Get the facts right, mmiliki wa Channel Ten ni Shabbir Abji, yule mwenye New Africa Hotel na washirika wake akiwemo Tanil Somaiya na sio Rostam Aziz, Rostam yeye anamiliki New Habari ambayo nayo iko hoi!.
Mmiliki wa kwanza wa Channel Ten ikiitwa DTV alikuwa Shabir Dewji na mdogo wake Murtaza Dewji, wakaiuza kwa Mtaliano Franco Tramonatana akaibadili kuwa Channel Ten ndipo akataka kuiuza na mnunuzi wa mwanzo alikuwa ni Mzee Reginald Mengi, TCRA wakazuia kwa hoja kuwa tayari anamiliki vituo vitatu vya TV, ITV, EATV NA Capital TV, Vituo 3 vya Redio, Radio One, EARadio na Capital FM, na magazeti zaidi ya 10, The Guardian, Nipashe, The Financial Times, Kulikoni, Lete Raha, Alasiri, ambayo yako chini ya kampuni ya The Guardian Limited, pia kuna magazeti chini ya kampuni ya Media Solution na shirika la habari la PST, hivyo akakataliwa, ndipo Shabbir Abdji aliyekuwa anamiliki kituo cha CTN akainunua na kuinganisha.
Hivyo Mengi hawezi tena kutaka kuinunua unless TCRA wamebadili kanuni.
P