Tetesi: Mazungumzo yaanza Bakhressa kuinunua Channel Ten

Tetesi: Mazungumzo yaanza Bakhressa kuinunua Channel Ten

Nadhani sababu ziko wazi sana kwa sasa, nitajaribu kuziweka hapa.
1/Umiliki wa chombo cha habari kwa sasa ni jambo la hatari kimaisha na kibiashara kwa mmiliki mwenyewe.
(Watawala wanaweza kumuandama mmiliki katika maisha yake yake ya kila siku kutokana tu na habari wasioipenda kurushwa katika kituo chake. Mzee Mengi analijua sana hili).

2/Biashara ya matangazo imedorora sana kwenye vituo vingi.
(Makampuni mengi makubwa ya kibiashara yamedorora sana kwa sasa, hayaoni tena umuhimu wa kuendelea kutumia pesa nyingi kufanya promotion za biashara zao kwao nguvu ya manunuzi kwa watanzania umeshuka kwa zaidi ya 50% ukilinganisha na hapo kabla).

3/Hakuna tena uwezekano wa chombo cha habari kwa sasa kuweza kutengeneza Brand yenye nguvu kupitia habari na mijadala huru ili kujenga Huge Capital Bundle width viewer ili uwe ndio mlango wa kuvuta matangazo ya biashara yenye pesa nyingi.

4/Gharama za uendeshaji ni kubwa mno kwa sasa kwa vyombo vya habari. (Kodi imekuwa msumari wa moto, makato ya TCRA nk vinawaumiza wamiliki).

5/Vyombo vya habari vimekuwa vingi mno, na watazamaji wamepungua sana, wako busy na mitandao zaidi.
Ndo maana kazi ya redio ndogondogo hizi zimebaki kupiga miziki kutwa nzima maana ni uchuro tu
 
Nakumbuka kipindi hicho Msiba na Ores Kawawa (OK) wakichambua soka channel ten, maisha yanaenda kasi sana, sasa Msiba naona ndo kasharukwa akili kabisa
 
Bora aiuze tu,a ukiangalia chanel 10 unajua kabisa kuna kitu hakiko sawa,either wafanyakazi hawalipwi mishahara au haina wafanyakazi at all,unaweza kuwa unatazama habari,mtangazaji anasema "ngoja tuungane na mwandishi wetu alieko mahakamani kwa taarifa zaidi" lkn cha ajabu inakuja habari ya nzige kushambulia shamba la mahindi Rukwa,na hali hii huwa sio siku moja ila ni Kila siku
Ha ha ha ha ha haaa
 
MBAVU ZETU...

Ahahahahaaaaaas....!!
 
Back
Top Bottom