Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Eneo la Mbagala lililomo kwenye wilaya ya Temeke ni eneo chafu sana sana, ili uweze kuelewa ninachokisema kabla haujanipinga ni vizuri utembelee eneo la Rangitatu nina uhakika hata hizo Rangitatu hautaziona kutokana na uchafu ulioko huko.

Mbagala ina barabara kuu ya Kilwa japo kote inaonekana safi ila ukifika Mbagala inatoweka kwa uchafu na unaiona tena ukiivuka Rangitatu! Mitaa yote ya Rangitatu ambalo ndilo eneo la biashara ni michafu na yenye vumbi na mashimo na ndiyo inayozalisha kura za ushindi wa ubunge kwa CCM huku wanyamwezi ardhi kama hiyo wanazalisha viazi vitamu.

Rangitatu kuna maduka yanauza nafaka ambazo humwagika na zikilowa huchacha na kusababisha harufu kali na joto linalotokana na pumba za mahindi zilizolowa, Mbagala ni chafu na inachangiwa zaidi na Serikali kuruhusu wamachinga kujazana barabarani wakifanya biashara na kukojoa hovyo kwani hakuna vyoo vya jiji licha ya jiji kukusanya kodi ya maendeleo na kutofanya usafi!

Tahadhari, usije Mbagala wakati wa mvua.
 
Mbagala mbona haijaanza Leo kusemwa ni chafu
 
Hata vyakula vya ovyo unaweza kulishwa huko sijui nyama ya chura, kenge, panya, nguruwe yaani Pako ovyo kinoma, nyumba hazina ustaarabu, kukabwa nje nje Tena hata saa Saba.
 
Viongozi wote wa CCM wameitelekeza, si mbunge, mkuu wa wilaya wala mkuu wa mkoa wanaiogopa Mbagala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…