Pre GE2025 Mazungumzo ya Upinzani kusimamisha mgombea Urais wa pamoja 2025 yanukia

Pre GE2025 Mazungumzo ya Upinzani kusimamisha mgombea Urais wa pamoja 2025 yanukia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
so mazungumzo yawepo au yasiwepo, na ikiwa Lisu na zito watamuendorse lipumba utajiskiaje🐒
Hawa wote ni viongozi wazuri, wakichukua nchi, Lissu rais, Lipumba kwasababu ni mtaalamu wa masuala ya uchumi anapewe eneo la Uchumi wa nchi, mdogo wangu Zuberi anapewa masuala ya kimataifa, ila ila hatuna waziri mkuu. Mbowe apewe viwanda na Biashara, Cheo madini, halafu na sisi tunaanza kununua kutoka kwao maana wapo ambao ni wazuri huko.
 
Mfano kwa mujibu wa makubaliano Lipumba awe mgombea urasi, kisha wakiunda serikali Lisu mwanasheria mkuu, zito waziri wa fedha, Rungwe viwanda na biashara, mbowe uvuvi, shibuda mambo ya ndani, unaonaje hii 🐒
 
Inasemekana CHAUMMA, CHADEMA, CUF, Sauti ya waTanzania na ADA-TADEA wameanza tayari mazungumzo ya awali yasiyo rasmi.

Mazungumzo rasmi ya kimkakati yanaeledea kuwekwa utaratibu mzuri na waleta pendekezo hilo, ambao ni miongoni mwa wanasiasa na wanaharakti wa ndani na nje ya nchi.

Unadhani chama gani kitaaminiwa na wengine na kupewa ridhaa na dhamana hiyo kubwa na nzito ya kupepreusha bendera ya urais, ikiwa agenda hii ikwafanikiwa kua rasmi?

Mgombea atakuwa nani?

Kumbuka kwa upande mwingine, kuna vyama vya siasa vya upinzani pia, havitasimamisha wagombea Urais, badala yake vitamuunga mkono mgombea Urais wa chama tawala 🐒
Tunasubiri Kwa hamu ili tuwarejeshe kwao Wazanzibar
 
Mimi sioni watu serious nje ya ccm zaidi ya cdm na kama watasimamisha mgombea moja huyo mgombea lazima atoke cdm
CCM yenyewe nje ya dola haina mtu serious. Chama cha siasa kinabakia kimoja tu.
 
Tuliza mihemko na munkari sasa,

Ikitokea zitoe, lisu, rungwe na vyama vingine wameamua kumuendoserse Ibrahim Haruna Lipumba kugombea urais, utapokeaje uamuzi huu? 🐒
Siwezi kupokea kitu ambacho hakipo. Hakuna kitu kama hicho.
 
Mfano kwa mujibu wa makubaliano Lipumba awe mgombea urasi, kisha wakiunda serikali Lisu mwanasheria mkuu, zito waziri wa fedha, Rungwe viwanda na biashara, mbowe uvuvi, shibuda mambo ya ndani, unaonaje hii 🐒
Iko sawa. Ila tarizo lipumba hana ushawishi mkubwa kwa watu. Ni mzuri sana, ila ushawishi mkubwa kwa watu hana. Walikuwa na ushawishi mkubwa sana kipindi wakiwa na maalim, ila wakatengenezewa zengwe. Lipumba kichwani yupo vizuri, ila ushawishi wake umepotea kwasababu aliingizwa kingi. Halafu unasema lisu awe mwanasheria mkuu, kwasababu gani? Kuna watu wapo vizuri kwenye hiyo sekta hapo upinzani kuliko lissu. Zito kwenye Fedha sawa, ila naona kama jamaa yupo fiti zaidi kwenye Foreign Affairs. Mbowe uvuvi ? Mmmh. Nasema biashara na viwanda kwasababu kwao toka kipindi cha mangi, walikuwa wanafanya biashara. Sasa uvuvi ... Kilimanjaro na uvuvi wapi na wapi, au ndio yale mambo ya Hussen Mwinyi ambae alikuwa anasomea udactari anapewa wizara ya tofauti na professional yake, Mwinyi nilikuwa nae Muhimbili, wakati yupo na BMW yake anatutesa akiwa mtoto wa Rais. Shibuda nilikuwa nae Muhimbili pia. Huyu anafaa sana USALAMA WA TAIFA.
 
Tunamtaka Tundu Lissu, ni mtu ambae hata kwenye campaign zake tulikuwa tunamwelewa. Tofauti na Lowassa ambae alipata watu wengi kwasababu watu walikata tamaa na ccm. Ila Lissu alipambana na Jiwe wakati Jiwe akiwa ni Rais. Tena Jiwe alikuwa na ushawishi mkubwa kwa watu.
Lissu alimpeleka dhalim Magufuli mchakamchaka hadi kila wiki anawekewa drip na alipotangazwa kibabe kuwa ameshinda akatoa amri Lissu amalizwe hadi akaenda kuchukua hifadhi ubalozini. Hata huko Jehannam aliko dhalim anajua kuwa Lissu ndiye kiboko yake.
 
Iko sawa. Ila tarizo lipumba hana ushawishi mkubwa kwa watu. Ni mzuri sana, ila ushawishi mkubwa kwa watu hana. Walikuwa na ushawishi mkubwa sana kipindi wakiwa na maalim, ila wakatengenezewa zengwe. Lipumba kichwani yupo vizuri, ila ushawishi wake umepotea kwasababu aliingizwa kingi. Halafu unasema lisu awe mwanasheria mkuu, kwasababu gani? Kuna watu wapo vizuri kwenye hiyo sekta hapo upinzani kuliko lissu. Zito kwenye Fedha sawa, ila naona kama jamaa yupo fiti zaidi kwenye Foreign Affairs. Mbowe uvuvi ? Mmmh. Nasema biashara na viwanda kwasababu kwao toka kipindi cha mangi, walikuwa wanafanya biashara. Sasa uvuvi ... Kilimanjaro na uvuvi wapi na wapi, au ndio yale mambo ya Hussen Mwinyi ambae alikuwa anasomea udactari anapewa wizara ya tofauti na professional yake, Mwinyi nilikuwa nae Muhimbili, wakati yupo na BMW yake anatutesa akiwa mtoto wa Rais. Shibuda nilikuwa nae Muhimbili pia. Huyu anafaa sana USALAMA WA TAIFA.
nadhani unafahamu kuhusu career development Lazima uzingatiwe unless hamna lengo moja....
Lakini pia, kwenye makubaliano na mgawanyo wa wengi , suala la kupewa jukumu la fani ulosomea au unalolipenda nadhani ni vigumu sana kulitekeleza . Yaafaa utakalo pewa ndilo la kufanya...

vp ikiwa makubaliano ni for one term presidency, yaani kupokezana urais kutoka chama kimoja kwenda kingine, unaonaje hii?🐒
 
we mwanafunzi wa siasa ndio unasema hakipo 🐒
Itoshe tu kusema kuwa kama mimi ni mwanafunzi wa siasa basi wewe bado ni yai kabisa kwenye siasa hata hatua ya kuwa kifaranga bado. Huu uchawa unawafanya mjione mko daraja la juu sawa na hao mnaowachawia. Umenichekesha hadi karibu hii whisky yangu inipalie.
 
nilitaka nishangae aise,

yaani uandishi huu pasiwepo msukumo wa chochote kweli?🐒

hatimae umeweka wazi mwenyewe kumbe najadiliana na whisky dah 🐒
 
nilitaka nishangae aise,

yaani uandishi huu pasiwepo msukumo wa chochote kweli?🐒

hatimae umeweka wazi mwenyewe kumbe najadiliana na whisky dah 🐒
Si bora whisky kuliko hicho kisungura kinachokufanya ujione umekuwa tai kumbe wewe ni shorwe tu.
 
Si bora whisky kuliko hicho kisungura kinachokufanya ujione umekuwa tai kumbe wewe ni shorwe tu.
ndiyo nini hivyo vitu?
si mnavijua ninyi wapiga vyombo tu,

Kwan had sisi tunahusika kujibust na mawisky ndio tunachangia mada 🐒
 
Inasemekana CHAUMMA, CHADEMA, CUF, Sauti ya waTanzania na ADA-TADEA
Umetumwa kazi usiyo iweza.
"Inasemekana" toka wapi/kwa nani?

Mbinu za kutaka kuswaga watu kwenye kundi ili mtu wenu apate pa kupenyea hamtaipata ng'o!

Hivyo vikura mnavyo vitegemea kwenye makundi maalum vitagawanywa kwenye vyama hivyo na kumwacha mtu wenu mtupu!

Nenda katafute mbinu nyingine.

Kwa kawaida huwa sijisumbui na hizi takataka zako, lakini nimeona nikupe chai ya moto kidogo kwa huu ujinga hapa.
 
Chauma tutasimama na Rungwe,labda kwenye muungano huo asimame Rungwe 😀😀.

#Ubwabwa time
 
C tulikubaliana hivyo vyama vingine n CCM-B 😎
 
Back
Top Bottom