Nadhani sababu ziko wazi sana kwa sasa, nitajaribu kuziweka hapa.
1/Umiliki wa chombo cha habari kwa sasa ni jambo la hatari kimaisha na kibiashara kwa mmiliki mwenyewe.
(Watawala wanaweza kumuandama mmiliki katika maisha yake yake ya kila siku kutokana tu na habari wasioipenda kurushwa katika kituo chake. Mzee Mengi analijua sana hili).
2/Biashara ya matangazo imedorora sana kwenye vituo vingi.
(Makampuni mengi makubwa ya kibiashara yamedorora sana kwa sasa, hayaoni tena umuhimu wa kuendelea kutumia pesa nyingi kufanya promotion za biashara zao kwao nguvu ya manunuzi kwa watanzania umeshuka kwa zaidi ya 50% ukilinganisha na hapo kabla).
3/Hakuna tena uwezekano wa chombo cha habari kwa sasa kuweza kutengeneza Brand yenye nguvu kupitia habari na mijadala huru ili kujenga Huge Capital Bundle width viewer ili uwe ndio mlango wa kuvuta matangazo ya biashara yenye pesa nyingi.
4/Gharama za uendeshaji ni kubwa mno kwa sasa kwa vyombo vya habari. (Kodi imekuwa msumari wa moto, makato ya TCRA nk vinawaumiza wamiliki).
5/Vyombo vya habari vimekuwa vingi mno, na watazamaji wamepungua sana, wako busy na mitandao zaidi.