Mazungumzo ya Ndg. Polepole leo 31 Agosti 2025 na umma

Mazungumzo ya Ndg. Polepole leo 31 Agosti 2025 na umma

1. Ndugu H. Polepole leo ameanza kuelezea bei ya mtungi wa gesi wa Kilo 20 Cuba ambayo ni 2000/= TZS na kusisitiza hapa Tanzania tunapigwa na Mafisadi, huku Gesi tunayo lakini mtungi ni 60,000/= TZS. Amefanya hivyo kwa kujibu hoja za Bwana Ezekiel Kimwaga aliyemkejeli Ndugu Polepole na kusema muongo kuhusu bei halisia ya mitungi ya gesi Cuba kupitia Press yake aliyoifanya tarehe 29-08-2025.

2. Pia amelezea kuhusu Jiografia ya nchi ya Cuba, kwa kutaja Miji mikubwa, Miji ya Utalii, Miji ya Kihistoria, Balozi na maeneo nyeti ya nchi ya Cuba na huku akifafanua kwa undani kuonyesha Nchi ya Cuba anaielewa kiundani zaidi. Huku akihitaja miji kama Matanzas, Havana (La Habana), Santa Clara, Bayamo, Cienfuegos, Santiago de Cuba, Camagüey, Guantánamo na mingineyo.

3. Pia amegusia kuwa Cuba ni nchi yenye uchumi wa kijamaa (socialist economy) na ndio nchi iliyowekewa vikwazo vigumu na Nchi ya Marekani. Lakini nchi ya Cuba ndiyo rafiki mkubwa wa nchi za Afrika kutoka ukanda wa Western Hemisphere -- akisisitiza Ndugu Polepole.

4. Pia amesisitiza na kupinga vikali swala la Raisi Samia Suluhu Hassan kugombea tena awamu hii, huku akisema hakutakiwa kugombea. Huku akisema Samia akipata Uraisi hata waheshimu na kuwasikiliza raia wake.

5. Amesema Mama samia analazimisha uongozi na kwenye kampeni alipaswa kuwasema akina Salim Mwalimu ambao ndio anagombea nao, sio kuwasema Chadema ambao hawapo kwenye uchaguzi amewapiga pini na kusema wameweka mpira kwapani.

6. Amesema Tanzania ina viongozi wabaya ambao hawaelewi maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

7. Pia amegusua ujenzi wa bandari kavu ya Kwala --- huku akisema tumesha chelewa ilitakiwa iwepo miaka 5 nyuma. Huku akisema Bandari kavu inatakiwa iwepo Morogoro na Dodoma, ilikupunguza msongamano wa Malori barabarani na kuongeza mzunguko wa mapato nchini.

Next Press -->Jumatano, Saa 3:00 Usiku -----> Kaa tayari.

"Ukombozi huanza akilini"

Link Below


View: https://www.youtube.com/watch?v=Uz_tHuV_lbc​


Mrithi wa nyerere
 
hatujui kusomea barua m bahasha. KASEMA KWA HERUFI KUBWA KUBA WAMEMFUNZA MENGI. miongon mwa hayo ni kama nini?
 
hakuna mtungi wa gesi wa chini ya dola moja huko Cuba, nimeulizia chatgpt ikanipa figure moja kubwa kidogo
Polepole ameshakujibu kuhusu kutumia Ai kupata taarifa hii ya bei.
Umekimbilia kumjibu au kumkosoa kabla hujamsikiliza.
Alijua wapo watu kama wewe watakuja kuongea hivi mfano wa vile ameongea Ezekiel Kamwaga Tosa boy anaye tuaibisha schoolmates wenzake.
Ai ipo kwenye training mode. Haipo sahihi wakati wote.
 
Amesema taarifa nyengine huwezi kuzipata kwenye platform au hizo source

Yeye ameishi Cuba na kwa hadhi yake ya kibalozi alipata taarifa nyingi

Hili nalo mnataka kubishana nae?

Amesema jumatano ni balaa!!
Mkuu tujifunze kureason.

Mtu anasema gas inauzwa 2000 lakini mtu huyo hyo anakiri kwenye black market inauzwa hadi laki 3.. sasa jiulize, mtu yeyote ambaye ni Rational anaweza kununua gas ya 2000 kwenye black market kwa 300000??? Maana yake bei ya soko kwa hakika ni hiyo bei ya black market; hiyo 2000 ina ruzuku kubwa ambayo gharama yake ni kubwa hadi uiaccsess mwa hiyo bei pengine karibia na hiyo bei ya black market (ikiwemo rushwa na usumbufu)... ndiyo maana black market inauza sana.

Hiyo ni reasoning ndogo sana inayothibitisha haiwezekani gas iuzwe 2000 halafu kwenye black market iwe laki 3 na inanunuliwa... yaani sukari kg 1 Tanzania iwe 2600 halafu kwenye black market iwe 250,000??? Is it possible???? Is it rational??? Huu utakuwa uchumi gani????

Nakaribisha mjadala.
 
Sahihi kabisa Mkuu,

Na kama sikosei Oryx ndio gesi ghali kuliko zote. Kwanini alalamikiwe Taifa Gas ambaye hata sio expensive kuzidi Oryx?

Lake wanauza gas kibao, Manjis halikadhalika, kuna O gas nk nk.

Tatizo la nchi yetu ni kuwa na vijana wajamaa wanaodhani maskini ndio watashikilia uchumi.. haiwezekani na haitawezekana.. mbona kuna maeneo mengi vitu ni bei ghali na wala Rostam hata hafanyi biashara hizo? Mbona mabando ya Ving'amuzi yanapanda kila siku?? Kwani na kwenyewe Rostam yuko? Mbona sukari awamu ya tano ilipanda mara dufu? Na kwenyewe Rostam yupo???

Kazi kweli.

Uko sahihi, shida yangu kubwa Iko pale tunapowatuhumu watu halafu hatuweki clear evidence/details za kussuport tuhuma zetu bali tunataka tuaminike kwa kusema tu fulani mwizi kasema fulani.

Mbaya zaidi wanataka ukubaliane uwe oyaoya na ukihoji utaitwa majina yoote, kutukanwa nk.
Inashangaza sana kuona hawa ndio watu tunaotaka CCM itoke madarakani.

ndani ya mitaa ya Hodeidah Yemen
 
Amesema taarifa nyengine huwezi kuzipata kwenye platform au hizo source

Yeye ameishi Cuba na kwa hadhi yake ya kibalozi alipata taarifa nyingi

Hili nalo mnataka kubishana nae?

Amesema jumatano ni balaa!!
Taarifa nyingi unazipata kwenye Chatgpt na wala siyo kama anavyodhani yeye double P.

Halafu asitudanganye kwani kuna bei ya serikali na bei ya black market ambayo ni kubwa sana, na yote hayo yametolewa maelezo lakini labda kiingereza kimepita upande.

Hiyo Cuba ameishi kwa miaka mingapi hata awe anajua kila kitu kuhusu hiyo nchi? Hiyo miaka miwili
 
Amesema taarifa nyengine huwezi kuzipata kwenye platform au hizo source

Yeye ameishi Cuba na kwa hadhi yake ya kibalozi alipata taarifa nyingi

Hili nalo mnataka kubishana nae?

Amesema jumatano ni balaa!!
hana lo lote, hiyo Cuba aliyoishi kwa miaka isiyozidi miwili na nusu ndiyo amekuwa expert wa historia yake?

Labda hajui power ya AI kuhusu taarifa inazoweza kukusanya, yuko busy kuleta fitina tu.
 
Acha wivu mkuu; kila kitu sokoni kwenye uchumi kiko controlled na kuna manipulations kibao - ni jambo la kawaida kiuchumi..kabla hujamlaunu Rostam ushawahi kujiuliza ni nani anayevontroll soko la vigae Tanzania na Easr Africa nzima? Je soko la float glass?? Tena hii ni East, Central, Sadc na sasa hadi North??? Viwanda hivyo vikonTanzani.. je aoko la mabati? Wako watatu tu, ninaweza kutaja vitu kibao... je bakhresa anacontrol nini na nini? Kwa kuwa yeye hapogiwi kelele tu lakini kuna vingi alivyoshikilia na ana manipulate, vipi kuhusu Sukari?? Na kwenyewe Rostam yupo?? Acha kuingizwa kwenye vita kati ya polepole na Rostamu Mkuu, wahenga wanasema usinunue ugomvi. Biashara ya soko huria is all about controll and manipulation ndio maana dhahabu dunia nzima iko controlled na kampuni chvhe sana, mafuta yko controlled na kampuni chache sana na wanaamua lini wapandiahe bei na wapandishaje... tutafute hela tu Mkuu
Lini ulisikia serikali inafanya promosheni ya kugawa mitungi ya oryx au manjis?
 
Kweli kabisa lakini yeye anaitumia kama basis of his argument. Pia amezungumzia ration cards wanazopewa waCuba kila miezi 3, sijui anataka turudie ule ukomunist wa enzi za Nyerere na Karume?

Wenzake tulishapitia huko tukiziita kadi za ukoo.
Sawa mkuu, nimekuelewa.
 
hana lo lote, hiyo Cuba aliyoishi kwa miaka isiyozidi miwili na nusu ndiyo amekuwa expert wa historia yake?

Labda hajui power ya AI kuhusu taarifa inazoweza kukusanya, yuko busy kuleta fitina tu.
Ukisikia maji kukorogeka ndiko huku sasa. Watu hawajui nani mtetezi wao maana Sukuma gang ya pole pole hawaitaki na wahuni pia hawatakiwi, Ccm pia kuna mpasuko. Labda chauma 😂😂😂😂😂
 
Asubuhi nimemwambia huyo Mwandishi ni bomu kabisa. Anatumia google kujibu hoja wakati ana simu na Anaweza kupata facts kutoka source? Si angeenda tu hata ubalozi wa Cuba kuuliza?

Tuna Waandishi wa habari vilaza kabisa.
Cuba Serikali yao iligawa bure mitungi ya Gas ikahakikisha kila mwananchi ana mtungi wa Gas ni sehemu ya huduma kwa jamii toka serikali yao ni kama vile ilivyokuwa Elimu bure au huduma za hospital bure kule Libya enzi za Gadafi, hiyo elfu 2000 ni kuchangia huduma tu, Hilo jambo hata kwa Tanzania lingewezekana pia kwa kutumia manisipaa wangesambaza mitungi kote Nchini kisha wananchi wanachangia Gas kidogo tu, kwani pesa zinatumika kuidhoofisha chadema kuilea chauma ubwabwa ni nyingi kuliko za kuwahudumia wananchi wa Tanzania ambao wanateseka hospital hazina Dawa mashule hayana madawati vyoo vya kutosha nyumba za walimu mishahara Duni na kero nyingi lakini pesa za kumlipa Angela kiziga kwa kazi hewa zipo
 
Ukisikia maji kukorogeka ndiko huku sasa. Watu hawajui nani mtetezi wao maana Sukuma gang ya pole pole hawaitaki na wahuni pia hawatakiwi, Ccm pia kuna mpasuko. Labda chauma 😂😂😂😂😂
ibilisi wa ccm wanatumia pesa nyingi kwa mambo ya hovyo kuliko maendeleo , pesa inayoibiwa na mafisadi ni nyingi pesa inayotumika kudidimiza demokrasia ni nyingi zaidi na laiti wangetumia hizo pesa kuleta maendeleo mda huu Tanzania ingekuwa mbali kimaendeleo na ccm wangekuwa wanapata kura halali pasipo kufanya uchakachuaji wala kuwabambikia kesi za uongo chadema
 
Hili mbona siyo jipya, na nina hakika atakapo rudi kwa kutumia hizi njia za kulazimisha hali itakuwa mbaya zaidi.

Kiongozi aliye amua kujitangaza wazi kuwa hataki kusikia kelele za wananchi wake kwa kujipachika jina la "chura Kiziwi" ili asisikie malalamiko ya wananchi unafikiri atafanyaje akirudi kwa hasira nyingi baada ya kutupiwa kila aina ya maneno asiyo penda kusikia!

Inawezekana tukashuhudia jambo ambalo hatujapata kulishuhudia ndani ya nchi hii iwapo mwanamke mwenye kiburi hhuyu ataendelea kukaa madarakani kwa nguvu.
Utabiri wa marehemu Sheikh Yahya unaenda kutimia Kisha Nchimbi awe Rais kesi za ufisadi zianze kuunguruma Nchi nzima moto uwake kila kona hicho ndicho kinafuata ingawa Kikwete Rostam Angela kiziga wanufaika wa utawala wa mkoloni kaburu Dikteta toka Zanzibar wanahaha kusoma madua visomo makafara kuzuia Utabiri wa Sheikh yahya usitimie kabla hawajamaliza kuiba kila kitu kama marehemu Mabutu na Rungu wa Zambia
 
Hakika ndugu Humphrey Polepole anazidi kutoa ufafanuzi wa ukweli wa chama dola kongwe tawala badala ya kuwa cha wafanyakazi na wakulima, sasa kimetekwa nyara na kundi la mwabwanyenye wachache.
Pesa inayoibiwa inayopotea inayoporwa inayotumika kuidhoofisha kuibomoa chadema na kuilea kuihudumis Chauma Ubwabwa ni kubwa sana ni pesa ambazo zingekuwa zinatumika vizuri kuleta maendeleo mda huu ccm wangekuwa wanapendwa sana na wasingekuwa wanahangaika kuwaua kuwateka kuwabambikia kesi za uongo chadema, wangevuna kura nyingi kulingana na maendeleo siyo kuwatesa wapinzani kisha kufanya uchakachuaji huku nchi ikifirisika kwa wizi wa Rasilimali unaofanywa na Rostam Aziz Angela kiziga na Genge lao
 
Huyu anazidi kuchanganyikiwa na kukosa hoja, mara alete ya Cuba mara wapi. Mwahisheni hospitali ya wehu
Wewe ndiyo uwahishwe Hospital umechanganyikiwa acha kuvuta Bangi huko gheto la ibilisi wa ccm kisha kujiona una Akili za kuona polepole hayupo sawa wakati wewe ndiyo chizi mwenyewe
 
hili la gas naungana nae, gas imekaa kama ushuzi pyuu imeisha elfu 60 imekwenda, ndo maana vijijini hawataki kusikia stori za gas, gas inachimbwa bure songosongo kwanini sie watuuzie ndoo ya gas elfu 60, na haichakatwi kama dhahabu
Nchi zilizoendelea Gas ni huduma nafuu kwa wananchi, mabomba ya Gas husambazwa kama mabomba ya maji ni sehemu ya huduma toka Serikali kuu wananchi huchangia kiasi tu
 
Mpaka mwaka Jana march 10kg ilikua 225CUP (cuban peso) ndo bei rasmi yenye ruzuku sasa change hiyo ndo utanielewa nachomaanisha ni almost ka 23k+ huko
Huduma ya Gas kule Cuba bure hizo 2000 ni kuchangia huduma tu, wao walijipanga vizuri wakaona watoe huduma nafuu kwa wananchi wao
 
Back
Top Bottom