuna Oryxy gas, camel, manjis, mihan na taifa wote Bei zao ni zilezile hazina tofauti yeyote.

Mbaya zaidi hao wengine ukiondoa Taifa wapo kwenye soko siku nyingi kabla ya Taifa gas, Taifa gas imezinduliwa awamu ya tano ilihali hao wengine walikuwepo huko nyuma.

Au labda Bei gas imepanda pale tu Taifa gas ilipoanza kuuza gas?

ndani ya mitaa ya Hodeidah Yemen
Sahihi kabisa Mkuu,

Na kama sikosei Oryx ndio gesi ghali kuliko zote. Kwanini alalamikiwe Taifa Gas ambaye hata sio expensive kuzidi Oryx?

Lake wanauza gas kibao, Manjis halikadhalika, kuna O gas nk nk.

Tatizo la nchi yetu ni kuwa na vijana wajamaa wanaodhani maskini ndio watashikilia uchumi.. haiwezekani na haitawezekana.. mbona kuna maeneo mengi vitu ni bei ghali na wala Rostam hata hafanyi biashara hizo? Mbona mabando ya Ving'amuzi yanapanda kila siku?? Kwani na kwenyewe Rostam yuko? Mbona sukari awamu ya tano ilipanda mara dufu? Na kwenyewe Rostam yupo???

Kazi kweli.
 
Back
Top Bottom